TANZIA Waziri Salome Mbatia afariki dunia, maswali yaibuka!

TANZIA Waziri Salome Mbatia afariki dunia, maswali yaibuka!

Mungu awalaze pema marehemu na awape nguvu majeruhi wapate kupona haraka
 
Mungu amlaze mahala pema peponi!.. duh, bongo jamani haya magari makubwa ya mkaa na magogo yatatumaliza. nadhani swala hapa sio kutazama tena magari ila barabara zetu hasa huko bara.
Sielewi kilisibu hasa, lakini nadiriki kusema hizi ndio gharama kubwa za kutojali ujenzi wa barabara bora!

Mkandara,

Mimi nimepita hiyo barabara mara nyingi. Tatizo sio barabara bali uendeshaji mbovu.

Kwa mwendo uliopangwa ile barabara inatosha kabisa. Tatizo madereva wengi hawataki kujali speed iliyowekwa na matokeo yake wote tunalia.
 
Poleni wafiwa na Mungu awape amani yake katika wakati huu mgumu
 
suala la kuangalia picha za maiti si geni kwa Watanzania na si la ajabu. Mfano mzuri ni wa ajali ya Mv. Bukoba, zile picha zilikuwa zinauzwa kama Njugu.. why? I have no idea. Tumekuwa tukiangalia picha za marehemu wakati wote. Sijui jinsi ya kutuma kupitia PM ningewatumia anayetaka kuona.. ila kama bado kuna watu hawajaziona naweza kuiweka tena hapa..
 
Mwenyezi Mungu amlaze marehemu mahali pema peponi~AMIN, na pia awape faraja familia yake, ndugu, jamaa na marafiki katika kipindi hiki kigumu kwao.
 
Seems she was still alive when this picture was taken. Had there been ra rapid response; who knows she could still be alive.

Mungu awarehemu wote waliopoteza maisha katika ajali hii.
 
Waziri Salome Mbatia afariki dunia

*Gari lake lagongana uso kwa uso na lori Fusso
*Waokoaji walazimika kukata mabati kuwatoa


NAIBU Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Bibi Salome Mbatia, amefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea jana saa 10: 45 eneo la Kibena Factory wilayani Njombe mkoani Iringa.

Akithibitisha kutokea kifo hicho kwa njia ya simu kutoka eneo la tukio, Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Dkt. David Mathayo, alisema marehemu Mbatia alikumbwa na mkasa huo akiwa safarini kutoka Dar es Salaam kuelekea Njombe, akiwa katika gari lake binafsi, Nissan Patrol namba T 724 AGZ.

"Tupo hapa tunajaribu kukata bati tuwatoe, ni kweli wamekufa alikuwa kwenye gari lake binafsi, Nissan Patrol yeye na dereva wake, "alisema Dkt. Mathayo.

Alieleza kuwa ajali hiyo ilitokea baada ya lori aina ya Mitsubishi Fusso lenye namba T 299 AFJ lililokuwa likitoka Njombe kwenda Makambako kuhama njia yakena kugongana uso kwa uso na gari la waziri huyo.

"Nimepata taarifa kuna watu walikuwa wanamsubiri (Naibu Waziri) huko Njombe, naamini alikuwa safarini kwenda huko lakini sielewi ilikuwa safari ya kikazi au binafsi," alisema Dkt. Mathayo.

Dkt. Mathayo alikumbana na tukio hilo wakati akiwa safarini kutoka Dar es Salaam kwenda Tunduma kikazi kufuatilia manunuzi ya korosho. Alisema mtu mmoja ambaye hakutambulika mara moja aliyekuwa kwenye lori hilo, naye alikufa papo hapo.

Francis Godwin kutoka Iringa anaripoti kuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Bw. Advocate Nyombi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo nakueleza nakuwataja waliofariki kuwa ni watu watatu, akiwemo Waziri Mbatia.

