Waziri Stergomena Tax ashiriki Ibada ya Pasaka Kigango cha Shishani Wilayani Magu

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax, tarehe 31 Machi, 2024 ameungana pamoja na waumini wa Dini ya Kikristu katika ibada ya kusherekea Sikukuu ya Pasaka katika Kigango cha Shishani kilichopo Parokia ya Mtakatifu Kizito Kabila, Magu, chini ya Jimbo Kuu la Mwanza.

Akitoa salamu za Pasaka Parokiani hapo Waziri Dkt. Tax ameshukuru kupata wasaa wa kujumuika na Waumini katika Sikukuu hiyo muhimu kwa Wakristu duniani kote kukumbuka ufufuo wa Yesu Kristu.

Waziri Stergomena amechukua fursa hiyo kumshukuru Mungu kwa baraka anazoendelea kulipatia taifa letu ikiwa ni pamoja na mshikamano, amani na maendeleo katika sekta mbalimbali za kijamii na kiuchumi.

Aidha, ametoa rai kwa waumini wa Parokia ya Mtakatifu Kizito kuendelea kuiombea Tanzania pamoja na Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na viongozi wanaomsaidia katika nafasi mbalimbali. Waziri Tax ameshiriki ameahidi kuendelea kuchangia kwenye ujenzi wa kanisa unaoendelea kila apatapo nafasi kuwa yeye ni sehemu ya Kata ya Shishani.

Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Kizito Kabila, Padri Andrea Buhembo, amemshukuru Waziri Stergomena Tax kwa moyo wa upendo na ukarimu aliounyesha wa kujiwekea utaratibu wa kukumbuka kwao katika hali zote amekuwa akishiriki kwa namna moja ama nyingine katika shughuli za kijamii na kiimani.

Usiseme siku muhimu kwa wakristo sema sikukuu muhimu kwa wakatoliki. Hii ni siku ya kipagani kwa sisi wakristo WA kweli wa efata.
 
..Musukuma na genge zima la Magufuli wanakwenda kuenguliwa kwenye chama.

..Na Musukuma akijifanya mjanja wanakwenda kumbinya kwenye biashara zake.

..walimdhalilisha na kumtukana Upendo sasa Maza kaamua kumuinua.
Sijajua usafi wa pendo peneza,,Huyu dada na baba yake ndo wamekua wanawalagainwananchi vinavyozunguka mgodi wa TemboNickel huko ngara ili wao walipwe fedha nyingi nakuwaacha wanna hi wakiwa maskini.Huyo oeneza siyo mtanzania wa asili bali ni mnyarwada
 
Vipindi viwili kama ES wa SADC halafu unaishia kwenye kuwanafiki watu kwamba unawajali upate ubunge km njia ya kujikimu, hao wanaopendekeza watu wa aina hii kwenye nafasi za taasisi nje ya nchi wana matatizo makubwa! huwezi kukaa SADC miaka 8 ukakosa jambo zuri la kuifaa nchi kukuza uchumi..

Ukiona mtu wa aina hii, huhitaji kuuliza kama elimu na uzoefu vimesaidia kumbadilisha mtazamo kugoka kuwa tegemezi na kuwa wa kutegemewa..akili, maarifa, ujasiri, uvumilivu nk..nchi hii ina safari ndefu!
Mbona wote walioki serikalini ndo maisha Yao yakuchuma serikalini na kustaf wakisubiri kula mafao
 
Kwanini huyu mama aliachana na jina la Bamwenda?
Hebu ongeza nyama kidogo mkuu nasi tuyajue ma2,ma3 kuhusu yeye na hilo jina la Bamwenda.

Isije ikawa ni mambo ya kutalikiana ndiyo yalisababisha.
 
Enzi hizo akiwa mwalimu akiitwa Stergomena Tax Bamwenda.... baada ya kuanza kupanda ngazi za mamlaka nikakutana nae siku moja nikaona amelikata hilo jina la Bamwenda na kuishia kwenye Lawrence Tax....

Namimi kabla sijaongeza yakwangu natamani kujua toka kwa watu wa karibu ilikuaje?
 
