Waziri Stergomena Tax ashiriki Ibada ya Pasaka Kigango cha Shishani Wilayani Magu

Kumuengua Musukuma mwenye pesa sio rahisi kihivyo.Huyo Peneza ataishia kwenye viti maalumu

..Musukuma na genge zima la Magufuli wanakwenda kuenguliwa kwenye chama.

..Na Musukuma akijifanya mjanja wanakwenda kumbinya kwenye biashara zake.

..walimdhalilisha na kumtukana Upendo sasa Maza kaamua kumuinua.
 
Vipindi viwili kama ES wa SADC halafu unaishia kwenye kuwanafiki watu kwamba unawajali upate ubunge km njia ya kujikimu, hao wanaopendekeza watu wa aina hii kwenye nafasi za taasisi nje ya nchi wana matatizo makubwa! huwezi kukaa SADC miaka 8 ukakosa jambo zuri la kuifaa nchi kukuza uchumi..

Ukiona mtu wa aina hii, huhitaji kuuliza kama elimu na uzoefu vimesaidia kumbadilisha mtazamo kugoka kuwa tegemezi na kuwa wa kutegemewa..akili, maarifa, ujasiri, uvumilivu nk..nchi hii ina safari ndefu!
 
Eminza......kuna mpambano mkubwa unakuja hapo Magu dhidi ya mbunge wa sasa, nadhani pia unga wa miti utatumika sana, Tax awe makini tu asipigwe na locally made rocket propelled grenades, maana Magu miksa bariadi si haba, Japo Tax ni mtoto pendwa wa dola
 
Hii nayo ni habari?
 
Sasa mtoto mzuri kama Stregomena Tax anagombea maubunge ya nini? Miaka yote aliofanya kazi ajapiga hela za kutosha tu kujiwekeza? au anatafta kufa tu kifo cha ajabu ajabu.
 
Mwanamke akiingia katika siasa huvuruga mambo mengi, mifano iko wazi, hata Bona, mumewe alikesha akimtafutia kura, akatumia na mali zake, akaishia kukamata live pale Dodoma
Mwanamke ukimpa power ya kiuchumi tayari umemkosa. Wachache sana wanaweza himili kupata fedha nyingi kwa ghafla
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…