Waziri Mwigulu Nchemba, nani kakutuma umchonganishe Rais na wananchi wake? Hautafanikiwa...

Kwamba unataka kusema Mwigulu anataka kumchafua Rais. Kwamba Rais naye alisaini muswada wa sheria ya fedha ya mwaka 2021 blindly bila kujua maudhui ya muswada husika!? If that is the case basi huyu Rais ni tatizo zaidi kuliko hata huyo Waziri wake. Kwa lugha nyingine hata yeye hafai vile vile kama ambavyo Ndugai alikuwa anauliza sheria mbaya inapitaje bungeni wakati yeye ndiye Spika.
NB: nilikuwa naamini wewe una akili kipindi kile cha utawala wa JPM, lakini naona dalili zote za akili za Cyprian Musiba zikiwa kwako pia
Waziri wa fedha ndo mshauri mkuu wa Raisi kuhusu masuala ya uchumi hasa kwenye kodi mpya na madhara yake Mwigulu is resiposible 100% kwahili
 
Kwa hiyo Rais naye akapokea ushauri wa kijinga kama huu na kuukubali? Hivi wewe ukishauriwa swala la kipumbavu na ukakubali kulitekeleza unataka lawama tuzipeleke kwa mshauri wako!?
 
Mmekua wajinga kupititliza mwigulu hawezi kuamua lolote, ukiona jambo limepita ni kwamba raisi karidhia. mbona mengi tu kayakataa iweje hili alikubali?
Kama mwigulu ameweza kumzidi ujanja kwenye Jambo kubwa Kama hili basi huyu mama HAFAI KUWA RAISI
 
Msimsingizie Mwigulu! Jambo kama la kodi mpaka linaletwa bungeni kwenye vikao vya baraza la mawaziri lishapitishwa!

Huyo Rais alimteua mshauri wake wa masuala ya kiuchumi anafanya kazi gani? Au anakula mshahara wa bure?
Mpaka jambo kubwa kama hili linapita jua lina baraka za rais.
 
nahisi mama hakupata muda wa kuipitia kwa kina rasimu ya bajeti kabla ya kupelekwa bungeni!
Nasikitika kwamba ni bajeti iliyojaa tozo ndio wabunge wa CCM walikuwa wakiishangilia muda wote leo wananchi wanalia machozi!
Mara leo mafuta bei juu, kesho tozo bei juu, kesho kutwa kitafuata kingine!
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na mambo mengine, ni mkuu wa nchi na mkuu wa Serikali. Kuongoza nchi na Serikali ni kuongoza watanzania wote: furaha na karaha zao huelekezwa kwa Rais. Mazuri yao na mabaya kwao wananchi husemwa kuwa yametokana na uongozi wa Rais aliye madarakani. Kwasasa, Rais wetu mpendwa ni Mama Samia Suluhu Hassan. Yeye ndiye dira yetu, nguzo yetu, tegemeo letu na nembo yetu.

Katika kutekeleza majukumu yake, Rais huwa na wasaidizi wake. Wapo wanaochaguliwa; wanaoteuliwa na hata anaowakuta anapoingia madarakani. Mawaziri ni kati ya wasaidizi wa Rais. Wao hubeba na kuzitekeleza ajenda/sera za Rais katika Wizara zao na kuzisimamia. Mawaziri ni mikono ya Rais. Mikono hiyo inapofurahisha, wananchi humfurahia Rais. Inapoumiza, wananchi humlalamikia na 'kumchukia' Rais.

Waziri wa Fedha, Daktari wa Falsafa Mwigulu Nchemba amekuwa gumzo lenye mzozo na kodi zake za miamala ya fedha kimtandao na hata kupanda kwa tozo kwenye mafuta na bidhaa nyinginezo. Amekosolewa na anaendelea kukosolewa kwa sauti kuu ya wananchi pamoja na kuziita kodi hizo kuwa ni kodi za kizalendo. Ajue kuwa uzalendo huwa haulazimishwi. Uzalendo ni uhiyari na utayari. Kulazimisha kodi si kulazimisha uzalendo. Ni kuubomoa.

Waziri Nchemba ameteleza. Amekosea pakubwa kwenye kodi husika. Amekaribisha madhara makubwa ikiwemo kupanda kwa gharama za maisha na hasara yenye hasira kwa wahusika wa huduma za kifedha. Wananchi wanaweza kuwa na 'mgomo' kwenye matumizi ya huduma hizo. Huduma zitaathirika na hata kufa. Uwekezaji utaathirika. Hasira na chuki kwa Rais. Uchonganishi. Bidhaa na huduma zitapanda bei. Maisha yatakuwa magumu. Hasira kwa Rais. Uchonganishi.

Nani hasa amekutuma huku akihema Waziri Nchemba umchonganishe Rais na wananchi wake? Kwa lengo lipi? Kwa faida ya nani? Ili iweje? Waziri Nchemba, amini nakwambia, hautafanikiwa. Rais Samia hatakubali kuchonganishwa na wananchi wake kupitia kodi na tozo. Atachukua hatua. Atajilinda. Atajitetea. Ataibuka mshindi. Lengo lako limeshajianika, halitafanikiwa.

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Arusha)
Huu siyo uandishi wako. Upo chini ya kiwango!!

Imetekwa?
 
Nimeandika uzi Kuhusu hili. Wale wa kupigania Legacy ya Shujaa na (au) waliojipanga Urais 2025 ndio masterminds wa hii issue. Lengo ni Mama aonekane hafai na achukiwe na Wananchi ili iwe ngumu kwake na 2025.

Inatakiwa ionekane hakutokua na Rais bora kuliko Shujaa, so yoyote anaeonekana kufanya vizuri lazima aharibiwe ili Shujaa abaki kama Shujaa.
 
Back
Top Bottom