Ingawa Mwigulu yuko chini ya Rais na hupokea maelekezo kutoka kwake lkn huyu Nchemba anaonekana ni mbinafsi na mwenye Roho mbaya mno. Kwa ujumla, nilimkatia tamaa kiongozi huyu kipindi kile Mh.Lissu apigwe Risasi, jamaa hakushituka wala kujisikia vibaya, kwamba Mbunge wa Mkoa wake, ndugu yake, wauwaji walikuwa wanakusudia kumuua na hivi km waziri mwenye dhamana ya ulinzi alipaswa kuwa na Option 2 ama kudili na tukio lile hadi Wauwaji wapatikane au km angeshindwa, ajiudhuru uwaziri wake km ishala ya kusikitishwa na tukio la Mbunge wenzie tena wa Mkoani kwake kuumizwa vile badala yake, Mwigulu kakomaa na uwaziri huo, yeyote anayetokea kumshauri kujiudhuru, anamdili kisawa sawa (Rejea Abdul Nondo)! Tukija swala hili na utekaji na uuwaji wa wa TZ wenzetu, Mwigulu hawezi kuwa na jibu tofauti zaidi ya hilo jibu jepesi kwa sbb hayo matukio ama anahusika au anajua kilichotendeka na wakina nani walitenda hivyo. Mwigulu hawezi kuwa Rais wa Nchi hii kwani hana ubinadamu Rohoni mwake, lbda apachikwe na chama chake km walivyofanya kwa huyu muasisi wa siasa za kuteka na kuua watu! Ninawakumbusha hii Serikali ya CCM, na huyu mwenyekiti mwao muasisi wa umwagaji damu wa wa TZ wenzetu, Kamwe Damu ya Binadamu haiondoki bure, Damu hii imejiandika kwenye Ardhi ya TZ, ipo siku Mungu atalipa kisasi kwa niaba yao! CCM wanapaswa kujua, siasa za kuteka na kuua watu wanaotofautiana nao mawazo na itikadi za vyama na Dini, zilishapita muda mrefu, mbinu hii ilishapitwa na wakati, itawaghalimu siku moja!
Haiwezekani Nchi iliyokuwa tulivu na ikiwa na amani tele, siku hizi inabaki kuwa ni Nchi ya kuviziana kuuana!! Siasa za kigaidi km za Al-shabab, Al-Quida na Boko haram zimekuwa ni kipao mbele cha CCM na Mwenyekiti wao. Inasikitisha mno!