Waziri Mwigulu Nchemba: Deni la Taifa lafikia Tsh Trilion 69.44

Jiwe hahusiki na uchafu huu..Hizo ni hera za deni la serikali ililloacha kuchangia pspss miaka ya nyuma..Soma uelee
Jiwe hahusiki na nini? Jiwe alifilisi mifuko ya jamii akachukua pesa akapeleka kwenye sgr na ndege na Bwawa..

Ili kuiokoa na kufilisika akaiunganisha..Baba yangu alikaa miaka 3 baada ya kustaafu ndio kapewa mafao napo walimpunja tukafuatilia zaidi ya miaka 2 ndio alikuwa kulipwa..

Ishu kubwa ilikuwa ni pesa hakuna.Kws hiyo Ili kuiokoa ndio maana Serikali imeamua itoe hizo bonds Ili wapate pesa wazilipe kwenye mifuko ..

On top of that miradi mingi ya mifuko kama majengo ya biashara,mall nk yalikosa wapangaji baada ya Jiwe kuvuruga Uchumi..

Naandika jambo ambalo Nina ufahamu nalo.
 
Kama maendeleo ni kuzunguka sana nje ya nchi, hiyo nchi ya Oman kiongozi wao mkuu huwa anafanya ziara wapi?
 
Vyambo vipya vya TOZO na Kodi kila koda.

Kwenye LUKU kodi, Kwenye Miamara Kodi.. n.k..
 
Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Mwigulu Nchemba leo Bungeni Dodoma amesema hadi April 2022 deni la Taifa lilikua ni Trilioni 69.44 ikilinganishwa na trilioni 60.72 kipindi kama hicho mwaka 2021 ambayo ni sawa na ongezeko la 14.4%". Source:MillardAyoUPDATE


Je tunaendelea kufurahia uwazi?
 
Tutakubali tu hatimaye!!
 
Nape, Mbowe, Lissu ,Zito, Lema wako bize kulamba asali hawatahoji chochote.

Siku moja mtamkumbuka Ndugai

Duh! Sijui CHADEMA ilikukosea Nini?. Chadema mliwanyima kura 2020 mkaichagua CCM , leo mnaanza kumlaumu Mbowe na Leama wakati bungeni mmejaza wabunge wa CCM wenye uwezo wa kuhoji serikali.

Punguza roho mbaya na uangalie reality.
 
Himilivu maana yake dhamana iliyopo nchini bado ni kubwa kuliko hilo deni, hivyo wanaweza kuendelea kukopa labda hadi trillion 300 hivi
 
Tanzania's national debt grows by TZS 8.72 TRILLION in one year

In April 2021, debt was TZS 60.72 trillion compared to TZS 69.44 trillon in April 2022, Finance and Planning Minister Mwigulu Nchemba told Parliament state of economy speech

👉This is a 14.4% increase in one year
 
Pongezi kwa Dr. Mwigulu kwa kuwasilisha Bajeti ya kimkakati na yenye malengo ya kuchochea maendeleo ya nchi na wananchi.

Pongezi kwa Serikali ya awamu ya 6 , kwa umakini na weledi wa viwango vya juuu.

wananchi wanaona jinsi akili inavyo tumika zaidi kuliko nguvu.


kazi iendeleeeee hadi 2030
 

External Debt in the United States increased to 23,370,708 USD Million​

Ukilinganisha na Tanzania ni sawa na Punje ya sisimizi kwa DEni la Marekani.
Mfanya biashara aliye serious huwa haogopi kukpppa.
Taifa lenye mipango thabiti ya Kiuchumi huwa haliogopi kuanzisha mirai mikubwa na haliogopi kuingia ubia na kukopa .
Kitu muhimu ni Uongozi makini naUsimamizi mzuri wa Deni la taifa na ukusanyaji wa kodi uliomzuri.
Nadhani Inafaa Serikali ikope mpaka kufikia Trilion 100 ili watanzania wapate viwanda, uzalishaji mzuri wa chakula,miundombinu iliyoboreshwa,na kukuza kiwango cha elimu na Ajira kwa watanzania.
 
On April 28, 2022, the Congressional Budget Office released a report which stated that in order to stabilize the $30 trillion in national debt
 
Umeongea kitu cha mingi sana mkuu, "ustawi wa maisha". Utaogopaje madeni, mapesa yako huko duniani ni ya kuchukua tu. Kesho itajisumbukia yenyewe.


Yesu ni Bwana

Ukopaji unaokwenda sanjari na leakage isiyo kifani hauna tija. Ni mzigo tu kwa wananchi wa kawaida wa kizazi cha sasa na vivazi vijavyo! Huwezi kujaza maji kwenye tenga la kubebea nyanya!
 
Ukopaji unaokwenda sanjari na leakage isiyo kifani hauna tija. Ni mzigo tu kwa wananchi wa kawaida wa kizazi cha sasa na vivazi vijavyo! Huwezi kujaza maji kwenye tenga la kubebea nyanya!
Kweli kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…