Vipindi viwili kama ES wa SADC halafu unaishia kwenye kuwanafiki watu kwamba unawajali upate ubunge km njia ya kujikimu, hao wanaopendekeza watu wa aina hii kwenye nafasi za taasisi nje ya nchi wana matatizo makubwa! huwezi kukaa SADC miaka 8 ukakosa jambo zuri la kuifaa nchi kukuza uchumi..

Ukiona mtu wa aina hii, huhitaji kuuliza kama elimu na uzoefu vimesaidia kumbadilisha mtazamo kugoka kuwa tegemezi na kuwa wa kutegemewa..akili, maarifa, ujasiri, uvumilivu nk..nchi hii ina safari ndefu!
Huyo mama hajawahi kupambana mwenyewe ktk maisha yake... all her life amebebwa tangu akiwa mwalimu hadi kuwa mkuu wa SADC!!

Hata huo ubunge alonao kachotewa kwenye sahani na sidhani hata kama anaweza kupiga kampeni... inshore hata uwaziri anabembelezwa kama mtoto aendelee nao.
 
..Dr.Stergomena Tax jimbo la Magu.

..Upendo Peneza jimbo la Geita vijijini.

..Joseph Musukuma anakwenda kuenguliwa.

..
Huyu mama hawezi gombea ubunge!! Hata kutamka CCM oyee tu hawezi!! Katika mazingira ya sasa huyu mama hatoboi....

Maisha yake yote kazoea kubebwa beware sana na wenye maamuzi hasa kwa vileeee.... kajichokea sana huo uwaziri tu anabembelezwa tu....
 
Enzi hizo akiwa mwalimu akiitwa Stergomena Tax Bamwenda.... baada ya kuanza kupanda ngazi za mamlaka nikakutana nae siku moja nikaona amelikata hilo jina la Bamwenda na kuishia kwenye Lawrence Tax....

Namimi kabla sijaongeza yakwangu natamani kujua toka kwa watu wa karibu ilikuaje?
Hiyo kawaida sana mkuu. Hapa jijini Dar kuna mbunge wa kike ambaye naye alikuwa mwalimu kabla ya kuingia kwenye siasa jina lake la awali alikuwa anaitwa Bonnah Moses Kaluwa.

Baada ya mumewe Dr. Kaluwa kumfumania huko Dodoma akila uroda na Anthony Mavunde akavunja ndoa na kufungua kesi ya kumtaka mbunge huyo wa sasa wa Jimbo la Segerea kukoma kutumia jina lake. Hivyo amelazimika kuondoa jina Kaluwa. Hivi sasa anaitwa Bonnah Moses (...sijui nani nani).
 
Huyu mama hawezi gombea ubunge!! Hata kutamka CCM oyee tu hawezi!! Katika mazingira ya sasa huyu mama hatoboi....

Maisha yake yote kazoea kubebwa beware sana na wenye maamuzi hasa kwa vileeee.... kajichokea sana huo uwaziri tu anabembelezwa tu....

..Dr.Stergomena ana PhD toka Japan.

..amefanya kazi serikalini na akapanda ngazi kama watumishi wengine, mpaka ikaonekana anafaa kuwa Katibu Mkuu wa Sadc.

..kusema kwamba amebebwa sio sahihi. Pia tusimhukumu kwa muonekano wake.
 
Sijajua usafi wa pendo peneza,,Huyu dada na baba yake ndo wamekua wanawalagainwananchi vinavyozunguka mgodi wa TemboNickel huko ngara ili wao walipwe fedha nyingi nakuwaacha wanna hi wakiwa maskini.Huyo oeneza siyo mtanzania wa asili bali ni mnyarwada

..Upendo na babaye wanawadanganya kivipi wananchi?

..hebu fafanua hoja yako ili tukuelewe.

..kama amezaliwa na kusomea Tanzania huyo ni mwenzetu hata kama wazazi ni Wanyarwanda.
 
..Dr.Stergomena ana PhD toka Japan.

..amefanya kazi serikalini na akapanda ngazi kama watumishi wengine, mpaka ikaonekana anafaa kuwa Katibu Mkuu wa Sadc.

