Waziri Mkuu: Wanaolalama kupata ongezeko la 20,000 ni wale wenye mishahara mikubwa

Waziri Mkuu: Wanaolalama kupata ongezeko la 20,000 ni wale wenye mishahara mikubwa

Mambo yanazidi kuwa "zig zag" kwa hiyo 78% ya watumishi walikuwa wanakula 300000 ( kima cha chini) maana ndo waliopewa 23%
Hapo umeelewa vyema mama anataka kuwainua wenye mishahara midogo na sio wenye mishahara ya mil5
 
Utaratibu wa kuinua watu wanaopata mishahara midogo sio kwa kuwapa nyongeza ya mwaka bali kubadilisha miundo yao ya utumishi. Nyongeza ya mwaka msingi wake ni motisha kwa wafanyakazi wote ili kuwasaidia kukabiliana na hali ya maisha inayobadilika kila wakati.
Hapo umeelewa vyema mama anataka kuwainua wenye mishahara midogo na sio wenye mishahara ya mil5
 
View attachment 2308131
Mhe. Waziri Mkuu amefafanua Vizuri Sana, Dhima ya Mhe Rais Samia Juu ya Sakata la nyongeza ya mshahara.

"78% YA WATUMISHI WAMEPOKEA NYONGEZA YA 23% YA MSHAHARA" Tukiwa bado katika kizungumkuti Juu ya Sakata la hivi karibuni kuhusu nyongeza ya mshahara kwa watumishi wa Umma, leo tarehe 29th mwezi July, Mhe Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania amefafanua wazi juu ya nyongeza hii ya asilimia 23%.

"Asilimia 75 - 78 ya watumishi wote wa Umma ndiyo wanaofaidika na hii asilimia 23 ya nyongeza ya mshahara, hata Mawaziri wetu na wao wanaongezewa asilimia 0.7" - Kassim Majaliwa - Waziri Mkuu

Waziri Mkuu ametoa ufafanuzi mzuri sana kuhusu mambo ya nyongeza ya 23.3% ya mishahara. Kama 78% ya wafanyakazi wote wamepata increment ya 23.3% then huyu anayelalamika ni nani?

"Ukiangalia mshahara kama wa Waziri wamepata 0.7%, sasa nani amepata hiyo ni yule mwenye kipato kikubwa, ujumbe wa msingi ni kwamba asilimia 23 iliyotamkwa haijalipa watu wote,"- Waziri Mkuu

"Hao wanaosema kwamba tumeongeza sh 20 ni wenye mishahara mikubwa, wako kwenye hii asilimia 22, huku ndiyo utawakuta Mawaziri, Makatibu Wakuu, Mameneja, Wakurugenzi na Wakuu wa mikoa ambao kidogo wana mshahara unaotosha,"- Waziri Mkuu

Hakika Mhe Rais Samia Suluhu Hassan ana nia ya dhati, na wafanyakazi wote aliwaambia ataendelea kuboresha maslahi ya watumishi. Hivyo tuendelee kuumunga mkono.
Dah! Aisee
 
Namwamini sana his excellence the prime minister, alichokisema Yuko sahihi, Mimi kwangu nimekuta pesa nzuri tu, lakini pia Mimi nilishajijengea Khali ya kushukuru kwa kila kitu


So pongezi kwa serikali yetu tukufu
 
Sijaskia nchi nyingine ndani ya EAC iliyoongeza mshahara watumishi wake kwa 3% au 5% huku wamenyimwa increment na promotion for 6 years!!
Tunaongozwa na wenye uwezo mdogo sana wa uongozi lkn mkubwa wa maneno.
Ingefaa tungeleta administration ya serikali toka nje huko maana hata kampuni nyingi zinazofanya vizuri administration ni ya wageni!!
Wanasiasa wetu wengi wangazi zajuu wanaakili za kimanara-manara hivi...
 
Isije ikawa wamekwisha malizana na tucta kwa sababu kauli ya mara ya mwisho kutoka serikalini walisema tucta wameenda kujadiliana... Sasa tucta kabla hawajasema tena kitu leo waziri mkuu amezungumza

Baheti ilishapitishwa, hata mkipiga kelele namna gani ni kazi bure! Chapeni kazi!
 
Unaelewa usichoelewa wewe kijanaa, walimu wameongezwa 4% sasa nchi hii walimu wapo kwenyekundi la mishahara mikubwa?? Hawa walimu tunaowaona njaa kali wanauza ubuyu, wanakopa kila mahali na kuishi kwa kupangisha vivyumba viwili!! Use common sense usidanganyike

Mjinga wewe inaonekana hata scale ya midhahara ya walimu huijui kabisa unapopoma tu! Nenda kaangalie TGTS zao halafu linganisha na upupu unaolipwa wewe!
 
