Waziri Selemani Jafo amsema Mkurugenzi wa SCOL Building Contractors Limited hadi akaanguka na kuzimia

Waziri Selemani Jafo amsema Mkurugenzi wa SCOL Building Contractors Limited hadi akaanguka na kuzimia

Mkuu huyo mtu ndio mmiliki wa skol sidhani km unaweza kumdharau hivyo. Always anavaa hivyo au ovaroli usimchukulie poa. Ana mashine za construction kibao halafu unaongelea buku 5.
Huyo mwenzetu atakuwa hamjui huyo mmiliki wa hiyo kampuni ya SKOL. Miaka nenda rudi amekuwa akijenga barabara nyingi tu nchini hususani jijini Dsm. Nakumbuka miaka michache nyuma hata Makonda alishampiga marufuku ya kufanya kazi mkoani Dsm. Yawezekana awamu zilizopita alizoea kunywa mvinyo na wenye maamuzi ya kutoa kandarasi na awamu hii ameshindwa kusoma alama za nyakati.
 



Mkurugenzi wa kampuni ya SCOL Building Contractors Limited ameanguka na kuzirai mbele ya Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo baada ya kubanwa kuhusu ucheleweshaji wa ujenzi wa barabara ya Martin Luther hadi Swaswa mjini Dodoma.

Tukio hilo limetokea jana Jumatano Desemba 4, 2019 baada ya Jafo kutembelea ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilomita nane iliyotakiwa kukamilika Agosti lakini ukaongezwa muda hadi Oktoba, 2019. Alizirai baada ya kuelezwa na Jafo kuwa kusuasua kwake kutasababisha asipewe kazi nyingine za ujenzi wa barabara
 
Hivi unapata wapi ujasiri wa kuzimia mbele ya waziri??
Je ukiwa mbele ya Rais si utakufa kabisa
Na ukisimama mbele za Mungu na huna Kristo ndani yako, si utatupiwa kwenye Jehanami ya moto kabisa
Acheni hizo bhana za kuzimia zimia
 



Mkurugenzi wa kampuni ya SCOL Building Contractors Limited ameanguka na kuzirai mbele ya TAMISEMI, Selemani Jafo baada ya kubanwa kuhusu ucheleweshaji wa ujenzi wa barabara ya Martin Luther hadi Swaswa mjini Dodoma.

Tukio hilo limetokea jana Jumatano Desemba 4, 2019 baada ya Jafo kutembelea ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilomita nane iliyotakiwa kukamilika Agosti lakini ukaongezwa muda hadi Oktoba, 2019. Alizirai baada ya kuelezwa na Jafo kuwa kusuasua kwake kutasababisha asipewe kazi nyingine za ujenzi wa barabara


Lazima utaanguka tu kwa Yale waliyoyasema:
1. Huku unadaiwa TRA hela unayolipwa inakatwa deni na Tra juu kwa. Juu
2. Huku kazi iko mbioni kunyang'anywa muda uliopewa hautoshi kumaliza
3. Wafanyakazi wanahitaji mishahara yao kama kawaida mambo ya madeni ya kampeni hayawahusu..
UTAZIMIA TU..
 
Duh...!, nimeona kweli jamaa kazirai!, ila tuelezane ukweli, jamaa alikuwa na matatizo mengine ya kiafya, hivyo kauli ya Jafo ikawa ni kama tuu kumsukuma mlevi, kinachomwangusha mlevi akisukumwa ni kilevi na sio kusukumwa, tena hapo Joffo anaongea kistaarabu sana, angekuwa ni yule anayefanya bullying?, jamaa si ingekuwa hapo hapo!.

Ila pia kiukweli Waziri Jafo na viongozi wote waliokuwepo hapo, wamekosa utu, ubinaadamu, mtu ameanguka ameziarai, that was emergence, ilibidi kila kitu kisimame, mgonjwa apatiwe huduma ya kwanza, lakini waziri aliendelea tuu, na DC wa Dodoma naye akafuatia as if nothing happened!. Tuchape kazi, yes, lakini pia tuwe na utu!, kunapotokea emergency kama ile, no one knows tatizo ni nini, kama ni pressure, asipopata msaada wa haraka in split of seconds, anything can happen!, utu kwanza, kazi baadae!.

P
 
Back
Top Bottom