Waziri Nape jiuzulu haraka, unatishia amani ya taifa letu

ngara23

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2019
Posts
9,091
Reaction score
21,087
Nashangaa inakuwaje Nape kwanini yupo ofsini hadi Leo.
Yaani ametoa kauli chafu na kuharibu amani yetu Bado anaona utani?
Utani Gani au uhuni amekuwa akirudia hii kauli.

Me ni mwana CCM ili siwezi kufurahishwa na ushindi wa wizi na kunajisi democracy. Tushindane Kwa sera na vyama vingine atakaeshinda ndo huyo

Hivi waziri tunaekuheshimu kujisifu ati ni mtaalamu wa kuiba kura na kunajisi democracy unasema ni utani

Nape amejivunjia heshima au anataka tuandamane kama Kenya?
Ametuona Watanganyika wapumbavu.

Rais Samia mtoe huyu jamaa ofsini haraka, ili tukuamini tuone kweli hii kauli ya mtendaji wako ilikuchukiza.
Kwani yeye ndo alizaliwa kuwa waziri.

Moderators msifute huu Uzi.
Maana naona nyuzi za kumhusu Nape mnafuta
 

Nape ni kiazi mbatata kichwani
 
NAPE, MAKAMBA & MWIGULU Hawana sifa wala Haiba ya kuwa hata KATIBU TARAFA. Ifike pahala tuchukue hatua, ndio maana Bwana yule aliwamwaga mapema sana maana aliwabaini kwamba Vichwani ni weupeee kama chaki. Kwahiyo tuache kuwalaumu, hapo ndipo uwezo wao unakomea.
 
Watakwambia wakati mzee Moses Nnauye,na wazee wenzake wanakijenga chama mzee wako alikuwa kizura mimba akilima mihogo
Ccm ina wenyewe
KUWA mpole
Wana CCM tuko sawa.
Wasijipe ubora kuliko wenzao.
Nape hana sifa ya kuwa kiongozi.
Ona anajisifu utalaam wa kuiba kura badala ajisifu kuleta maendeleo
 
Huu uzi ukidumu ni bahati mana kuna sehemu Nape ni boss wa Melo
Kwaiyo siku hizi ukimgusa tu Nape uzi unafutwa.
 
Rais hawezi kumtoa Nape maana huo ndio msimamo wa Rais na ccm yake. Rais ni lazima aaogope kumuwajibisha Nape maana atakuwa amemuonea kwa yeye kusema ukweli.
 
Rais hawezi kumtoa Nape maana huo ndio msimamo wa Rais na ccm yake. Rais ni lazima aaogope kumuwajibisha Nape maana atakuwa amemuonea kwa yeye kusema ukweli.
Hapa ndo tutajua rangi halisi ya Rais wetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…