Waziri Mwigulu Nchemba: Deni la Taifa lafikia Tsh Trilion 69.44

Waziri Mwigulu Nchemba: Deni la Taifa lafikia Tsh Trilion 69.44

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba amesema hadi kufikia Aprili 2022, deni la Serikali lilikuwa Sh69.44 trilioni ikilinganishwa na Sh60.72 trilioni kwa kipindi kama hicho mwaka 2021, sawa na ongezeko la asilimia 14.4.

Kati ya kiasi hicho, deni la nje lilikuwa Sh47.07 trilioni na deni la ndani lilikuwa Sh22.37 trilioni

Dk Nchemba amesema hayo leo Jumanne Juni 14, 2022 wakati akiwasilisha hali ya uchumi wa Taifa na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka wa fedha 2022/23.

Amesema ongezeko la deni la Serikali lilitokana na kupokelewa kwa mikopo mipya kutoka vyanzo vyenye masharti nafuu na ya kibiashara kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo.

Aidha, ongezeko la deni lilitokana na kutolewa kwa hatifungani maalumu yenye thamani ya Sh2.18 trilioni kwa ajili ya deni la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) lililotokana na michango ya watumishi wa kabla ya mwaka 1999.

Amesema taarifa ya tathmini ya uhimilivu wa deni iliyofanyika Novemba 2021 inaonesha kuwa deni la Serikali bado ni himilivu katika kipindi cha muda mfupi, wa kati na mrefu kwa kuzingatia ukomo wa viashiria vyote vinavyokubalika kimataifa.

Hii speed ya kukopa ni disaster kwa nchi. Juzi tena wamekopa TZS 2.4 trillion kutoka World Bank.

Sijui hili deni litakuwa limefikia wapi by the time huyu ombaomba anamaliza hii term. Ipo siku, when it’s too late, Watanzania watajuta kuipotezea ile warning ya Ndugai!
 
Acha porojo wewe.

Hizo hesabu za Trillion 1.8 uliona wapi?

Nadi ya Mwaka Mkopo Trillion 9... Mara sita ni Trillion 54. Tuaisoma namba wote..huku wachache wakilamba asali.
Samia sio wa level za wachunga Ng'ombe ni corporate leader 👇
 
Attachments

  • Screenshot_20220406-164902.png
    Screenshot_20220406-164902.png
    90.3 KB · Views: 7
  • Screenshot_20220406-163449.png
    Screenshot_20220406-163449.png
    53.8 KB · Views: 6
Hii speed ya kukopa ni disaster kwa nchi. Juzi tena wamekopa TZS 2.4 trillion kutoka World Bank.

Sijui hili deni litakuwa limefikia wapi by the time huyu ombaomba anamaliza hii term. Ipo siku, when it’s too late, Watanzania watajuta kuipotezea ile warning ya Ndugai!
Inauma sana
 
Turuhusu kilimo cha bhangi, mirungi, Coke na opium, Serikali ikope ianzishe na kuboresha mashamba, ndani ya mwaka tu Tanzania itakuwa ni nchi ambayo haina deni kabisa..
 
Turuhusu kilimo cha bhangi, mirungi, Coke na opium, Serikali ikope ianzishe na kuboresha mashamba, ndani ya mwaka tu Tanzania itakuwa ni nchi ambayo haina deni kabisa..
Hizo ndumu mtakuwa mnawauzia nchi gani?
 
Unaleta vipeperushi na akili yako inaishia hapo?

Hakikisha kwanza kama kichwa hakijatobolewa.. usije kuta umemwaga ubongo.

Hadi 2025 - Tuaandika TANZANIA SOLD.
Kaandike kwenye sebule yako mke wako na watoto watakuwa wanasoma kila siku itawasaidia kupata pesa
 
Back
Top Bottom