Waziri Selemani Jafo amsema Mkurugenzi wa SCOL Building Contractors Limited hadi akaanguka na kuzimia

Waziri Selemani Jafo amsema Mkurugenzi wa SCOL Building Contractors Limited hadi akaanguka na kuzimia

....uhai wa mtu waeza potea ivi ivi..mkidhania anazuga kumbe yuko seriously...kaanguka hata huduma ya kwanza?
 
Safi Sana. Walizoea kufanya kazi Kwa mazoea. Kule kuambiwa kuwa amekatwa Milioni 85/- akaanguka. Jamani Barbara ya km 1 kujengwa Kwa miaka miwili Kweli?
Ushawahi kufanya kazi za Serekali ndugu? Tafuta ile clip mkandarasi analalamika kila akitoa hela watu wa halmashauri wanataka.

Acha tu wakandarasi wanafanya kazi mazingira magumu sana.
 
Mkandarasi mwenyewe anaonekana kabisa kashaliwa na mwezi kama nazi...
 
Hahaha HapAna Mkuu
Nilisubiri useme ndio tuu, ili nitafute namna ya kumuwajibisha Mkurugenzi was TBC kwa kuajiri insane person katika chombo cha taifa kinacho endeshwa na kodi zetu.
 
Nadhani haikuwa sahihi kwa waziri kuanza kumsema mkurugenzi mtendaji huyo wa Skol mbele ya vyombo vya habari mpaka kupelekea kuanguka na kupoteza fahamu, yule ni mlipa kodi na ameajiri mamia kwa maelfu sasa tukio lile halileti picha nzuri kwa taasisi/kampuni anayo iendesha tena mbele ya waajiriwa wake. Taratibu za mawasiliano zipo wazi katika mkataba na namna ya kuzitekeleza sio kuanza kuzodoana mbele ya vyombo vya habari kushushiana heshima kwa kiwango cha juu sana kunapaswa kukemewa na watu wote, maana leo yametokea kwa Skol kesho hatujui kwa nani? Haijalishi kama Skol walikuwa nyuma ya muda katika utekelezaji wao au vinginevyo kitendo kile cha kukemeana mbele ya waandishi sio sawa, pengine watu wanaweza sema mbona namba moja huwa anafanya hivyo hata nae wasaidizi wake wanapaswa kumwambia kuwa sio sawa.
 
Me nadhani tuwape makandarasi Wa nje wetu bado sio serious,au tuwaongezee jkt nguvu waijenge nchi.Check TBA wamebebwa awabebeki.Haya mambo ya uzawa ndo yanaturudisha nyuma check mradi Wa mabus ya mwendokasi alishinda tenda Mjerumani tukamwacha tukampa mzawa blah blah nyingi kila mtu shahidi.
 
kijereshi,
Ndo vizuri ili wengine wazikimbize kazi harakaharaka unapewa kila kitu unashindwa vipi kukimbiza kazi.Check kama yule Wa igunga Pesa unapewa kila mwaka miaka 4 sasa hata kilometa moja ya lami hakuna
 
Kwanini mmebagua sumaye?

Hii dhambi itawatafuna
Nilisubiri useme ndio tuu, ili nitafute namna ya kumuwajibisha Mkurugenzi was TBC kwa kuajiri insane person katika chombo cha taifa kinacho endeshwa na kodi zetu.
 
Waziri Jafo anaingia katika orodha ya watu wenye historia ya aina yake hapa nchini. Baada kucheza kwa kisigino pasi kama Ile ya 2015 ya Jecha kule Zanzibar, na kuifuingia CCM bao muhimu ktk uchaguzi wa 2019 wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji. Naona sasa anatema mistari ya vina mpaka watu wanapandisha mzuka na kuzimia.
 
Hizi taarifa ni kweli??
IMG-20191205-WA0021.jpeg
 
Back
Top Bottom