Waziri Mwigulu: Makato ya Miamala ya Simu tunatunisha mfuko, ni 'Solidarity Fund'

Waziri Mwigulu: Makato ya Miamala ya Simu tunatunisha mfuko, ni 'Solidarity Fund'

Kuna siku nilisikia huyu mama anasema alisoma uchumi, mpaka unashangaa pamoja na taaluma yake hiyo ameshindwa kutambua kuwa kuongeza kodi ya dhuruma kwenye miamala ya simu ni kuuwa uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Serikali na wachumi uchwara wanakaa wanaweka jumla yakodi tatu kwenye muamala mmoja wa simu hizi si dharau za waziwazi nakutuona mazuzu ,wanapandisha kwa makusudi bei ya mafuta kitu ambacho ni kichocheo namba moja cha ushughuli za kiuchumi nchini.

Jambo la kuchekesha zaidi nikaona hapa hakuna kiongozi nikupunguza kodi kwenye vitu ambavyo havina tija kwenye uchumi wa nchii, yaani mtu anapunguza kodi kwenye betting/gambling ,pombe halafu anapandisha tozo kwenye gharama ya mafuta.

Yaani mama katika vipaumbele vyako vyote kwenye shughuli za kiuchumi nikuchochea kamali na unywaji pombe, vingine vyoote umepiga chini. Watu wanasema mwigulu anakufanyia hujuma sio kweli vitu vidogo kama hivyo havihitaji mpaka usome macro economics yaani umepwaya kweli kweli.

Oky kodi mmeshaanza kuchukua jee zitasaidia vipi wananchii kama sio kuibia masikini, Mama ebu rejea bajeti ya ofisi ya waziri mkuu ya mwaka 21/22 asilimia 80 ya bajeti yote ni matumizi binafsi asilima 20 ndio inapelekwa kwenye shughuli za maendelea.
Matumizi binafsi wanalipana posho mara mbili mbili, vikao visivyo na tija, wanakula bata huku wakiaacha raia kwenye janga la umasikini.

Uongozi mbovu,, muundo wa serikali mbovu, bunge bovu, katiba mbovu

Sent using Jamii Forums mobile app
View attachment 1855593
Kama golini yupo mwana wa kalidayo unategemea nini,kikubwa hapo maombi tu.
 
Kama nchi tulipita kipindi kigumu sana. Biashara zilifungwa, watu walifilisiwa, kodi nyingi za haramu zilibambikwa kwa wafanyabiashara. Aliyejaribu kufungua mdomo wake kulalamikia hayo labda asijulikane. Vinginevyo angetekwa kisha ama akapotea kabisa au akabambikiwa kesi itakayomuweka mahabusu muda mrefu au angehujumiwa kwa namna yoyote

Inashangaza kuona Wabongo ni wasahaulifu kiasi hiki. Angalau sasa kuna japo kauhuru ka kulalamikia hayo hadharani na usiwe na hofu ya kupotezwa. Au labda wanaotoa maneno makli dhidi ya awamu ya sita ni wale wachache sanasana waliokua wafaidika wa utawala ule!

Kodi hizi za miamala ni mbaya lakini haiondoi ukweli kwamba awamu iliyopita ilikua ya kidhalimu sana. Lakini kutamani eti ile hali ya mambo ya awamu ya tano irudie tena kwa Watanzania ni roho mbaya na utovu wa shukrani kwa Mungu wetu. Angalau Mama na serikali yake hamkamati mtu kwa kupinga sheria mbaya.

Mimi naamini ni suala la muda tu kodi kandamizi zitafutwa kutokanana na usikivu wa awamu ya sita. Lakini kutamani kurudi tulipotoka HAPANA

kipindi cha makufuli kilikuwa kizuri sana tutamkumbuka
 
Kwa jinsi nilivyokuwa namkubali huyu Sina la kusema naona aibu,shikamooni wote tuliowaita Sukuma gang
Katangaza Corona sasa hivi watalii wote wamesitsha kuja Zanzibar wafanyakaz wa hotel wanaenda kupoteza Ajira, hotel zitafungwa, uchumi unaenda kusimama Zanzibar.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na Bado[emoji23][emoji23] yetu macho na masikio[emoji124][emoji125][emoji125]
Utasikia mama kaupiga mwingi 😂
IMG-20210716-WA0023.jpg
 
AAache kuongeza kodi ila afwatilie zile pesa walozopiga watu
JPM alikuwa anafanya hivi alionekana MKUDA ila alijua walioiba lazima zirudi sio kuwakaba watu wa hali ya chini hata mlo wao SHIDA.
 
