Waziri Sangu: Mtu anaajiriwa leo anataka kuwa milionea, anaanza kuwaona wengine sio wajanja

Waziri Sangu: Mtu anaajiriwa leo anataka kuwa milionea, anaanza kuwaona wengine sio wajanja

Bawabu wa pili

Senior Member
Joined
Nov 14, 2025
Posts
147
Reaction score
433
Serikali imesema itachukua hatua stahiki za kuwawajibisha Watumishi wa umma wanaokiuka maadili ya utumishi na kushindwa kusimamia miradi ya maendeleo ipasavyo pamoja na viongozi wanaodhalilisha Watumishi wa Umma hasa kwenye ziara za ukaguzi wa miradi ya maendeleo

Hayo yamesemwa jana Januari 15, 2025, Jijini Dodoma wakati Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu, akifungua kikao cha 31 cha Baraza Kuu la Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU).

Soma pia: Naibu Waziri Sangu, kielelezo Cha ma CCM na Dola, katika Utawala wa Sheria, alipaswa kua tayari Kaondoshwa kwenye Uwaziri



Kauli hiyo inakuja kufuatia kuibuka kwa matukio ambapo baadhi ya viongozi walionekana hadharani wakizungumza kwa lugha kali dhidi ya Watumishi wa Umma

Awali katika risala yake, Kaimu Katibu Mkuu wa TALGWU, Wandiba Kongoro, aliweka bayana jinsi ambavyo kumekuwa na wimbi la Viongozi wa Kisiasa kuwadhalilisha Watumishi wa umma, jambo linalochochea changamoto katika utendaji wa kazi na usimamizi wa miradi ya maendeleo.
 
Mtu anakuwa Rais wa mchongo, ndani ya muda mfupi anajaza ndugu na watoto kwenye teuzi. Anawaona Marais waliotangulia kama hawakuwa na watoto.
 
Back
Top Bottom