BabuKijiko
Member
- May 3, 2024
- 24
- 38
"Moja ya hoja iliyokuwa inatolewa ni kushushwa kwa VAT kutoka 18% kwenda 12%, na mimi ningetamani iwe hata 10% lakini hatujaacha tu kuishusha sababu ya kiburi cha Wizara au Serikali tu imekataa, hatujashusha kwasababu kuna nambo mengi ya msingi tunatekeleza."
"Ukishusha 2% ya VAT unapoteza bilioni 600 kwa pamoja. Ukishusha hivyo na tuna miradi mikubwa tunatekeleza inaathiri bajeti. Ukishusha kwa kiasi hicho unakuwa na 10%, bajeti ya Serikali itaathirika. Tumesema twende nayo hatua kwa hatua"
Waziri Mwigulu amezungumza haya leo, Juni 26, 2024 Bungeni wakati akijibu hoja za Wabunge na kinachoendelea nchini kwa sasa ikiwahusu wafanyabiashara kuendeleza mgomo wakidai kuchoshwa na vitendo wanavyofanyiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Hadi sasa mikioa ya Iringa, Dar es salaam, Mwanza, Mbeya na Mtwara. Mgomo wa Wafanyabiashara kutokufungua maduka nchini ulianza Juni 24, 2024 jijini Dar es Salaam.