PostGE2025 Waziri Mkuu Mstaafu, Pinda: Maandamano gani ya kuchoma Nyumba za Watu?

PostGE2025 Waziri Mkuu Mstaafu, Pinda: Maandamano gani ya kuchoma Nyumba za Watu?

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Tarehe 29 Kuna watu wengi waliuawa hata hawakuwa kwenye maandamano, Tatizo linaanzia japo.
Damu za watu wengi wasiokuwa na hatia zilimwagwa, tatizo liko hapo.
Walianza 'waandamanaji' kutoka na kufanya vurugu au vilianza vyombo vya usalama kufyatua risasi?
Hivi ni kweli ha
 
Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Nne, Mizengo Pinda, amesema maandamano yaliyotokea Oktoba 29 hayakuwa ya amani, akieleza kuwa baadhi ya Vijana walishiriki bila kupata maelekezo sahihi, hali iliyosababisha mipango ya kuharibu mali na miundombinu ya umma pamoja na kuvuruga amani ya nchi.

Ameyasema hayo wakati wa sherehe za Mwaka Mpya zilizofanyika katika Shule ya Sekondari Mizengo Pinda, iliyopo nyumbani kwake Kibaoni, Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe, mkoani Katavi.

Katika hafla hiyo, Waziri Mkuu mstaafu alijumuika na ndugu, jamaa, marafiki pamoja na taasisi mbalimbali za Serikali na zisizo za kiserikali.

Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Kayanza Peter Pinda aliiasa jamii kuwapatia Watoto wao malezi bora ili kujenga jamii na Taifa lenye Vijana waadilifu, waliostaarabika na wenye uzalendo, ambao hawawezi kujihusisha na vitendo vinavyoweza kuligawanya Taifa.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Abdulmajid Mwanga, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi, amesema Serikali inaendelea kubaini na kuibua fursa mbalimbali za maendeleo mkoani humo.

Amesema miongoni mwa miradi inayoendelea ni utekelezaji wa ujenzi wa barabara ya Sitalike-Kibaoni kwa kiwango cha lami, mradi ambao hapo awali ulikuwa umesimama kwa miaka mingi na kusababisha adha kubwa katika usafirishaji wa mizigo na abiria.

Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo wamesema ujumbe uliotolewa na Waziri Mkuu mstaafu umejikita katika kuliponya na kuliunganisha Taifa kufuatia machafuko yaliyotokea Oktoba 29, 2025.

Huwezi kuponya taifa hili bila kufanyia mabadiliko ya tume ya uchaguzi na kuacha kusaidia kuwaibia ccm kura. Hayo mengine wanayosema ni porojo tu.
 
Kujipa.majina ya kijamii eti MKULIMA

Muuaji mkubwa huyo na wenzake
 
Huwezi kuponya taifa hili bila kufanyia mabadiliko ya tume ya uchaguzi na kuacha kusaidia kuwaibia ccm kura. Hayo mengine wanayosema ni porojo tu.

..Mzee Pinda anaangalia vijana walioandamana, na kuharibu mali.

..Vipi kuhusu vijana waliouwa waandamanaji utadhani wanauwa wanyama?

..Vijana walioko kwenye vyombo vya dola, wanaoteka, kutesa, na kupoteza, hao Mzee Pinda hakuwagusa kabisa.
 
Hayo siyo maandamano ya warsha na makongamano!!

Ni wapi maandamano ya amani yalileta mabadiliko Afrika??

Lugha inayoeleweka zaidi ndiyo inayotumiwa kufikisha ujumbe!!
 
Tupo wepesi kuwa waangalizi na kusoma ripoti

Mheshimiwa Mohammed Chande Othman, Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania, kuwa Kiongozi wa Misheni ya Uangalizi ya Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC - SEOM)

12 November 2024
kutoka
Port Louis, Republic of Mauritius

Jaji mkuu mstaafu Chande akisoma Taarifa ya Awali ya Mkuu wa Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa SADC (SEOM)

View: https://m.youtube.com/watch?v=1_-jMi1uGxw
Taarifa ya Awali ya Mkuu wa Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa SADC (SEOM) kwenye Uchaguzi wa Bunge la Jamhuri ya Mauritius, Mheshimiwa Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa zamani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyotolewa huko Port Louis, Mauritius tarehe 12 Novemba 2024.
 
Pinda alivyotimba ndani ya uchaguzi wa Botswana kama mwangilizi, yakwetu tunaruka kimanga hatuwataki :

TOKA MAKTABA:
Gaberone, Botswana
23 October 2024

MHESHIMIWA PINDA AKUTANA NA KATIBU MTENDAJI WA SADC JIJINI GABORONE​

Mkuu wa Missoni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Africa (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda (kulia) akisalimiana na Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Mhe. Elias Magosi walipokutana jijini Gaborone, Botswana, kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Said Shaib Mussa.
 
KUPIGA RISASI WAANDAMANAJI ILI KUBAKI MADARAKA KUPITIA UCHAGUZI HARAMU

TOKA MAKTABA:
25 Julai 2025

Comrade Mizengo Pinda kuiwakilisha CCM katika Kongamano la Vyama Vya Ukombozi​

MADA : KULINDALI MAFANIKIO YA VYAMA VYA UKOMBOZI BAADA YA UHURU, VINAENDANA NA HAJA YA VYAMA HIVYO KUBAKI MADARAKANI
1767363956541.jpeg

Picha maktaba : Mizengo Peter Kayanda Pinda

African National Congress (ANC) itakuwa mwenyeji wa Kongamano la Kilele cha Vyama vya Ukombozi 2025 katika Hoteli ya Radison Blu, Kempton Park kuanzia leo tarehe 25 hadi 28 Julai 2025 chini ya mada: "Kulinda Mafanikio ya Ukombozi, Kuendeleza Maendeleo Jumuishi ya Kijamii na Kiuchumi, Kuimarisha Mshikamano wa Afrika."