Alisema polisi mkoani hapa wanaendelea na uchunguzi ajali hiyo, watatoa taarifa kamili baada ya kukamilika uchunguzi.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Njombe, Dkt. John Luanda alithibitisha kupokea majeruhi wa ajali hiyo na kwamba baadhi ya madaktari walikwenda eneo la tukio kusaidia kutoa miili iliyong'ang'ania kwenye mabaki ya magari hayo.

Habari zaidi kutoka eneo la tukio, zilisema mbali ya Dkt. Mathayo, watu wengine walikuwa kwenye eneo la tukio na kutoa msaada mkubwa ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Bw. Zitto Kabwe ambaye alikuwa safarini kwenda mkoani Ruvuma.

Bw. Kabwe alimweleza mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu kuwa alishuhudia magari hayo yakigonganga uso kwa uso na kulazimika kukatiza safari yake kusadia kuwahisha majeruhi hospitali.

Moja ya matukio ya kukumbukwa kwa naibu waziri huyo ni kwamba Machi 8 mwaka huu wakati wa kilele cha Siku ya Wanawake Duniani, alitembelea chumba cha habari cha gazeti la Majira kama mgeni rasmi na kujionea jinsi waandishi na wafanyakazi wanawake, walivyokuwa wakiandaa gazeti siku hiyo.

Akiwa kwenye chumba hicho cha habari, marehemu Mbatia aliwaasa wanawake wa Kampuni ya Business Times inayomiliki magazeti ya Business Times , Majira, Dar Leo, Spoti Starehe na Maisha kuwa wachapakazi na kueleza jinsi alivyofurahishwa kuona jitihada zao.

Kwa mujibu wa tovuti ya Bunge, marehemu Mbatia, alizaliwa Juni 17, 1952 na kupata elimu yake ya msingi katika shule za St. Ann (1959-1962), St. Theresa (1963-1964) na Shule ya Msingi Msimbazi (1965-1966).

Aliendelea na elimu ya sekondari kwenye shule ya St. Joseph (1967-1970) na kuhitimu elimu ya juu ya sekondari kwenye Shule ya Wasichana ya Korogwe mwaka 1972.

Marehemu pia alikuwa mmoja wa wanawake wasomi kwa kupata elimu ya juu katika vyuo mbalimbali ndani na nje ya nchi akiwa mtaalamu aliyebobea katika masuala ya utawala na uchumi.

Wasifu wake unaonesha kuwa alipata shahada ya kwanza ya sanaa [BA (Hons)] kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1976 kabla ya mwaka 1982 kujiunga na Chuo cha ADL nchini Marekani ambako alipata shahada ya uzamili katika utawala (MSc. Management).

Pia alikwenda nchini Uholanzi mwaka 1987 ambako alipata Diploma ya Uzamivu katika Utawala (Post-Graduate Diploma in Administration & Management) kutoka chuo cha RVB Delft.

Kabla ya kuingia katika siasa, marehemu alifanya kazi mbalimbali za fani alizosomea ambapo mwaka 1977 aliajiriwa na Bodi ya Biashara ya Nje akiwa mfanyakazi-mwanafunzi kabla ya kupanda vyeo hadi kuwa Meneja Masoko na kisha Meneja wa Mauzo wa Kanda.

Mwaka 1979 alijiunga na kampuni ya Biashara Consumer Services Co. Ltd ambako alipanda vyeo hadi kufikia wadhifa wa Meneja Mkuu mwaka 1990.

Mwaka 1998 alikuwa Katibu Mkuu wa Taifa wa Jumuiya ya Wanawake ya CCM (UWT) wadhifa alioutumikia hadi mwaka 2005.

Aliingia kwenye siasa mwaka 2000 ambapo amekuwa Mbunge wa Viti Maalum (CCM) kutoka mkoa wa Kilimanjaro na kuwa pia mjumbe wa Mkutano Mkuu. Amekuwa pia kwa miaka kadhaa sasa mjumbe wa Bodi ya Shirika la Uwekezaji la Taifa (NICO).

