Waziri anakosea anapokiri bima ya afya NHIF inakaribia kufa, kwanini wasitafute njia mbadala itakayowawezesha kumudu hayo mazingira ya kuongezeka gharama za matibabu?
Kuna watu wanaweza kupoteza ajira zao hapo kutokana na kufa kwa hicho kitengo, wasiwe wepesi kukiri kushindwa bila kwanza kutafuta majibu ya changamoto zinazoukabili huo mfuko.
Mfano, kama inapoonekana gharama za matibabu anazopata mwanachama ni kubwa zaidi ya kile anachochangia mwanachama, kwanini NHIF wasigawane gharama za matibabu na mwanachama 50/50 ili kuepuka tatizo la mfuko kuzidiwa na gharama mwishowe kutengeneza madeni?
Hili nimeona linatokea kwa bima nyingine za afya, licha ya wanachama kulipiwa na mifuko hiyo, bado hutakiwa kutoa sehemu nyingine za gharama ya matibabu yao toka mifukoni mwao ili kufidia nyongeza ya kile wasichochangia kwenye bima zao za afya.
Kama hilo lisipowezekana, basi nashauri kiasi cha pesa anazochangia mwananchama ambaye ni mgonjwa wa hayo magonjwa makubwa yasiyoambukiza kiongezwe ili kuendana na gharama halisi za matibabu yao.