Sijajua lengo lako ni nini?Wewe utakua na mambo yako binafsi mbele ya huyu mama!!
Umekazana sana na PhD sijui ya Japan na blah blah nyingi! Stergomena ndiye mtu wa kwanza nchi hii kuwa na PhD na akabebwa? Hivi PhD kwako ndo kipimo cha akili na utendaji bora kwa mtanzania??
Unaonekana huna facts:: unasema huyu ndo msomi wa kwanza kuongoza wizara ya ulinzi? Vipi Prof Kapuya? Prof Sarungi?
Tangu lini nchi hii ukiwa na PhD tu ndo unakua katika shortlist ya Rais? Are you sure? Aisee ni wazi una mambo binafsi na huyu mama maana umeandika kwa hisia sana. Nani kamdhalilisha huyu mama? Huyu mama mimi namfahamu binafsi kitambo sana na nimefanya naye kazi kwa karibu nikiwa MFA nayeye akiwa SADC!!
Eti amegombea unazijua taratibu za kumpata Katibu wa SADC? Unajua anapendekezwaje kwenda huko?
Kuna wasomi wangapi wamepitia vyuo bora kabisa duniani ni wajinga kupindukia utadhani hawajaenda shule?
Kwq taarifa yako zaidi ya 70% ya viongozi wenye PhD serikalini walizipata huko duniani kwenye vyuo bora sana na hizo nafasi walizipata kwa dirisha la msaada kwa nchi za maskini wengi tu na tunauona ujinga wao!!
Nimekushangaa sana kuhusudu PhD ya Japan eti ndo SI Unit kwako kupima kiongozi bora!! Sijaona hoja uliyoweka kuthibitisha bora wa huyu mama zaidi ya ngonjera za PhD ya Japan.
Kuwa bold mkuu.