Volatility
JF-Expert Member
- Aug 22, 2018
- 3,935
- 7,513
Mkuu, hao watu mara zote wamekuwa wakishindwa kudhibiti majanga ya moto na mara zote wamekuwa wakisingizia kuishiwa maji au miundombinu mibovu kufikia maeneo ya tukio.Shida ya fire brigade ni aina ya watu waliopo pale siyo vifaa wala maji, ni wajanjawajanja fulani, hata mwaka ule nyumba ya Rais (kama sijakosea Mkapa) ilipoungua walisuasua mpaka wakalalamikiwa Bungeni, nadhani ili kufupisha hadithi kikosi kifumuliwe kiundwe kitu kingine kabisa
huu moto wa kariakoo kwao naufananisha na zoezi la kutest uwezo wao, kwa sababu hakuna kitu unaweza sema ni impediment iliyokuwapo, magari yapo,maji yapo,askari wapo,na jengo lenyewe ukiliangalia lilijengwa katika namna ambayo ni friendly kabisa kukabiliana na majanga.
kwa nini wameshindwa?
tunatakiwa kupata majibu badala ya kukubali kuentertain statement za hovyo kama za umi, yaani katikati ya failure kubwa namna hii anajitokeza waziri anatoa ahadi, hii na dharau au upumbavu?