Waziri Mwigulu: Makato ya Miamala ya Simu tunatunisha mfuko, ni 'Solidarity Fund'

Waziri Mwigulu: Makato ya Miamala ya Simu tunatunisha mfuko, ni 'Solidarity Fund'

Kabisa mzee yani kabisa mwenye njaa ndio anaelewa au aliye nje ya madaraka! Nimeskiliza clip moja ya werema aliekuwa mwanasheria wa serikali! Anadai katiba mpya ni muhimu sababu madaraka ya raisi ni makubwa hatukatai ila mbona hajasema hilo akiwa mwanasheria mkuu wa serikali!
Wengi nima-snitch baada ya mfumo kuwatema Kuna siku hata yule full-tank wa Bunge la saccos ya CCM atakuja kusema katiba mpya ni muhimu Kama anavyo badilika kuhusu bandari ya Bagamoyo
 
Akihojiwa katika kipindi cha 360 cha Clous FM , Waziri wa Fedha na Mipango Mh. Mwigulu Nchemba amesema: "Mtu anayetuma kuanzia 1000-2000 anakatwa shilingi 10. 20,000 mpaka 30,000 anakatwa 960. Milioni 1 mpaka Milioni 3 ni 9000 na Milioni 3 na kuendelea ni 10,000.

Kwa mtu anayetuma 100,000 mpaka 200,000 anakatwa 2500. Kama unaweza kutuma 10,000 kwanini usichangie shughuli za maendeleo?
 
Wengi nima-snitch baada ya mfumo kuwatema Kuna siku hata yule full-tank wa Bunge la saccos ya CCM atakuja kusema katiba mpya ni muhimu Kama anavyo badilika kuhusu bandari ya Bagamoyo
Yani mtu akitolewa kwenye sinia la menu ndio anaona misingi ya katiba imevunjwa ila akiwepo kwenye sinia humwambii kitu! Kuna haja ya kuondosha wanafiki katika system
 
Kabisa mzee yani kabisa mwenye njaa ndio anaelewa au aliye nje ya madaraka! Nimeskiliza clip moja ya werema aliekuwa mwanasheria wa serikali! Anadai katiba mpya ni muhimu sababu madaraka ya raisi ni makubwa hatukatai ila mbona hajasema hilo akiwa mwanasheria mkuu wa serikali!
Mkapa,Membe,jk, Lowasa, sumayi nao wamesema baada ya kutoka madarakani, hata mama akitoka nae ataona umuhimu wake. Ukiwa madarakani huwezi ona.
 
CCM ni balaa tupu,hii mijitu sijui wanaitolea wapi?

Huo ndio ufafanuzi kweli?
Hivi mtu anayepanga kodi yetu waitumieje anaweza kuwa na akili kweli ya kujua 500 ni bajeti nzima ya familia ya mtu kwa siku.Hali mwanae upewa elf 10 ya shule kwa siku.
 
Huku ni mwisho wa kufikiri namna ya kutafuta mapato ya Taifa. Hili moja je matumizi yake je au ndio mnaanza kuficha hesabu na kumwona CAG ni tatizo, huu ni wizi mtupu. Hii kodi inabidi ifutwe na yale matrilioni yaliyopotea yarejeshwe yaje yazibe hilo gap katika mapato. Hata kama alificha nje ya nchi kama Taifa tunaweza kuzirejesha kwa wananchi.
 
Wizara nzima na taasisi zake zinashindwa kuja na vyanzo vingine vya mapato miaka nenda rudi zaidi ya miamala, pombe na mafuta. Hii ni aibu kwa serikali na mfumo mzima wa elimu.
 
Hizo fedha zetu tunaomba zitumike kwa uwazi ... tupewe updates ya kiasi kinachopatikana na kinakwokwenda msije mkatumia kuhongea malaya DODOMA
Ndugu hiyo ya uwazi matumizi sahau, kosa walifanya wabunge wako walipogonga zile meza bungeni wakichekelea na kupitisha kwa 100% bajeti.....muwe wapole tu.
 
Solidarity fund na majizi, wahuni na mafisadi!?
Hizi hela ziende kweli kwenye maendeleo. Naogopa sana zisitumike watu kusafiria kutoka Dar Dodoma na Dodoma Dar, eti wanasafiri kikazi.
Hayo ni matumizi mabaya ya kodi za wananchi. Kama mmeamua kukaa Ddodoma basimiwe hivyo, kupunguza matumizi. Tunahitaji maendeleo. Kodi zetu inapaswa nyingi ziende kwenye maendeleo
 
Mwiguru anapaswa kuja na mpangonwa Serikali wa kupunguza matumizi, Hii Serikali ina matumizi makubwa sana.

Bajeti yenyewe % kubwa ni matumizi ya kawaida,

Huwezi sema nchi ijitegemee wakati kwenye matumizi bado ni ni anasa tupu.

Kwanza Serikali ije na Mpango wa kupunguza matumizi yake ili basi wananchi waonr kwelie Serikali iko Seriouse.
 
Ndugu hiyo ya uwazi matumizi sahau, kosa walifanya wabunge wako walipogonga zile meza bungeni wakichekelea na kupitisha kwa 100% bajeti.....muwe wapole tu.
Unavyosema wabunge wangu una maanisha nini ?mana mimi nilimchagua mmoja nakumbuka.
 
Back
Top Bottom