Waziri Selemani Jafo amsema Mkurugenzi wa SCOL Building Contractors Limited hadi akaanguka na kuzimia

Waziri Selemani Jafo amsema Mkurugenzi wa SCOL Building Contractors Limited hadi akaanguka na kuzimia

Hiki ni kitu kipya kwa Wabongo walizoea mdebwedo, kupelekeshwa kwa kasi, kitu ambacho cha kawaida Kenya, yaani jamaa anahojiwa na waziri hadi akazimia. Ndugu zetu, hiyo ndio hali yenyewe, mkitaka kutukaribia kiuchumi lazima mkubali kwenda kwa kasi, na mtazimia sana kabla kuja kuzoea.

Ukiwa meneja kwa Wabongo yaani utatamani kulia, full vijisababu na utepetevu wa kufa mtu.

Hivi hakuna taratibu za watumishi kujitetea kabla ya kuadhibiwa? Au ndo nyakati za ukweli na uwazi....jitetee hadharani.
 
Mkurugenzi wa kampuni ya SCOL Building Contractors Limited ameanguka na kuzirai mbele ya Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo baada ya kubanwa kuhusu ucheleweshaji wa ujenzi wa barabara ya Martin Luther hadi Swaswa mjini Dodoma.

Tukio hilo limetokea jana Jumatano Desemba 4, 2019 baada ya Jafo kutembelea ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilomita nane iliyotakiwa kukamilika Agosti lakini ukaongezwa muda hadi Oktoba, 2019. Alizirai baada ya kuelezwa na Jafo kuwa kusuasua kwake kutasababisha asipewe kazi nyingine za ujenzi wa barabara

Ni udhalilishaji wa makandarasi wazalendo unaofanywa na awamu hii.
Kandarasi kuwa na matatizo hilo jambo la kawaida.
Ukichunguza nyuma ya pazia kuna uchleweshaji mkubwa wa malipo.

Makandarasi wengi tu wa kichina wanapendelewa, wengi tunajua hilo.

Tazama na sikiliza vizuri maneno ya Mh Jafo, zaidi ya PUNITIVE ACTION he doesnt offer any solution.
Ndio aina ya viongozi tulionao Tanzania.

Itakuwa Jafo amefurahi sana kumzima pumzi mkandarasi, na alifurahi kuwa anakatwa pesa kufikia 82milion kwa kuchelewesha kazi.
Lakini ukweli kama alivyoainisha msimamizi, kukatwa fedha kunampunguzia mkandarasi uwezo wa kumalizia mradi.

USHAURI KWA MKANDARASI
Bwaga manyanga, watakuua na kufurahia hilo wanasiasa wa awamu ya tano.
 
Je kama haya yanatokea, ni nini viongozi wetu wakuu wenye mamlaka wanapaswa wajifunze wanapotoa tamko/adhabu kama kutumbua au kumemea kiongozi aliye chini yake?

Mfano
1: Mwanri alimzimisha afisa Elimu baada ya kumtumbua

Majibu ya Mwanri baada ya mtu kuzimia - Kuzimia, yawezekana mtu amelala chini – is not an issue.

2: Jafo amzimisha mkurugezi baada ya kumpa muda mfupi ili kukamilisha mradi

Majibu ya Jafo - Eee bwana wee simama wewe.

Je ni wangapi walio pata shida walipo tumbuliwa na mkuu wanchi?

Je ni nini kifanyike ili kupunguza makali ya maneno kuepusha madhara zaidi?
Ile ishu za MAKONDER...
 
Hehehe hii ibaki huku huku Wakenya tuijadili maana ni sababu kuu ya kwanini tunaongoza kuchumi, yani Kenya huwa full mzukaaaaa!!! Labda tukija kuajiriwa Bongo ndio kidgo huwa tunapumzika na kuhisi ni kama tuko likizo vile.....hehehe
Kiko wapi 😂😂😂
Nenda ujadili uchumi wenu na upunguze kuwashwa washwa
 
Je kama haya yanatokea, ni nini viongozi wetu wakuu wenye mamlaka wanapaswa wajifunze wanapotoa tamko/adhabu kama kutumbua au kumemea kiongozi aliye chini yake?

Mfano
1: Mwanri alimzimisha afisa Elimu baada ya kumtumbua

Majibu ya Mwanri baada ya mtu kuzimia - Kuzimia, yawezekana mtu amelala chini – is not an issue.

2: Jafo amzimisha mkurugezi baada ya kumpa muda mfupi ili kukamilisha mradi

Majibu ya Jafo - Eee bwana wee simama wewe.

Je ni wangapi walio pata shida walipo tumbuliwa na mkuu wanchi?

Je ni nini kifanyike ili kupunguza makali ya maneno kuepusha madhara zaidi?
Awamu hii !!
mmmmh......
 
1575527953576.jpeg

Maendeleo hayana chama
 
Back
Top Bottom