Mapema leo nimefanya mazungumzo kwa njia ya mtandao na Dkt. Sidi Ould Tah, Mkurugenzi Mkuu wa @badeabank kujadili namna ya kuharakisha upatikanaji wa fedha za mkopo nafuu na msaada Dola Bilioni 3 sawa na takriban Shilingi Trilioni 7.
Benki ya BADEA iliahidi kuipatia Tanzania mkopo huu wa masharti nafuu (soft loan) katika kipindi cha miaka mitano ijayo, zitakazotumika kwenye miradi ya maendeleo sambamba na kuiwezesha sekta binafsi.
Hakuna mkopo mzuri kwa serikali wa miaka 5!!!. Ni ngumu kupata mikopo ya bank mizuri kwa nchi. Nchi zinatakiwa kuuza Government bonds au kukopa kwa bank maalumu za kukopa nchi na mikopo ni ya miaka 15-25 sio miaka 5!. Hii ndiyo sababu makusanyo mengi yanaenda kulipa madeni. Lakini hujaleta detail za mkopo wenyewe hapa