Waziri Ummy: Masoko na Stendi zote zinazomilikiwa na TAMISEMI kujengewa Visima vya Maji ili kukabiliana na moto

Waziri Ummy: Masoko na Stendi zote zinazomilikiwa na TAMISEMI kujengewa Visima vya Maji ili kukabiliana na moto

Angetafuta ushauri wa kitaalamu kabla ya kutoa kauli hiyo ya ajabu. Hivi hajui kuwa visima vinaweza kuwepo na visiwe na maji?
Kujenga visima pekee bila kutoa elimu ya kuzingatia taratibu za "emergency preparedness and response plans" nadhani si suluhisho!
Akajipange tena!
 
Leo ndo wamekumbuka au?
Wazee wa matukio!!yaani miaka yote hiyo hilo ndio wanaliona leo yaani serikali za kiafrika bwana!!nakwambia hakuna kitakachofanyika, yaani badala ya kuzungumzia kuweka vituo vya kuchukulia maji(water hydrants) karibia maeneo yote ya mji, unazungumzia visima kwenye masoko/stendi? Kesho ikiungua hospital tunachimba tena kisima hapo hospital?!!ee bwana akili zetu waafrika tunazijua wenyewe.POTELEA PWETEE MUNGU NDIO ANATULINDA
 
Waziri wa Tamisemi mh Ummy Mwalimu amesema Serikali itajenga visima vya maji kwenye masoko na stendi za mabasi zote zinazomilikiwa na Halmashauri ili kukabiliana na majanga ya moto pindi yanapojitokeza.

Chanzo: Radio One
Kwamba moto unazimwa na maji haya ya dawasco??? Kwamba nabi ya fire extinguisher kuna maji?
Khee
 
Magari ya washawasha hapa Tanzania hayajawahi kukosa maji japokuwa yale maji yake ni more technical na ni gharama zaidi ila magari ya zimamoto ambayo maji yake ni ya kawaida hayana maji.Mtu mweusi ni Kima aliechangamka🐒🐒🐒
 
Wazee wa matukio!!yaani miaka yote hiyo hilo ndio wanaliona leo yaani serikali za kiafrika bwana!!nakwambia hakuna kitakachofanyika, yaani badala ya kuzungumzia kuweka vituo vya kuchukulia maji(water hydrants) karibia maeneo yote ya mji, unazungumzia visima kwenye masoko/stendi? Kesho ikiungua hospital tunachimba tena kisima hapo hospital?!!ee bwana akili zetu waafrika tunazijua wenyewe.POTELEA PWETEE MUNGU NDIO ANATULINDA
Tanzania ni kisiwa cha amani bwana Mungu anatupenda, tuzidi kumwomba tu atatusaidia😆😆
 
Bora hivyo visima vichimbwe kwenye vituo vya zima moto ili upatikanaji wa maji kwa magari yao uwe rahisi, na si kila moto unataka uzimwe na maji.
Inshu sio visima kuchimbwa wapi, sasa wakivichimba kwwnye vituo vya zima mto mfano pale fire, moto unatokea mbagala hicho kisima kitakuwa na msaada gani?!!unaposema sio kila moto unazimwa na maji, ni kweli lakini vyovyote vile lazima maji yahitajike tu ktk uchanganyaji wa hizo chemikali, kutegemea na kundi la moto husika, ndio maana hakuna gari la zima moto lenye kutumia mchanga ktk kuzima moto,.cha msingi ni kujenga water hydrants kila sehemu za mji na ziwe na maji muda wote hii nayo ni changamoto nyingine!! ili moto kila sehemu unapotokea upatikanaji wa maji unakuwa karibu hapo!!
 
Na ukichimba kisima kwa mazingira ya stand ni lazima uweke na pampu ya kuvuta maji,sasa pampu nayo inatumia umeme.....mpaka hapo sijaelewa lengo la Waziri Ummy Mwalimu ni nini,
 
Back
Top Bottom