Kuna siku nilisikia huyu mama anasema alisoma uchumi, mpaka unashangaa pamoja na taaluma yake hiyo ameshindwa kutambua kuwa kuongeza kodi ya dhuruma kwenye miamala ya simu ni kuuwa uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Serikali na wachumi uchwara wanakaa wanaweka jumla yakodi tatu kwenye muamala mmoja wa simu hizi si dharau za waziwazi nakutuona mazuzu ,wanapandisha kwa makusudi bei ya mafuta kitu ambacho ni kichocheo namba moja cha ushughuli za kiuchumi nchini.

Jambo la kuchekesha zaidi nikaona hapa hakuna kiongozi nikupunguza kodi kwenye vitu ambavyo havina tija kwenye uchumi wa nchii, yaani mtu anapunguza kodi kwenye betting/gambling ,pombe halafu anapandisha tozo kwenye gharama ya mafuta.

Yaani mama katika vipaumbele vyako vyote kwenye shughuli za kiuchumi nikuchochea kamali na unywaji pombe, vingine vyoote umepiga chini. Watu wanasema mwigulu anakufanyia hujuma sio kweli vitu vidogo kama hivyo havihitaji mpaka usome macro economics yaani umepwaya kweli kweli.

Oky kodi mmeshaanza kuchukua jee zitasaidia vipi wananchii kama sio kuibia masikini, Mama ebu rejea bajeti ya ofisi ya waziri mkuu ya mwaka 21/22 asilimia 80 ya bajeti yote ni matumizi binafsi asilima 20 ndio inapelekwa kwenye shughuli za maendelea.
Matumizi binafsi wanalipana posho mara mbili mbili, vikao visivyo na tija, wanakula bata huku wakiaacha raia kwenye janga la umasikini.

Uongozi mbovu,, muundo wa serikali mbovu, bunge bovu, katiba mbovu

Sent using Jamii Forums mobile app
View attachment 1855593
We taga unasumbuliwa chuki binafsi tu!

Huna hoja yoyote ya maana. Bajeti hii,ilikuwa imeandakiwa na mwendazake. Je kama mwendazake angekuwepo ungeporomosha hayo matusi yako?

Kila mtanzania lazima alipe kodi ili kugharimia miradi ya maendeleo. Hakuna njia ya mkato.
 
yupo bize nje huko, ukiona unashauriwa na watu wa pwani ujue unaingizwa chaka situka...hatariii
 
Kama nchi tulipita kipindi kigumu sana. Biashara zilifungwa, watu walifilisiwa, kodi nyingi za haramu zilibambikwa kwa wafanyabiashara. Aliyejaribu kufungua mdomo wake kulalamikia hayo labda asijulikane. Vinginevyo angetekwa kisha ama akapotea kabisa au akabambikiwa kesi itakayomuweka mahabusu muda mrefu au angehujumiwa kwa namna yoyote

Inashangaza kuona Wabongo ni wasahaulifu kiasi hiki. Angalau sasa kuna japo kauhuru ka kulalamikia hayo hadharani na usiwe na hofu ya kupotezwa. Au labda wanaotoa maneno makli dhidi ya awamu ya sita ni wale wachache sanasana waliokua wafaidika wa utawala ule!

Kodi hizi za miamala ni mbaya lakini haiondoi ukweli kwamba awamu iliyopita ilikua ya kidhalimu sana. Lakini kutamani eti ile hali ya mambo ya awamu ya tano irudie tena kwa Watanzania ni roho mbaya na utovu wa shukrani kwa Mungu wetu. Angalau Mama na serikali yake hamkamati mtu kwa kupinga sheria mbaya.

