Kamukhm
JF-Expert Member
- Aug 30, 2015
- 2,801
- 4,216
Unahitaji msongamano kukuza biashara... Controlled population density... Na hiyo inakuwa kihesabu.. biashara zinahitaji watu.. kama hakuna watu unadhani utauzia miti bidhaa!?Kunakutanua fursa na kubana fursa,,kimsingi mgomo wa jana umesababishwa kwa kiasi kikubwa na wenye maduka mjini wakiamini biashara zimeshuka kutokana na abiria kutoshushwa stendi ya mjini,,wenye magari waeunga mkono kuupa mgomo nguvu.
Kuhusu maduka yote kufungwa sio kweli,,ila kwa katikati ya mji kulikuwa na maduka machache wazi mfano kwa Abbas na kwa Mohamed na mitaani maduka mengi yalikuwa wazi,
Hoja yao kubwa ni magari kuingia mjini,,binafsi siafiki kwa sababu inapelekea msongamano usio wa lazima na watu wanaongezeka baada ya miaka mitano mbele wanaopinga wataelewa.
Kubwa na eneo dogo kutafanya biashara kubwa chache na zenye tija.. kwann uwe na huduma zimeachanaaana wakati hazina tija?
Jenga mji unaohamasisha watu kutembea.. mdogo wenye watu wengi. Ndio matumizi sahihi ya miji.
Shida yetu barabara hazijengwi kumpa pedestrian uhuru.. hakuna parking za uhakika.. hatupangi matumizi kwa kuzingatia miundombinu.. hakuna mji wa watu laki mbili ukawe na stand km 10 Way!?
Watu laki mbili wanatakiwa wakae kwenye maximum ya 30-40 Km Square kama tunajenga horizontally... Ambayo ni sawa na square ya urefu wa kilomita 8 na upana wa kilomita 5.
Hiyo 40sqm ni sawa na Mita za mraba 40,000,000, sawa hekta 4000, ambazo ni ekari 10000, na zinaweza kutoa viwanja vya ujazo wa kati (medium density) 50,000, maeneo ya huduma na barabara za kutosha..maeneo ya wazi na michezo.
Kwa Tanzania tunaamini familia/kaya moja ina watu watano.. ikiwa kila kiwanja kitakuwa na kaya moja.. basi hili eneo litaleta jumla ya watu 250,000/ kirahisi.. ukiweka makazi ya watu wengi, apartments, high-rise, extended family homes, kupangisha kinyemela.. eneo hili linaweza kuongeza idadi almost mara mbili.. kufikia Watu laki tano hadi milioni.
Watu wakiongezeka kwenye eneo dogo, faida yake Miundombinu midogo au michache inasave watu wengi.. kilomita moja inasave watu wengi kuliko kujenga kilomita kumi kwenda stand wakati Sehemu kubwa ya barabara inapita mashambani.. kilomita moja ya bomba, kilomita moja ya waya ya umeme, nguzo, fiber, shule chache zinafikika na wengi.. madaraja machache, maeneo ya wazi machache , masoko.. ofisi za mitaa na kata.. faida ni lukuki.
Na thamani ya ardhi inakuwa sana.. na kuwaondoa watu kwenye umasikini.