Waziri Selemani Jafo amsema Mkurugenzi wa SCOL Building Contractors Limited hadi akaanguka na kuzimia

Hiki ni kitu kipya kwa Wabongo walizoea mdebwedo, kupelekeshwa kwa kasi, kitu ambacho cha kawaida Kenya, yaani jamaa anahojiwa na waziri hadi akazimia. Ndugu zetu, hiyo ndio hali yenyewe, mkitaka kutukaribia kiuchumi lazima mkubali kwenda kwa kasi, na mtazimia sana kabla kuja kuzoea.

Ukiwa meneja kwa Wabongo yaani utatamani kulia, full vijisababu na utepetevu wa kufa mtu.

 
Hivi hakuna taratibu za watumishi kujitetea kabla ya kuadhibiwa? Au ndo nyakati za ukweli na uwazi....jitetee hadharani.
 
Ni udhalilishaji wa makandarasi wazalendo unaofanywa na awamu hii.
Kandarasi kuwa na matatizo hilo jambo la kawaida.
Ukichunguza nyuma ya pazia kuna uchleweshaji mkubwa wa malipo.

Makandarasi wengi tu wa kichina wanapendelewa, wengi tunajua hilo.

Tazama na sikiliza vizuri maneno ya Mh Jafo, zaidi ya PUNITIVE ACTION he doesnt offer any solution.
Ndio aina ya viongozi tulionao Tanzania.

Itakuwa Jafo amefurahi sana kumzima pumzi mkandarasi, na alifurahi kuwa anakatwa pesa kufikia 82milion kwa kuchelewesha kazi.
Lakini ukweli kama alivyoainisha msimamizi, kukatwa fedha kunampunguzia mkandarasi uwezo wa kumalizia mradi.

USHAURI KWA MKANDARASI
Bwaga manyanga, watakuua na kufurahia hilo wanasiasa wa awamu ya tano.
 
Ile ishu za MAKONDER...
 
Hehehe hii ibaki huku huku Wakenya tuijadili maana ni sababu kuu ya kwanini tunaongoza kuchumi, yani Kenya huwa full mzukaaaaa!!! Labda tukija kuajiriwa Bongo ndio kidgo huwa tunapumzika na kuhisi ni kama tuko likizo vile.....hehehe
Kiko wapi πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Nenda ujadili uchumi wenu na upunguze kuwashwa washwa
 
Awamu hii !!
mmmmh......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…