Waziri Ummy: Bima ya Afya (NHIF) inakaribia kufa

Alianzisha au alicopy na kupaste kutoka nchi nyingine
 
Mwananchi apewe ruhusa kuchagua bima ya afya. Ataingia makubaliano yeye binafsi ie makato, coverage. NHIF inaendeshwa kisiasa zaidi. Bunge plus wizara are to blame. This was pointed out by the CAG. What action was taken???
 
Watumiaji wakubwa wa NHIF ni watumishi wa serikali na mashirika ya umma. Niliwahi kuuliza humu nikajibiwa kwamba wanakatwa 3% ya mshahara kama ada ya uanachama. Maana yake anayepokea milioni moja kwa mwezi atakatwa 30,000 na kwa mwaka 360,000.

Kijana wa miaka 25 anachangia zaidi ya 500,000 kwa mwaka kama si muajiriwa. Mfanyakazi anapata huduma kwa hadi watu sita. Mtu binafsi ni yeye peke yake.

Hawa wanaochangia binafsi wamepunguziwa huduma ambazo wafanyakazi na wategemezi wao wanapata pamoja na kwamba wao wanalipa zaidi ya wafanyakazi.

Hili linahitaji kuangaliwa.
 
Changamoto huo mfuko wanaua wenyewe wanaenda kukopa matokeo yake hawalipi madeni, staff wa NHIF wanalipana posho na kucheza dili.
 
Mwananchi apewe ruhusa kuchagua bima ya afya. Ataingia makubaliano yeye binafsi ie makato,coverage. NHIF inaendeshwa kisiasa zaidi. Bunge plus wizara are to blame. This was pointed out by the CAG. What action was taken???
Unahisi unaweza changia strategies, jubilee? Hawa gharama zao kwa mwaka ni kubwa sana ila wanakulimit kutibiwa mwisho 500,000 kwa mwaka.
 
Hata mimi nimeliongelea hili swala

Kuwa wanaokwamisha huu mfuko ni wafanyakazi wa Serikali na wategemezi wao.

Serikali kunusuru huu mfumo wabadilishe mfumo wa matibabu, mtu atibiwe kulingana na michango yake, tegemezi waondolewe.
 
Kitakachoiua NHIF siyo gharama za matibabu bali udanganyifu. Natamani ningekuwa na mamlaka nchi hii ili nioneshe mfano ila ndio hivyo wenye mamlaka wengi uwezo ndo hivyo na wenye uwezo wengi hawana mamlaka.
 
Kitakachoiua NHIF siyo gharama za matibabu bali udanganyifu. Natamani ningekuwa na mamlaka nchi hii ili nioneshe mfano ila ndo hivyo wenye mamlaka wengi uwezo ndo hivyo na wenye uwezo wengi hawana mamlaka.
Huu ndio ukweli, Kuna mmoja alinisimulia kinachofanyika Muhimbili nikabaki nashangaa tu. Kuna udanganyifu mkubwa usio wa kawaida.
 
Wakati mikakati ya kuboresha huduma za afya ikiendelea kuwekwa, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amebainisha dalili za kufa kwa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kutokana na kulemewa na madeni ya matibabu ya wanachama wake...
Mfuko bado uko imara kuendelea kutekeleza majukumu yake ikiwemo kufanya malipo kwa wanufaika wake.

Hatua zinazotakiwa kuchukuliwa kwa sasa ni wananchi wengi zaidi kujiunga ili kuimarisha zaidi uhai wake.
 
Wakati mikakati ya kuboresha huduma za afya ikiendelea kuwekwa, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amebainisha dalili za kufa kwa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kutokana na kulemewa na madeni ya matibabu ya wanachama wake...
Dhana ya Mfuko ni kuchangia kabla ya kuugua ili uwe na uhakika wa kutibiwa hata kama huna fedha kwa kutumia kadi ya bima ya Afya.

Pamoja na kuwepo kwa utofauti wa michango viwango vya huduma za matibabu vipo sawa kwa kila mwanachama na hakuna ukomo wa huduma kulinga na kiwango ulichochangia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…