#COVID19 Waziri Mkuu Majaliwa: Zoezi la chanjo ya Uviko-19 limefikia zaidi ya asilimia 80


Ukiona hivyo ujue wanaopinga hilo kwa nguvu zote ni hao hao ambao hawawezi waka survive kwenye fair system.

Sasa wanatumia lolote hata kwa kupotosha tu, kama itawasaidia kuendelea kuwapo.

Hawana uchungu wowote na nchi wala watu, bali matumbo yao.
 
Sawa! Ila mbona hatusikii taarifa za vipimo? Mwatoa chanjo na wananchi hawapimwi! Hivyo vipimio mmetia kibindoni!??
Huu ni usanii wa hali ya juu.!

Sent from my SM-A115AZ using JamiiForums mobile app
 
80% ya chanjo 1m zilizopo ni sawa lakini ya chanjo ni tungo tata
Exactly yaani asilimia ya chanjo zilizopokelewa lakini siyo asilimia ya idadi ya watu wanaohitajika kupata chanjo. Mfano Rwanda wamevuka zaidi ya asilimia 40 ya raia wake...
 
Mahakama ndio kila kitu
Tumwache siro astaafu kwa amani

Kuchagua kustaafu kwa amani ni kama kutaka kuvuna dengu.

Kila mtu huvuna anachopanda.
 
Exactly yaani asilimia ya chanjo zilizopokelewa lakini siyo asilimia ya idadi ya watu wanaohitajika kupata chanjo. Mfano Rwanda wamevuka zaidi ya asilimia 40 ya raia wake...

Haiko KIMKAKATI zaidi?
 

Kwahiyo unambishia kiongozi wa kitaifa si ndio
 
Maria Sarungi kule Jamhuri ya Twitter anasemaga hawa viongozi wanakabiliwa na 'credibility gap'. Kwa kimasai unaweza kusema 'wamepoteza uaminifu'.

Watanzania wana desturi ya kuwaamini viongozi wao sana ila hakuna wakati katika historia ya nchi hii wananchi wameikaidi serikali yao waziwazi kama wakati huu wa zoezi la chanjo. Nadhani kampeni za uchaguzi wa 2020 unafuatia.
 
Kichupa kimoja Cha chanjo unajua Watu wangapi wanachomwa?
 
Safi sana!! Maana hakuna namna nyingine! Ni suala la kauli tu, tumesema zimeisha na kauli hiyo ni ya mwisho!! Beberu kama hauamini shauri yako! Maana tukisema tusubiri hadi ziishe kweli tutasubiri sana!! Suluhisho ni kutamka kauli tu biashara inaishia hapo!!!
 

Kama kutamka mheshimiwa yuko busy na mafaili ofisini? Kwamba mnataka kumwona magomeni au kariakoo?

Yumkini angali busy.

Uongo ni kipaji.
 
Waziri mkuu anashusha heshima kwa Wananchi kwa kusema uongo Kila muda.Nakumbuka Treni ya umeme kutoka dar to Moro alisema itaanza kazi 2019 hadi Sasa hivi hakuna kitu.Juzi msrmaji wa serikali kasema waliochanja ni laki 4 na doz zipo milion na point ambayo ni kama asilimia 40 ya chanjo sasa hizo asilimia 80 zimetoka wapi?Tafafhali Mheshimiwa Taifa linakuamini hivo TUNAKUOMBA uwe unasema ukweli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usiseme ni uwongo. Wewe kutochanja, usidhani wote hawajachanjwa.

Jana nimeongea na ndugu yupo kijijini. Anasema zilipoletwa walichanja watu 6 tu, lakini baada ya Paroko wa RC, wachungaji wa KKKT na Anglikana kuwahuburia waumini wao Jumapili iliyopita, mpaka kufikia jana, chanjo zote zilizopelekwa katani zimekwisha, na wameomba nyingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…