Kati ya mwaka 2002 na 2005 alikuwa Mweka Hazina wa chama hicho na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na kuonesha umahiri katika siasa hasa wakati wa kampeni ambapo alikuwa mmoja wa makada waliokuwa wakiaminika sana katika kuipigia kampeni CCM hasa kwenye majimbo yaliyokuwa yakionekana kuwa na upinzani mkali.

Januari mosi mwaka jana, aliteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa Naibu Waziri wa Uchumi, Mipango na Uwezeshaji kabla ya Oktoba 17 mwaka huo huo kuhamishiwa kuwa Naibu Waziri Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, nafasi aliyokuwa nayo hadi mauti yalipomfika jana.

Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi!

Source: Majira
 
Pole wafiwa wote na Mungu !RIP, Deputy Minister ,MBATIA (Mrs)!
Kuhusu Picha Hapa ni Sehemu ya kupashana Habari, sasa wale mnaosema picha ziondolewe mkiondoa hapa na huko sehemu nyingine za media mtaziondoa?Mimi naona mziwache na zitaendelea kuwa sehemu ya historia na kumbukumbu kwani pamoja na ubinadaamu wake alikuwa ni Public Figure.Cha msingi aliyeileta hapa amejaribu kuhifadhi vitu vingi ambavyo labda vingeonyeshwa isingekuwa vizuri!
 
Namwomba Mwenyezi Mungu Azilaze Pahala Pema Peponi Roho za Marehemu. Nawaombea na Kuwaunga Mkono Katika Majonzi Wanafamilia na Marafiki Wote, Pia Nawaombea Ahueni na Usalama Majeruhi Wote. Amina.


SteveD
 
mungu awalaze marehemu wote peponi. amin
picha ziondolewe zile zenye kuonyesha miili ya marehemu, ila zibakishwe zenywe kuonyesha over view ya ajali yenyewe.
 
yeah, mkjj nnategemea umetimiza wajibu wako, sasa tunaomba uweke zile picha ambazo zinaonyesha tukio lenyewe kwa ujumla pasipo kuonesha wahanga.

nnazani kuna moja nimeiona hiyo gari kwa mbele ilivyoumia. sio mbaya ukatuletea za hiyo lori na views mbali mbali bila ya kuathiri hisia za wengine.

haya nimaoni yangu safi kwako mkuu, una hiyari juu ya kuyaweka kapuni au kuyafanyia kazi
 
Wajamani,

Mie nimeshtushwa sana na vifo hivi kama ninavyoshtuka nikisikia ajali yoyote ile.

I dont see the difference, waliokufa wote ni wa Tanzania na ni binadamu. Tofauti ni kuwa mmoja wao alikuwa na uwezo wa kusaidia ajali kama hizo zipungue lakini hakufanya hivyo au alifanya akashindwa.

Mungu azilaze roho za marehemu wote mahala pema peponi AAAmen!
 
she was....
Mungu amempenda zaidi..poleni familia ya mama Mbatia

Why pole kwa familia ya Waziri tu jamani. Tupende kujali watanzania wote! waliokufa umeambiwa ni wanne.

Hii ndio hulka na tabia ya watanzania, ndio maana hata mkingia madarakani mnajijali nyinyi tu. Ni kitu tulichonacho lakini huwezi kujijua unajikuta tu ni mbinafsi. Thread hii imewaonyesha wengi wenu. Including Mwanakijiji!
 
jamboonormal_pichayaajali.jpg
Mzee Mwanakijiji mbona umetoa Picha ya ajali,naomba unitumie katika PM yangu
 
Mungu warehemu wote waliopoteza maisha na wajalie faraja ndugu,jamaa na rafiki zao. Habari nyingine zinaeleza kuwa waziri wake bi Sofia Simba naye alikuwa mgonjwa na alilazwa huko south africa.
 
Back
Top Bottom