Waziri Mkuu: Watu Bilioni 3.9 Duniani jana walifuatilia Shughuli za Kumuaga Hayati Magufuli

Waziri Mkuu: Watu Bilioni 3.9 Duniani jana walifuatilia Shughuli za Kumuaga Hayati Magufuli

Akiwa anatoa maelezo kabla ya kumkaribisha Rais wa Zanzibar, Waziri Mkuu amesema kwa taarifa walizonazo jana wakati wa shughuli za kumuaga Hayati JPM watu waliofuatilia tukio hilo duniani ni 3.9 bilioni kama siyo 4 bilioni.

Na hivyo amevishushukuru sana vyombo vya habari kwa kurusha matangazo ya moja kwa moja.
Kwa hiyo nusu ya wanadamu walikuwa wanafuatilia mazishi ya Magufuli? Tangu aseme uongo kule Njombe hajaacha ameamua kuwa muongo jumla
 
The number of internet users in the world

There are 4.66 billion internet users in the worldtoday.

The total number of internet users around the world grew by 319 million in the past 12 months – almost 875,000 new users each day.

Kwa data za Waziri Mkuu ina maana ni watu 76 M tu ambao hawakufuatilia
 
Mkuu Tanzania haifahamiki wala haina umaarufu wowote Duniani
Kama hujatoka nje waweza shangaa huko duniani watu wanavyofikiria Africa ni nchi moja, tunaishi msituni, hawawazii kwamba kama hivyo basi huenda hata balozi zao zipo kwenye treehouse, na wanaamini tunafuga simba na tembo kama pets! 😅 😅
Media zao hazionyeshagi bata la Africa, wao kutwa kuonyesha mbuga na magonjwa na vita! Beberu anahakikisha hakuna mtu tokea huko atatamani kuja huku!
Na kwao hawatuonyeshi shida, wazungu maskini, homeless, isolated communities, wezi, addicts..wanatuonyesha raha, maghorofa na viwanda vya teknolojia ya hali ya juu, tutavuka na kuogelea kwenda kusugua vyoo, kufagia barabara, kuzoa taka na kuchambisha vibibi.

Everyday is Saturday................................😎
 
Hapa kuna mawili. Labda anadanganya au haelewi. Yote ni hatari. Kama wamefika 3.9bln basi hili tukio limevunja rekodi ya dunia. Tukio lililoangaliwa zaidi ni Olympics ya uingereza mwaka 2012 kukiwa na watazamaji 3.6bl kwa ujumla.
 
Chochote kitakachotoka kinywani kwa huyu kichukuliwe kama ni uongo.
1616496715861.jpeg

Back
Top Bottom