Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Nne, Mizengo Pinda, amesema maandamano yaliyotokea Oktoba 29 hayakuwa ya amani, akieleza kuwa baadhi ya Vijana walishiriki bila kupata maelekezo sahihi, hali iliyosababisha mipango ya kuharibu mali na miundombinu ya umma pamoja na kuvuruga amani ya nchi.
Ameyasema hayo wakati wa sherehe za Mwaka Mpya zilizofanyika katika Shule ya Sekondari Mizengo Pinda, iliyopo nyumbani kwake Kibaoni, Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe, mkoani Katavi.
Katika hafla hiyo, Waziri Mkuu mstaafu alijumuika na ndugu, jamaa, marafiki pamoja na taasisi mbalimbali za Serikali na zisizo za kiserikali.
Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Kayanza Peter Pinda aliiasa jamii kuwapatia Watoto wao malezi bora ili kujenga jamii na Taifa lenye Vijana waadilifu, waliostaarabika na wenye uzalendo, ambao hawawezi kujihusisha na vitendo vinavyoweza kuligawanya Taifa.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Abdulmajid Mwanga, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi, amesema Serikali inaendelea kubaini na kuibua fursa mbalimbali za maendeleo mkoani humo.
Amesema miongoni mwa miradi inayoendelea ni utekelezaji wa ujenzi wa barabara ya Sitalike-Kibaoni kwa kiwango cha lami, mradi ambao hapo awali ulikuwa umesimama kwa miaka mingi na kusababisha adha kubwa katika usafirishaji wa mizigo na abiria.
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo wamesema ujumbe uliotolewa na Waziri Mkuu mstaafu umejikita katika kuliponya na kuliunganisha Taifa kufuatia machafuko yaliyotokea Oktoba 29, 2025.