Waziri Mwigulu: Makato ya Miamala ya Simu tunatunisha mfuko, ni 'Solidarity Fund'

Waziri Mwigulu: Makato ya Miamala ya Simu tunatunisha mfuko, ni 'Solidarity Fund'

Hapa napo katika hii solidarity fund napo cag mwakani apapitie. Halafu wanapoanzisha haya mamvo wanakubaliana na na nani.
 
"Mtu anayetuma 1000 hadi 2000 anakatwa Tsh.10, anayetuma 20,000 hadi 30,000 anakatwa 960, Mil. 1 hadi Mil. 3 ni 9000 na Mil 3 na kuendelea ni 10,000, kwa anaetuma 100,000 hadi 200,000 anakatwa 2500, kama unaweza kutuma 10,000 kwanini usichangie shughuli za maendeleo?”

"Mimi naunga mkono dira ya Rais ya kutaka maji yapatikane kila kijiji, sasa tunafanyaje? tukasema tuchangishane, hivi unaona tunaweza kupoteza maisha ya Mtoto sababu ya maji, kisa unalia unakatwa Tsh.5?, mbona milio ya simu tunaweka na unakatwa Tsh. 100?"———Mwigulu via Clouds360

"Kuna Shule zinakusanya watoto mpaka 1500 au 1000 na Shule haina maji wanaambiwa waende Shule na kidumu cha maji, sasa tunafanyaje ili maji yapatikane? ndio maana kuna uwepo wa kukatwa Tsh. tano kila unapotuma hela kwa ajili ya huu mfuko wa mshikamano"———Mwigulu via Clouds360

"Watu wanalalamika kuhusu hela za miamala, hii ni solidarity fund, tuna mambo ambayo tunakubaliana hayapaswi kuendelea mfano ubovu wa Barabara vijijini, kama Taifa tuongeze Tsh.100 katika mafuta ili kila fedha itakayoongezeka iende kuleta maendeleo"——Mwigulu Nchemba via Clouds360

"Kwenye chungu, ni lazima bajeti, fedha zitatoka wapi ni lazima tutoe kodi, mwaka huu tumeleta kodi ya miamala, ni vizuri sana mjue hili la kwenye miamala sio tu kodi, hili tunatunisha mfuko, ni solidarity fund, huu ni mfuko wa mshikamano wa Watanzania"

"Akaunti zilifungwa kipindi kile kwasababu ya masuala ya kikodi na Wafanyabiashara wanarudishiwa fedha zao kwasababu akaunti imelipa kodi au hesabu zake zilipigwa vibaya kwahiyo kuna fedha ambayo haikuwa kodi inarudishwa"

"Kenya, Uganda, Malawi, Rwanda, Msumbiji mafuta yako bei juu kuliko sisi, ulishaona hizo Nchi waje kununua mafuta Tanzania?, nitoe rai Watanzania wawe Wazalendo kwasababu kwenye Nchi zote zinazotuzunguka Tanzania ndio Nchi inayouza mafuta bei ya chini"
Ndiyo tumefika hapa kama Taifa.

R.I.P JPM.
 
Serikali ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan imedhamiria kuendelea kuiunganisha nchi kwa kutengeneza miundombinu mipya ya barabara katika maeneo yasiyofikika ambayo kwa asilimia kubwa yapo vijijini.

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba amesema ili kuhakikisha kwamba lengo la Mhe. Rais la kuinua uchumi linafanikwa kama alivyoahidi ameanza kwa kutengeneza miundombinu ya barabara za Vijijini kupitia ongezeko la Shilingi 100 kitakachopatikana kwenye mafuta ambapo Serikali itakusanya zaidi ya Shilingi Bilioni 322.

Waziri Nchemba amesema barabara za Vijijini zikishakamilika itapunguza vifo vya Mama Wajawazito ambao kwenye maeneo mengi wanajifungulia njiani sababu ya barabara hazipitiki, lakini pia itasaidia maeneo yasiyokua na maendeleo kupata maendeleo kwa kasi.

