Nadhani haikuwa sahihi kwa waziri kuanza kumsema mkurugenzi mtendaji huyo wa Skol mbele ya vyombo vya habari mpaka kupelekea kuanguka na kupoteza fahamu, yule ni mlipa kodi na ameajiri mamia kwa maelfu sasa tukio lile halileti picha nzuri kwa taasisi/kampuni anayo iendesha tena mbele ya waajiriwa wake. Taratibu za mawasiliano zipo wazi katika mkataba na namna ya kuzitekeleza sio kuanza kuzodoana mbele ya vyombo vya habari kushushiana heshima kwa kiwango cha juu sana kunapaswa kukemewa na watu wote, maana leo yametokea kwa Skol kesho hatujui kwa nani? Haijalishi kama Skol walikuwa nyuma ya muda katika utekelezaji wao au vinginevyo kitendo kile cha kukemeana mbele ya waandishi sio sawa, pengine watu wanaweza sema mbona namba moja huwa anafanya hivyo hata nae wasaidizi wake wanapaswa kumwambia kuwa sio sawa.