..kusema kwamba amebebwa sio sahihi. Pia tusimhukumu kwa muonekano wake.
Namfahamu huyu mama tangu akiwa mwalimu hadi kuwa katibu mkuu wizara fulani kisha SADC!! Siongei kwa kukisia huyu mama bila JK asingefika hapo alipo!! Huyu mama kuna kipindi akiwa MFA alichoka kabisa mwisho wa siku akamuomba Samia amrudishe ulinzi kusiko na heka heka....

Kipindi TZ inatakiwa kutoa katimku mkuu wa SADC kulikua na vichwa wengi tu waliopendekezwa akapelekwa huyu mama na kulidorora sana huko SADC!

Hiyo kumhukumu labda umemhukumu wewe mi nimetoa tu wasifu wake....

Bottom line: Kwanini siku hizi hatumii tena jina la Bamwenda?
 
..hakuna mtu serikalini au kwenye siasa anayepanda kwa nguvu zake mwenyewe bila msaada wa wakubwa zake.

..tatizo mtu huyo anapokuwa mwanamke basi anaanza kupewa sifa mbaya za kumvunjia heshima na utu wake. Utamaduni huo sio mzuri.

..Dr.Stergomena ni msomi wa ngazi ya PhD aliyoipata Japan. Mtumishi wa serikali akiwa na PhD moja kwa moja anakuwa ktk shortlist ya kupata uteuzi wa Raisi.

..Hivyo ndivyo huyu Mama alivyopanda ngazi akiwa serikalini na haswa akitumikia ktk Wizara ya Fedha.

..Nafasi ya Katibu Mkuu wa SADC huwa ya ushindani. Sio suala la zamu kwa nchi wanachama. Na wahusika hufanyiwa usaili ikiwemo na wakuu wa nchi za SADC. Dr. Stergomeno alipitia mchakato wa ushindani na wagombea wengine na akaibuka kidedea.

..Sasa unaweza kusema alibebwa ktk hatua ya kupendekezwa na serikali ya Tz. Swali linakuja, kama alikuwa hafai, au hana sifa, aliwezaje kushinda mchakato unaohusisha kusailiwa na nchi zote wanachama wa Sadc?

..Kwa maoni yangu huyu Mama amesoma vizuri na ana uwezo. Huenda kihistoria ndiye Waziri wetu wa ulinzi mwenye elimu kubwa, na uzoefu wa kimataifa, kuliko watangulizi wake.
 
Wewe utakua na mambo yako binafsi mbele ya huyu mama!!

Umekazana sana na PhD sijui ya Japan na blah blah nyingi! Stergomena ndiye mtu wa kwanza nchi hii kuwa na PhD na akabebwa? Hivi PhD kwako ndo kipimo cha akili na utendaji bora kwa mtanzania??

Unaonekana huna facts:: unasema huyu ndo msomi wa kwanza kuongoza wizara ya ulinzi? Vipi Prof Kapuya? Prof Sarungi?

Tangu lini nchi hii ukiwa na PhD tu ndo unakua katika shortlist ya Rais? Are you sure? Aisee ni wazi una mambo binafsi na huyu mama maana umeandika kwa hisia sana. Nani kamdhalilisha huyu mama? Huyu mama mimi namfahamu binafsi kitambo sana na nimefanya naye kazi kwa karibu nikiwa MFA nayeye akiwa SADC!!

Eti amegombea unazijua taratibu za kumpata Katibu wa SADC? Unajua anapendekezwaje kwenda huko?

Kuna wasomi wangapi wamepitia vyuo bora kabisa duniani ni wajinga kupindukia utadhani hawajaenda shule?

Kwq taarifa yako zaidi ya 70% ya viongozi wenye PhD serikalini walizipata huko duniani kwenye vyuo bora sana na hizo nafasi walizipata kwa dirisha la msaada kwa nchi za maskini wengi tu na tunauona ujinga wao!!

Nimekushangaa sana kuhusudu PhD ya Japan eti ndo SI Unit kwako kupima kiongozi bora!! Sijaona hoja uliyoweka kuthibitisha bora wa huyu mama zaidi ya ngonjera za PhD ya Japan.

Kuwa bold mkuu.
 
Back
Top Bottom