Hakika Mama hakukosea aliposema nia yake ni kuisimamisha nchi kiuchumi, na kazi hiyo anaifanya kwa kasi kubwa sana, muhimu Watanzania tuendelee kumuombea na kulipa kodi kihalali.
 
Serikali ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan imedhamiria kuendelea kuiunganisha nchi kwa kutengeneza miundombinu mipya ya barabara katika maeneo yasiyofikika ambayo kwa asilimia kubwa yapo vijijini...
Mie kinachonishosha ni kuona nguvu za kulazimisha viongozi wavae barakoa wakati kwa miaka 2 walikuwa hawavai pamoja na uwepo wa covid -19.

Wenye akili tushajua miezi mitatu tu baada ya kifo cha JPM tunasarandia pesa za wahisani.INAUMA SANA. Yaani na matakwimu ya wagonjwa yanatangazwa hadharani na mwisho watu wanachelewesha mitungi ili ionekane wagonjwa ni wengi na mitungi imeisha.INAUMA SANA.

INAUMA SANA hizo barabara za vijijini ni kwa kiwango cha changarawe yaani sio lami tena.lakini ndio mawazo yaliopo!!!
 
KAMA NI KWELI KUNA NIA NJEMA YA KUONGEZA MAPATO:
1.Serikali punguzeni kodi ya kuagiza gari ili wengi waagize na mtapata kodi zaidi wengi wakinunua mafuta.

2.Mnataka mpate mapato zaidi kwenye pombe na vileo, Serikali mruhusu baa ziendele kutoa huduma hadi saa 8 usiku badala ya saa 6 usiku, na mwananchi anaruhusiwa kunywa pombe muda wowote ili mradi havunji sheria.

3.Zipo mbinu nyingi za kupata mapato bila kutumia nguvu,bila mwananchi kulalamika.

4.Ukisikia wananchi wanalalamika mjue mmetumia nguvu au mazoea bila ubunifu katika kutekeleza majukumu yenu!!!
 
Anaongelea sh 100 kana kwamba hiyo ndio Kodi pekee kwenye mafuta! Anajisahaulisha msururu wa karibia Kodi 20 kwenye mafuta hayohayo!.Apuuzwe
Hakukuwa na haja ya kuongeza hata 50 kwenye mafuta..ongezeko lolote kwenye mafuta linasababusha ongezeko la bei kwenye kila bidhaa
 
KAMA NI KWELI KUNA NIA NJEMA YA KUONGEZA MAPATO:
1.Serikali punguzeni kodi ya kuagiza gari ili wengi waagize na mtapata kodi zaidi wengi wakinunua mafuta...
I hope mama anapita huku ayaone haya mawazo mbadala nje ya mawazo ya wasaidizi wake
 
Mie kinachonishosha ni kuona nguvu za kulazimisha viongozi wavae barakoa wakati kwa miaka 2 walikuwa hawavai pamoja na uwepo wa covid -19.
Wenye akili tushajua miezi mitatu tu baada ya kifo cha JPM tunasarandia pesa za wahisani.INAUMA SANA..
Barabara zenyewe zitazojengwa nafikiri nyingi ni za changarawe sasa hapo kwa sie wenye kidogo, ndo zenye upigaji kweli....maana ni kumwaga vifusi tu na kusambaza.

Mvua ikinyesha kesho/kesho kutwa ikapitiwa maji na (ukizingatia kutokana na ujenzi wenyewe wa contractors wetu wengi tuliozoea ambao mara nyingi unakuwa na viwango vya chini) ,inakuwa back to square one' na barabara kuhitaji kujengwa upya tena within short period of time... na matokeo yake yaani tija inakuwa ni zero.

Hivyo mie naona itakuwa ni aina ya ufujaji mwingine wa pesa tu,na labda ningependekeza basi angalau zingekuwa barabara zile za' aina ya 'bitumen single surface dressings' ili kupata kidogo 'Value for money' kwenye miundombinu hiyo ,especially kwa nchi kama zetu maskini, ambazo hatuna ukwasi endelevu wa pesa.

Kazi iendelee.
 
