Waziri Mkuu: Wanaolalama kupata ongezeko la 20,000 ni wale wenye mishahara mikubwa

Kwa hiyo anatuambia kwamba walokuwa wanalalamikia nyongeza ndogo ya mishahara ni mawaziri siyo? Hovyo kabisa
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 

Lakini ukumbuke hiyo increment hata kama ni laki ni kwa mwaka siyo kwa mwezi! Ongezeko la mshahara ni kwa mwezi, kwa mfano aliyeongezewa 20,000/- kwenye mshahara mpya ina maana kwa mwaka ana 240,000/-
 
Huyu nikimwona kama kiongozi wa kutufaa hapo baadaye. Kumbe ni walewale. Sijui ni hofu ya yaliyompata Ndugai!
 
Mr Pm miaka iliyopita serkali si ni ile ile?Hata hivyo wafanyakazi wamapasa kushukuru
 
Mnaonaje na wanasiasa wapewe mishahara kulingana na kiwango Chao cha elimu aliyonayo?hata Kama anacheo gani serikali ili heshima iwepo na tuache kuwaumiza zaidi walipa Kodi wazalendo wa Nchi ? maana wanasiasa Sina hakika Kama Kodi inakatwa kwenye mishahara yao!
 
Uwezo wa huyu waziri mkuu ni mdogo mno.
Sema kwa vile ni mwana CCM mwenzetu.
 
Waziri Mkuu ameelewa vyema sana,
ufafanuzi mzuri sana.
kazi iendeleeeeeeeeeeee.
 
Kuna mshahara mkubwa unaolipwa hapa bongolala? yaani mil. 2 kwenda mil. 4 ndo PM anasema mshahara mkubwa.......ingekuwa mishahara inayo range mil. 15 hadi mil. 40 kama waliokuwa wanajilipa kule NHC ningemwelewa, siyo hii ya 2-4 mil. Waache kuleta propaganda waweke nyongeza inayoeleweka kama ilivyokuwa kipindi cha kikwete.​
 
Hiyo ndiyo imesababisha inflation,,,,,,,,,,,
Kumridhisha kiumbe anayeitwa binadamu ni ngumu sana.
 
Ngoja nikuulize hivi, increment kwa kiswahili ni nn?
 
Hujui unachozungumza alafu unaongea kwa confidence.
TGS C na D hawajalalamika? Wameongezewa ngapi? Hujui walimu na kada zingine zote ambazo sio science huanza na TGS D
 
Ongezeko la mishahara lazima liendane na hali halisi ya uchumi wa nchi, tusije kuishia kujilipa mishahara huku tukishindwa kutekeleza majukumu mengine ya kimaendeleo.
Inasikitisha sana wengi kuona kama nyongeza ya mishahara ni hisani.Ukiajiri lazima ulipe ujira stahili kwa waajiriwa kulingana na makubaliano.Hivyo Serikali na waajiri wote,ni wajibu wenu kuongeza na kulipa mishahara ya wafanyakazi wenu na muache longo longo.
Hivi hapa Tanzania kima cha chini ni shilingi ngapi,wafanyakazi wa kima cha chini ni wangapi?Tumepigwa tena!
 
Hilo ongezeko ndio ambalo Mh Rais aliwaahidi Wafanyakazi ? Majaliwa tangu aliposema Magufuli ni Mzima na anachapa kazi nani atamuamini tena ?
 
Hao wafanyakazi wamesubiri ongezeko la mishahara tangia alikoshia JK.Wapo waliostaafu kabla ya June 2022 ambao hawakupanda madaraja kwa miaka 7,naye anatakwa kushukuru?Hivi mfanyakazi anaweza kufikia umri wa kustaafu akiwa bado ni wa KCC?
 
Hiyo miaka kadhaa inafidiwaje katika utumishi wa wafanyakazi?Siku hazigandi,kila mfanyakazi anayo tarehe yake ya kustaafu. Hivi PM anapotuambia mawaziri wameongezewa hadi 0.02% anamaana gani?Waziri analipwa Tsh ngapi ili tufanye hesabu?Usikute hiyo 0.02% ni milioni kadhaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…