Mkutano huu muhimu unathibitisha misingi ya kiitikadi ya vyama sita vya ukombozi Kusini mwa Afrika - ANC, MPLA, SWAPO, FRELIMO, ZANU-PF na CCM - na jukumu lao la kihistoria katika kupata uhuru, utu na maendeleo katika eneo lote la Kusini mwa Afrika.

Pia Kongamano linalenga kusisitiza umuhimu wa harakati hizi kuwa katika mpangilio unaotambua mabadiliko ya mazingira ya kisiasa na kimataifa yanayobadilika haraka.

Vyama vya ukombozi vya Kusini mwa Afrika vilibadilisha hali ya kisiasa ya eneo hilo, kupinga utawala wa kikoloni na ubaguzi wa rangi, na kukaribisha utawala unaozingatia watu.

Tangu uhuru, vuguvugu hizi zimetekeleza sera muhimu kuhusu mageuzi ya ardhi, elimu, makazi, miundombinu na ulinzi wa kijamii.

Hata hivyo, mafanikio haya sasa yanakabiliwa kumegeka kutokana shinikizo jipya la mataifa ya kibeberu, migogoro ya kiuchumi, na majaribio ya kuingiliwa na ukoloni mamboleo.

Mkutano huu unatoa jukwaa moja la kukabiliana na matishio haya na kujumuisha majibu ya kimaendeleo ya kikanda yanayokitwa katika Pan-Africanism (Umajimuhi wa Kiafrika), internationalism na multilateralism.

Mkutano huo ni uingiliaji wa kimkakati katika uanzishaji upya wa mpango kazi (framework), kuimarisha mshikamano wa ndani ya chama, na kurekebisha harakati za ukombozi na matarajio ya kijamii na kiuchumi ya kizazi kipya.

ANC inaamini kwamba uhai wa kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni wa urithi wa ukombozi wa Kusini mwa Afrika unahitaji kuchunguzwa kwa uaminifu, ukweli, kujifunza kwa pamoja na umoja unaoweza kutekelezeka.
Mkutano huo utaendeleza mifumo ya ushirikiano kati ya vyama, ushirikiano wa kikanda, ushirikishwaji wa vijana, na utawala huru wa rasilimali.

Kupitia kuthibitisha tena maadili ya pamoja na kuimarisha ushirikiano, Kongamano la Vyama la Ukombozi 2025 utapanga njia mpya ya kusonga mbele, ambayo inalinda mafanikio ya zamani huku ikijenga mustakabali wa Afrika wenye haki, jumuishi na unaojiamulia.

Vyombo vya habari vinashauriwa kuzingatia yafuatayo:
Wajumbe wameanza kuwasili leo, Alhamisi, tarehe 24 Julai 2025 na Wakuu wengi wa Wajumbe watawasili kesho Ijumaa, tarehe 25 Julai 2025. Watatua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Reginald Tambo, Wanaowasili Kimataifa,.

Wakuu wa Ujumbe :

  • Cde. Mizengo Kayanza Pinda, Head of Delegation, CCM, Tanzania
  • Cde. Chakil Aboobacar, Katibu Mkuu, FRELIMO, Msumbiji
  • Cde. Mara Baptista Quiosa, Naibu Rais, MPLA
  • Cde. Sophia Shaningwa, Katibu Mkuu, SWAPO
  • Cde. Obert Mpofu, Katibu Mkuu wa ZANU-PF
  • Cde. Liu Jianchao, Kamati Kuu ya CPC (IDCPC), Chama cha Kikomunisti cha China (CPC)
  • Cde. Mohamed Yeslem Beisat, Mkuu wa Ujumbe, Polisario Front
  • Cde. Jibril Rajoub, Katibu Mkuu, Harakati ya Ukombozi wa Kitaifa ya Palestina - FATAH
  • Cde. Solly Phetoe, Katibu Mkuu wa COSATU
  • Cde. Solly Afrika Mapaila, Katibu Mkuu, SACP
  • Cde. Mike Soko, Katibu Mkuu wa SANCO
  • Cde. Apa Poe, Katibu Mkuu, PAC
The African National Congress (ANC) will host the 2025 Liberation Movements Summit at the Radison Blu Hotel, Kempton Park from the 25th to 28th of July 2025 under the theme: “Defending the Liberation Gains, Advancing Integrated Socio-Economic Development, Strengthening Solidarity for a Better Africa.”
Source : https://www.anc1912.org.za/liberati...ng-the-gains-confronting-the-future-together/
 
Car number T
 
Attachments

  • 20260102_172307.jpg
    20260102_172307.jpg
    25.8 KB · Views: 20
Huyu Mzee ni mjinga kitambo.
Hakuna nyumba ya binadamu ilichomwa,zilichomwa nyumba za wanyama wauaji na wanaowaunga mkono wauaji.
 
Back
Top Bottom