Waziri Mkuu: Wanaolalama kupata ongezeko la 20,000 ni wale wenye mishahara mikubwa

Waziri Mkuu: Wanaolalama kupata ongezeko la 20,000 ni wale wenye mishahara mikubwa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Waziri Mkuu, Kasimu Majaliwa amesema wengi wanaolalamika kupata ongezeko dogo la mishahara ni wale ambao wana mishahara mikubwa. Ametolea mfano wa mawaziri kuwa wako baadhi ambao ongezeko lao ni 0.02%

Amewaomba watumishi kuwaamini viongozi wa vyama vya wafanyakazi. Amesema wengi waliopata ongezeko kubwa ni wale watumishi waliokuwa wanapata mishahara midogo.

Pia amesema wananchi wanapaswa kushukuru kwa ongezeko hilo ambalo miaka kadhaa iliyopita haikuwepo
 
Mshahara wa milioni moja na point kwa mwezi ndiyo kwake anauita mshahara mkubwa! Na hapo bado huyo mfanyakazi hajakopa ili ajenge kibanda cha kumuhifadhi! Maana hakai kwenye nyumba ya serikali kama yeye Waziri mkuu! Hana deni Bodi ya mikopo!

Kweli alieyeshiba hamjui mwenye njaa. Ifikie wakati Wagombea binafsi waruhusiwe ili tupate watu wenye mawazo ya kitajiri, na hivyo kuachana kabisa na hawa watu wenye mawazo ya kimaskini na kibinafsi miaka nenda.
 
Tusiwafanye watumishi kuwa mazuzu na vyama vya wafanyakazi wasiburuzwe kizembe!

Binafsi mkewangu aliye mwalimu kaongezwa 3.7% ya mshahara wake sasa waeleze ukweli sio blah blah za kisiasa kutafuta masifa yasiyo stahili. Nchi za wenzetu walitangaziwa percentage ya nyongeza na ikatimizwa bila makelele sisi wanasiasa wanawazuga watumishi nakuleta janjajanja na maneno meeengi kisa nini!!! Kwanini nchi hii inaujinga mwiiingi? WHY?

Serikali iwe open na ifanye kazi kisomi na kistaarabu bila hila.
Swali, mishahara imeongezwa kwa asilimia ngapi?

Kama viongozi serikalini nao hawajui waseme waache kudanganya wafanyakazi kama watoto!!
Kama kipindi marehemu anaumwa mtu huyu alijitokeza na kudanganya wananchi kuwa haumwi yuko kazini mpaka kifo kilipowaumbua atashindwa nini kudanganya wafanyakazi kuhusu mishahara??? Sijawahi kumuamini huyu katelephone!! Aende akadanganye watoto wake, wafanyakazi ni wasomi na welewa kuliko yeye...SHAME!! asifanye tumwite MR. BIG LIER
 
Tusiwafanye watumishi kuwa mazuzu na vyama vya wafanyakazi wasiburuzwe kizembe!!! Binafsi mkewangu aliye mwalimu kaongezwa 3.7% ya mshahara wake sasa waeleze ukweli sio blah blah za kisiasa kutafuta masifa yasiyo stahili. Nchi za wenzetu walitangaziwa percentage ya nyongeza na ikatimizwa bila makelele sisi wanasiasa wanawazuga watumishi nakuleta janjajanja miiingi.
Wawe open mishahara imeongezwa kwa asilimia ngapi??? Kama nawao hawajui waseme waache kudanganya wafanyakazi kama watoto
BInafsi sijaelewa mishahara ya mawaziri imeingiaje ingiaje kwenye ishu ya mishahara ya watumishi wa umma, katelephone ni changamoto sana
 
Yule aliyekuwepo hakuongeza mishahara lakini miundombinu ilijengwa. Huyu wa sasa haieleweki fedha inaenda wapi
tena yule ni bora kuliko huyu, yule alipunguza PAYE ambayo iliongeza mshahara kiasi cha kutosha, huyu anashauriwa vibaya na walamba asali kina mwigulu, huku danganya toto nyongeza ya shahara huku unaongeza mitozo kila pahala ili mradi tu kumkera mwananchi, ee Mungu eee tumekuachia baba! amua na huu ugomvi
 
tena yule ni bora kuliko huyu, yule alipunguza PAYE ambayo iliongeza mshahara kiasi cha kutosha, huyu anashauriwa vibaya na walamba asali kina mwigulu, huku danganya toto nyongeza ya shahara huku unaongeza mitozo kila pahala ili mradi tu kumkera mwananchi, ee Mungu eee tumekuachia baba! amua na huu ugomvi
PAYE kwani imeongezeka??
 
Back
Top Bottom