Mimi naamini ni suala la muda tu kodi kandamizi zitafutwa kutokanana na usikivu wa awamu ya sita. Lakini kutamani kurudi tulipotoka HAPANA
[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji106][emoji106][emoji106]
 
Kila mwaka huwa wanapandisha kodi kwenye bidhaa zile zile zenye umuhimu kwa wananchi, halafu wanajisifu kwa ubunifu wao.

Mwigulu anataka kusema amekosa kabisa chanzo kingine cha mapato zaidi ya kumnyonya mwananchi wa kawaida kwenye bidhaa adimu wanayoitumia kila siku?

Kule kwenye machimbo ya madini mliyowapa wazungu kwa kuchukua 10% pangefaa zaidi kuwaongezea kodi wale wafanyabiashara kutokana na faida wanayopata, kuliko kuyafanya mafuta yaonekane anasa.

Kwa hali hii mnaondoa vipi umasikini kwa mwananchi wa kawaida hasa kule vijijini kama bado mnamuongezea mzigo matumizi kwenye mahitaji yake muhimu? hata tukiwatumia pesa za matumizi kwa njia ya simu nako mmepandisha kodi!.
tozo ya shilingi mia kwa kila lita ya mafuta haina athari yeyote kiuhalisia kaka.

kule kwny migodi ya madini msijisahaulishe,
mlisema serikali imekurupuka na kwamba itashitakiwa, kipindi kile serikali ilipokaa mezani na wawekezaji
 
Wamesahau
 
"Mtu anayetuma 1000 hadi 2000 anakatwa Tsh.10, anayetuma 20,000 hadi 30,000 anakatwa 960, Mil. 1 hadi Mil. 3 ni 9000 na Mil 3 na kuendelea ni 10,000, kwa anaetuma 100,000 hadi 200,000 anakatwa 2500, kama unaweza kutuma 10,000 kwanini usichangie shughuli za maendeleo?”

"Mimi naunga mkono dira ya Rais ya kutaka maji yapatikane kila kijiji, sasa tunafanyaje? tukasema tuchangishane, hivi unaona tunaweza kupoteza maisha ya Mtoto sababu ya maji, kisa unalia unakatwa Tsh.5?, mbona milio ya simu tunaweka na unakatwa Tsh. 100?"

"Kuna Shule zinakusanya watoto mpaka 1500 au 1000 na Shule haina maji wanaambiwa waende Shule na kidumu cha maji, sasa tunafanyaje ili maji yapatikane? ndio maana kuna uwepo wa kukatwa Tsh. tano kila unapotuma hela kwa ajili ya huu mfuko wa mshikamano"

"Watu wanalalamika kuhusu hela za miamala, hii ni solidarity fund, tuna mambo ambayo tunakubaliana hayapaswi kuendelea mfano ubovu wa Barabara vijijini, kama Taifa tuongeze Tsh.100 katika mafuta ili kila fedha itakayoongezeka iende kuleta maendeleo"

"Kwenye chungu, ni lazima bajeti, fedha zitatoka wapi ni lazima tutoe kodi, mwaka huu tumeleta kodi ya miamala, ni vizuri sana mjue hili la kwenye miamala sio tu kodi, hili tunatunisha mfuko, ni solidarity fund, huu ni mfuko wa mshikamano wa Watanzania"

"Akaunti zilifungwa kipindi kile kwasababu ya masuala ya kikodi na Wafanyabiashara wanarudishiwa fedha zao kwasababu akaunti imelipa kodi au hesabu zake zilipigwa vibaya kwahiyo kuna fedha ambayo haikuwa kodi inarudishwa"

"Kenya, Uganda, Malawi, Rwanda, Msumbiji mafuta yako bei juu kuliko sisi, ulishaona hizo Nchi waje kununua mafuta Tanzania?, nitoe rai Watanzania wawe Wazalendo kwasababu kwenye Nchi zote zinazotuzunguka Tanzania ndio Nchi inayouza mafuta bei ya chini"

Chanzo: CLOUDS 360
Ya kulipa deni la ipitieli itatoka humu humu au yenyewe itakuwa na solidaliti nyingine.
Na ya ma BX yale ma baiskeli makubwa solidaliti yake nayo humo humo au nayo ina kodi yake
 
Back
Top Bottom