Waziri Mwigulu Nchemba, nani kakutuma umchonganishe Rais na wananchi wake? Hautafanikiwa...

Waziri wa fedha ndo mshauri mkuu wa Raisi kuhusu masuala ya uchumi hasa kwenye kodi mpya na madhara yake Mwigulu is resiposible 100% kwahili
 
Waziri wa fedha ndo mshauri mkuu wa Raisi kuhusu masuala ya uchumi hasa kwenye kodi mpya na madhara yake Mwigulu is resiposible 100% kwahili
Kwa hiyo Rais naye akapokea ushauri wa kijinga kama huu na kuukubali? Hivi wewe ukishauriwa swala la kipumbavu na ukakubali kulitekeleza unataka lawama tuzipeleke kwa mshauri wako!?
 
Mmekua wajinga kupititliza mwigulu hawezi kuamua lolote, ukiona jambo limepita ni kwamba raisi karidhia. mbona mengi tu kayakataa iweje hili alikubali?
Kama mwigulu ameweza kumzidi ujanja kwenye Jambo kubwa Kama hili basi huyu mama HAFAI KUWA RAISI
 
Msimsingizie Mwigulu! Jambo kama la kodi mpaka linaletwa bungeni kwenye vikao vya baraza la mawaziri lishapitishwa!

Huyo Rais alimteua mshauri wake wa masuala ya kiuchumi anafanya kazi gani? Au anakula mshahara wa bure?
Mpaka jambo kubwa kama hili linapita jua lina baraka za rais.
 
nahisi mama hakupata muda wa kuipitia kwa kina rasimu ya bajeti kabla ya kupelekwa bungeni!
Nasikitika kwamba ni bajeti iliyojaa tozo ndio wabunge wa CCM walikuwa wakiishangilia muda wote leo wananchi wanalia machozi!
Mara leo mafuta bei juu, kesho tozo bei juu, kesho kutwa kitafuata kingine!
 
Huu siyo uandishi wako. Upo chini ya kiwango!!

Imetekwa?
 
Nimeandika uzi Kuhusu hili. Wale wa kupigania Legacy ya Shujaa na (au) waliojipanga Urais 2025 ndio masterminds wa hii issue. Lengo ni Mama aonekane hafai na achukiwe na Wananchi ili iwe ngumu kwake na 2025.

Inatakiwa ionekane hakutokua na Rais bora kuliko Shujaa, so yoyote anaeonekana kufanya vizuri lazima aharibiwe ili Shujaa abaki kama Shujaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…