Waziri Simbachawene: Huwezi kumchukua aliyepata divisheni 1 ili akalinde benki au kucheza gwaride, lazima muelewe jamani

Wameshazoea kuwatumia polisi vile watakavyo, na polisi wamejiweka kwenye nafasi ya kutumiwa na wanasiasa kama wapendavyo. Heshima ya jeshi la polisi imeshuka. Kwahiyo kauli kama hizo wanatakiwa wazizoee tu!
 
Kwanza huyo waziri hafai kuendelea kubaki kwenye nafasi hadi dakika hii.

Unamdharau mlinzi kwamba hatakiwi kuwa na akili za darasani?

No, he has to go regardless of whether upon his own discovery he has messed up he apologizes or change statement that he was misquoted, he won't be tolerated at all; this is too much arrogance behaviour towards the accountable cops.
 
Jeshi la polisi litaendelea kuwa la hovyo na polisi wa hovyo hadi wabadili mifumo ya kuwapata hawa watu. Binafsi huwa nasikitika na kuona aibu ninapoongea na polisi wetu.
 
Mmeelewa vibaya ama mleta mada ameleta mada nusunusu. Nilivyomuelewa amesema wazi kuwa kutokana na mahitaji ya wakati huu ndioa maana wamechukua vijana hao, kwa kuzingatia hata maofisa waliohitimu karibu 2000+ lazima watahitajika wale makonstebo na ndio maana wamechukua hao vijana. Lkn pia ajira sio mwisho wake, miaka ijayo zitatoka na zitaeleza aina ya wahitaji.
 
Mwisho wa kufikiri kwa viongozi wa kisiasa hapo; wanatengeneza 'inferiority complexity' kwa wataoulinda benki ili wawaamuru kutenda chochote wanachotaka sio!!!

PGO iliyochambuliwa imefumua mengi mno pamoja na hicho anachokikataa
Hii Kauli ya Waziri inaweza sababisha Mgawanyiko Sana baina ya Askari na ni Kauli mbaya Sana ya kufanya Askari wetu Wadharaurike Mtaani.Kakosea sana Waziri.Hizi Kauli ndio Hufanya watu watuchukie CCM Kwa mambo ya Watu wachache ambao hawapimi wanachooongea kwenye Jamii ni kipi
Yupi yupo Sahihi Kati ya mleta mada au Wewe? Kwani hii Kauli sio nzuri kabisa
 
Watakaowekwa katika ngazi ya upelelezi itakuwaje? Naona waliofaulu vizuri lakini wakakosa nafasi waende polisi na si vingenevyo.
 
Kama kweli waziri kasema hivi basi ajitafakari Kama alijiandaa kabla ya kurekodi hicho kipindi
 
Mimi niko sahihi, mleta mada amekata kipande ili kuleta taharuki tu lkn alitoa ufafanunuzi yakinifu na wenye mashiko.
 
Duh! Simbachawene hebu jaribu kujiheshimu. Ng'ombe
 
Dah
 
Simbachawene Kalidharau Jeshi la Polisi na Kadhiririsha Jeshi Letu.Hii Kauli haikupaswa kuongelewa kabisa
 
Kwahio ndio maana wanatusumbua kumbe Vilaza wamejazana humo,wengine wamezeeka lakini akili za kushikiwa tu

Asante Waziri[emoji28]
 
wengi mnaolalama humu ni mapolice kama sivyo basi baba zenu au mama zenu ni mapolice.

Ila ukweli unauma. Waziri amesema ukweli. Ila sasa wabadilishe utaratibu watu washaelimika, wasomi wenye vigezo ni wengi mitaani. Wachukue wasomi waachane na kuajiri la saba na form four failure.

Nchi iende kisomi zaidi, na ndio lengo la taifa. Sasa nashangaa wao bado wanang'ang'ana na system za kizamani, akati wasomi wamejazana.
 
Undata niliukataaga katukatu. Sijawahi jutia kukataa ugali kwa mfumo wa kuwa afande.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…