Maneno ya Marie Antoinette ktk kasri ya KiFalme nchini Ufaransa yalisababisha ghadhabu kubwa kupanda kwa raia wa Paris na kupelekea mapinduzi ktk miaka ya mwisho ya 1790's

Juzi kule Colombo Sri Lanka wafanyakazi wa sekta ya umma waliambiwa ili kukabiliana na hali ngumu ya kiuchumi na kipato wajiongeze kwa kuanzisha mashamba ili wajikimu, hii baadaye ilipelekea wananchi kuungana na kuiteka Ikulu walioipangisha kwa viongozi waliowachagua hivyo kusababisha viongozi hao kukimbia na kuachia uongozi.


HISTORIA
Paris, France
Marie-Antoinette was King Louis XVI’s wife and the Queen of France during the French Revolution. At some point around 1789, when being told that her starving subjects had no bread, Marie-Antoinette supposedly sniffed, ‘Qu’ils mangent de la brioche’— ‘Let Them Eat Cake’ in French. because brioche is more expensive than bread, the anecdote has been cited as an example of Marie-Antoinette’s obliviousness to ordinary people’s conditions and daily lives in France. With that insensitive remark, the Queen became a hated symbol of the decadent monarchy and fueled the revolution that would cause her to (literally) lose her head in 1793)

https://www.aljazeera.com › news
Crisis-hit Sri Lanka allows gov't workers 4-day week to grow food
Colombo Srilanka
14 Jun 2022 — The nation asks public sector employees to take off on Fridays to grow crops in back yards to avoid a food shortage


Endelea kuota ndoto za alinacha kama hutakuja kukimbia wewe na mke aako na watoto wako!
 
Waziri Mkuu, Kasimu Majaliwa amesema wengi wanaolalamika kupata ongezeko dogo la mishahara ni wale ambao wana mishahara mikubwa. Ametolea mfano wa mawaziri kuwa wako baadhi ambao ongezeko lao ni 0.02%

Amewaomba watumishi kuwaamini viongozi wa vyama vya wafanyakazi. Amesema wengi waliopata ongezeko kubwa ni wale watumishi waliokuwa wanapata mishahara midogo.

Pia amesema wananchi wanapaswa kushukuru kwa ongezeko hilo ambalo miaka kadhaa iliyopita haikuwepo
Rais ndiyo alisema hivyo kweli? Sifa za kijinga
 
Kuna kitu sielewi, hii mishahara ya serikali ndio inayotumika sekta binafsi au? na vipi serikali inapanga mishahara ya sekta binafsi au uhusiano uko vipi kati ya serikali na mishahara ya sekta binafsi

Wewe ukitaka mwenye baa apangiwe mshahara wa wafanyakazi wake na serikali?
 
Mjinga wewe inaonekana hata scale ya midhahara ya walimu huijui kabisa unapopoma tu! Nenda kaangalie TGTS zao halafu linganisha na upupu unaolipwa wewe!
Mpumbafu wewe scale zawalimu nazijua vyema wengi wameangukia nyongeza ya 5% kushuka chini...
Akili kisoda huwezi elewa utabaki kusifu na kuabudu viongozi wako... walimu serikalini wanahali ngumu wanashindwa hata kujinunulia chakula kazini wanaibia chakula cha wanafunzi.
Mtaani wenyemaduka tunawadai mmmno wengi ifikapo kwenye tar. za 17 hivi hadi vibiriti wanakopa
 
Tatizo wameondoa increment...ambayo huwa inabusti sana salio mara dufu ya hilo ongezeko la elfu kumi na mbili..
Mbona hajazungumzia increments ambayo ipo kisheria na wameiondoa?
Kama serikali ambayo ndio mwajiri mkuu nchini inavunja Sheria wazi wazi na hawa waajiri wengine watafanyeje?

Kila kitu ni bajeti, kama bajeti imegota hauwezi kupewa! Swali kuu hapa ni, Je, mnafanya kazi kwa bidii kweli humo maofisini? Au mnadhinda mnachat tu na simu na kuzururazutura mitaani?
 
Kwa majibu kama haya inatosha kusema 2025 wasalimie Ruangwa. Majibu hayana mashiko kabisa na mbaya zaidi Hangaya aliamua kuwapa matarajio makubwa wafanyakazi.
Ni lini na wabunge watalalamika posho ndogo? Ikitokea hii kweli nitaona uzalendo umemkuta mkutwa.

Subirini lile jambo letu bado kidogo, linaenda aste aste!
 
Sawa ni kidogo sana ila naomba tukumbushane
 
Back
Top Bottom