Tumemuelewa vizuri Waziri wa Fedha kwa Ufafanuzi alio ufanya juu ya ulipaji wa kodi hizo na madhumuni ya kodi. Shime Watanzania wenzangu tuijenge nchi yetu, tusikubali kudanganywa na watu ambao sio wazalendo.
 
Mimi sina shida na kodi ya mafuta ambapo hadi sasa miradi imetuzidia yaani,safi Sana.

Kwenye maendeleo watu wanapayuka ila kuchangiana kadi za sherehe za kijinga hawaulizagi ,kulewa hawaulizi na kuhonga hutowasikia wakisema ni costful.

So long as hiyo mia haiathiri chochote Mwigulu pigilia msumali japo mm sijaridhishwa na formula mliyotumia kugawanya hizo pesa maana maeneo ya Miji mumeyabana huku Vijijini kwa kweli mumewapa mgao wa kutosha sio chini ya Bil.1
 
Serikali ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan imedhamiria kuendelea kuiunganisha nchi kwa kutengeneza miundombinu mipya ya barabara katika maeneo yasiyofikika ambayo kwa asilimia kubwa yapo vijijini...
Aelezee pia litakavyo ongeza mfumuko wa bei
 
Tatizo hizo pesa zinakuja kupigwa na wachache, alafu inaishia kuunda tume za uchunguzi na hizo tume zinapiga tena pesa hizo hizo...
 
safi sana Dr. Mwigulu kwa ufafanuzi safi na sahihi.
wazalendo wote wa kitanzania wamekuelewa sasa tuko tayari kuchangia maendeleo yetu sisi wenyewe.
Mjenga nchi ni mwananchi mwenyewe.....Kamwe tusiibomoe nchi yetu kwa kudanganyana, tuchangie maendeleo yetu.
kila siku tunachangia harusi,eee off, kicheni pati, na takataka nyingine kibao! leo hii tushindwe kuchangia sh 100? 1000? 10? 500? jamani tuone aibu, tuwe wazalendo.

Safari hii hakuna atakaye chezea pesa ya walipa kodi wazalendo, ole wake atakaye dokoa, ole wake atakaye chelewesha maendeleo ya wananchi wazalendo.
 
Hapo kwenye kusema nchi za wenzetu mafuta yako juu sidhani kama yuko sahihi. La pili kwani lazima kufanya kwa kujilinganisha na hao aliowataja? Kama wakija kununua kwetu sisi tutakuwa tunapata hasara gani? Juzi niliona kule mbeya watu wanaamka saa tisa kwenda kupanga foleni kununua mafuta zambia ambako yanauzwa 1700 je waziri analifahamu hilo?
 
safi sana Dr. Mwigulu kwa ufafanuzi safi na sahihi.
wazalendo wote wa kitanzania wamekuelewa sasa tuko tayari kuchangia maendeleo yetu sisi wenyewe.
Mjenga nchi ni mwananchi mwenyewe.....Kamwe tusiibomoe nchi yetu kwa kudanganyana, tuchangie maendeleo yetu.
kila siku tunachangia harusi,eee off, kicheni pati, na takataka nyingine kibao! leo hii tushindwe kuchangia sh 100? 1000? 10? 500? jamani tuone aibu, tuwe wazalendo.

Safari hii hakuna atakaye chezea pesa ya walipa kodi wazalendo, ole wake atakaye dokoa, ole wake atakaye chelewesha maendeleo ya wananchi wazalendo.
 
Hali ya kiuchumi ikoje kwa upande wako toka ujio wa mgeni wetu mpya solidarity Tax?
Mnatumia mbinu gani kuweza kukabiliana na haya majanga ya kutuma hela wenzangu! Hebu tupeane mawazo maana spana zimezidi!

Wale wenye michuma hasa V6 mnaona mnaweza kuendelea kutumia vyombo vyenu kwa muda gani toka sasa!
 
eti kodi ya mshikamano 🤣 🤣 🤣

yani taifa linashikamana vipi kwa kuongezewa kodi na linashikamana na nani?

CCM na Mwigulu wameshaona kuwa wananchi wote ni makondoo.
 
Back
Top Bottom