Waziri Stergomena Tax ashiriki Ibada ya Pasaka Kigango cha Shishani Wilayani Magu

Waziri Stergomena Tax ashiriki Ibada ya Pasaka Kigango cha Shishani Wilayani Magu

Kumuengua Musukuma mwenye pesa sio rahisi kihivyo.Huyo Peneza ataishia kwenye viti maalumu

..Musukuma na genge zima la Magufuli wanakwenda kuenguliwa kwenye chama.

..Na Musukuma akijifanya mjanja wanakwenda kumbinya kwenye biashara zake.

..walimdhalilisha na kumtukana Upendo sasa Maza kaamua kumuinua.
 
Vipindi viwili kama ES wa SADC halafu unaishia kwenye kuwanafiki watu kwamba unawajali upate ubunge km njia ya kujikimu, hao wanaopendekeza watu wa aina hii kwenye nafasi za taasisi nje ya nchi wana matatizo makubwa! huwezi kukaa SADC miaka 8 ukakosa jambo zuri la kuifaa nchi kukuza uchumi..

Ukiona mtu wa aina hii, huhitaji kuuliza kama elimu na uzoefu vimesaidia kumbadilisha mtazamo kugoka kuwa tegemezi na kuwa wa kutegemewa..akili, maarifa, ujasiri, uvumilivu nk..nchi hii ina safari ndefu!
 
Eminza......kuna mpambano mkubwa unakuja hapo Magu dhidi ya mbunge wa sasa, nadhani pia unga wa miti utatumika sana, Tax awe makini tu asipigwe na locally made rocket propelled grenades, maana Magu miksa bariadi si haba, Japo Tax ni mtoto pendwa wa dola
 

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax, tarehe 31 Machi, 2024 ameungana pamoja na waumini wa Dini ya Kikristu katika ibada ya kusherekea Sikukuu ya Pasaka katika Kigango cha Shishani kilichopo Parokia ya Mtakatifu Kizito Kabila, Magu, chini ya Jimbo Kuu la Mwanza.

Akitoa salamu za Pasaka Parokiani hapo Waziri Dkt. Tax ameshukuru kupata wasaa wa kujumuika na Waumini katika Sikukuu hiyo muhimu kwa Wakristu duniani kote kukumbuka ufufuo wa Yesu Kristu.


Waziri Stergomena amechukua fursa hiyo kumshukuru Mungu kwa baraka anazoendelea kulipatia taifa letu ikiwa ni pamoja na mshikamano, amani na maendeleo katika sekta mbalimbali za kijamii na kiuchumi.

Aidha, ametoa rai kwa waumini wa Parokia ya Mtakatifu Kizito kuendelea kuiombea Tanzania pamoja na Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na viongozi wanaomsaidia katika nafasi mbalimbali. Waziri Tax ameshiriki ameahidi kuendelea kuchangia kwenye ujenzi wa kanisa unaoendelea kila apatapo nafasi kuwa yeye ni sehemu ya Kata ya Shishani.


Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Kizito Kabila, Padri Andrea Buhembo, amemshukuru Waziri Stergomena Tax kwa moyo wa upendo na ukarimu aliounyesha wa kujiwekea utaratibu wa kukumbuka kwao katika hali zote amekuwa akishiriki kwa namna moja ama nyingine katika shughuli za kijamii na kiimani.

Hii nayo ni habari?
 
Eminza......kuna mpambano mkubwa unakuja hapo Magu dhidi ya mbunge wa sasa, nadhani pia unga wa miti utatumika sana, Tax awe makini tu asipigwe na locally made rocket propelled grenades, maana Magu miksa bariadi si haba, Japo Tax ni mtoto pendwa wa dola
Sasa mtoto mzuri kama Stregomena Tax anagombea maubunge ya nini? Miaka yote aliofanya kazi ajapiga hela za kutosha tu kujiwekeza? au anatafta kufa tu kifo cha ajabu ajabu.
 
Mwanamke akiingia katika siasa huvuruga mambo mengi, mifano iko wazi, hata Bona, mumewe alikesha akimtafutia kura, akatumia na mali zake, akaishia kukamata live pale Dodoma
Mwanamke ukimpa power ya kiuchumi tayari umemkosa. Wachache sana wanaweza himili kupata fedha nyingi kwa ghafla
 
Back
Top Bottom