Waziri Mwigulu: Tukishusha 2% ya VAT tutapoteza Bilioni 600, Bajeti ya Serikali itaathirika

Ukishusha, watu wengi zaidi watalipa. Tena wangeishusha zaidi ili wapate zaidi.

Amandla...
 
Kama hali ngumu Serikali ibane matumizi sioni haja ya kununua magari ya kifahari V8(mkurugenzi, mkuu wa Wilaya, DAS, mkuu wa mkoa, RAS, waziri, N/w, Makatibu n.k) vipuli, service na mafuta ni gharama kubwa, harafu tunalundikiwa kodi. Nashauri vikao vya bunge vipunguzwe kuokoa mabillion.
 
Pumbavu punguza matumizi ya serikali kufidia hilo pengo
 
Kwa kiwango cha madini kilichopo na yanayochimbwa nchini yangetosha zaidi ya kutosha.
Waambie kudi watazipata kwenye ufisadi wanaofanya
 
Kitakacho athirika ni mifuko yao mafisadi ambao hua wanatajwa na Cag kukwapua mabilioni kila mwaka, kama wangedhibiti matundu ya upigaji ambayo waliyatoboa wenyewe alafu wakayaziba kwa mkate kupunguza utitiri wa Kodi inawezekana kabisa na hakuna ambae angewaza kukwepa kodi
 
WAKATI MWINGINE SEREKALI NI LAZIMA IFANYE BIASHARA KATIKA KUZIBA BAADHI YA MAPENGO, MFANO, IAGIZE YENYEWE SUKARI KUPITIA JESHI ILI KUZIBA BAADHI YA MAPENGO!, AIDHA BIDHAA FULANI ADIMU!, SEREKALI NYINGI TU HUFANYA HILI, KATIKA KU RESCUE HALI FULANI, IACHANE NA KUTUMIA WAFANYABIASHARA MAANA HUMO NDIMO WIZI HUFANYIKA.
 
Kwanini hagusii suala la wao kupunguza matumizi waanze kupanda SGR Dar Dodoma hakuna mashangingi tena wapande economy class sio kuendelea kuoandisha kodi ambazo wao binafsi hazilipi kwakua wanahudumiwa bure kwanini wao wakandamize tu wananchi halafu baadae lawama wanawapa TRA
 
Ukishusha, watu wengi zaidi watalipa. Tena wangeishusha zaidi ili wapate zaidi.

Amandla...
Kitu watu hawajui ni hakuna mfanyabiashara anatakiwa kulipa Kodi ya ongezeko la thamani ,anayelipa ni mlaji(final consumer)ni ajabu badala kupambana service levy ifutwe wanahangaika Kodi isiyowahusu,wafanya biashara ni mawakala wa kukusanya Kodi hiyo na ndio maana vat wanayolipa wanaponunua bidhaa za kuuza wanarudishiwa na zile walizokusanya toka kwa waliowauzia bidhaa wanatakiwa kuwasilisha kwa Mamlaka za serikali,vat iwe 20%au 18%au12%si yao.wao wapambane na withholding tax,service levy,income tax na nyingine kama tozo tozo,business licence,billboard fee na ongeza...,.
 
Mwigulu anachofikiri ni Kuongeza Kodi tu na si kushusha hiyo 18% na ile 25% sijui waliitoa wapi aisee...Nchi nyingi ni 14% na 15% VAT..
 
Nakubaliana na hatua za kubana matumizi, wabunge waslishwe upepo na waziri Mwiguru. kukusanya bila austerity measures za matumizi ni kazi bure. Pia wawe wabunifu fedha nyingi iko informal sector wanaiachia kisiasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…