Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi amesema kuwa Serikali imezitaka mamlaka za TPDC, PBPA na EWURA kuhakikisha kuwa punguzo la bei ya mafuta katika soko la dunia linaanza kuonekana kwa wananchi nchini kuanzia mwezi ujao.
Agizo hili linakuja kufuatia kuanza kushuka kwa bei ya mafuta ghafi duniani hadi kufikia dola 70 kwa pipa, baada ya kupatikana kwa makubaliano ya kusitisha mapigano ya siku 60 (ceasefire) katika mgogoro wa Mashariki ya Kati ulihusisha nchi za Iran, Israel na Marekani.