Kwa nafasi aliyonayo waziri mkuu hakupaswa kutoa kauli kama hii.
Kauli hii inaonyesha picha kubwa kuwa;

1. Serikali ya CCM imeishiwa kabisa pumzi kuhusu kutatua tatizo la ajira kwa wasomi waliozagaa mitaani na vyeti.

2. Elimu ya chuo kikuu kwa sasa kwa sehemu kubwa haina maana yoyote kuweza kumkomboa kijana kiuchumi na kijamii.

3. Kijana wa kitanzania anayepambana kusoma mpaka kuhitimu chuo kikuu basi anapoteza tu muda, nguvu, akili na rasimali, maana elimu hiyo haina maarifa ya kuweza kumkomboa kimaisha.
 
Aanze mwanaye kusoma huko.
 
Yeye Majaliwa anawaza tu kugombea ubunge tena

Anaogopa mno Makonda kugombea ubunge utafikiri hatakuwa na mafao ya kudumu asipogombea ubunge

Hakuna watu waoga maisha mtaani kama.mawaziri hawa wawili Majaliwa na Lukuvi
 
Haya ndiyo madhara ya kuchagua viongozi wasio na maono.
Kuna haja gani sasa ya kusomesha watoto wetu hadi vyuo vikuu halafu wakimaliza masomo yao inabidi waende tena veta kupata ujuzi(sawa na wanafunzi wa darasa la saba)?
 
Tayari sasa hivi madogo WKitoka form 4 wanaenda vyuo kupewa Elimu practical, baadhi ndio wanaenda 5 na 6
 
Mkuu hakuna ugomvi kwa Waziri Mkuu Majaliwa wala mleta hoja na wachangiaji.
Majaliwa kaleta UFUNUO wa ajira.

Tusibeze kwa kuwa kuna wakati elimu ya aina fulani haileti chakula mezani.
Barabarani usiku unakuta biashara ya ngono na watu wenye hata degree ya ualimu.
Bahati nzuri siku hizi kupata maarifa sio lazima uende shule au chuo ukalili miaka kadha halafu wakupe cheti,ambacho wakati mwingine utasota hata miaka kadhaa bila ajira.
Jibu la msingi ni kufanya kazi itayokupa mkate regardless of what.
Ni wakati wa kutafakari elimu na mafunzo yatolewayo kama yanaendana ma wakati wa leo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…