Waziri Ummy: Masoko na Stendi zote zinazomilikiwa na TAMISEMI kujengewa Visima vya Maji ili kukabiliana na moto

Waziri Ummy: Masoko na Stendi zote zinazomilikiwa na TAMISEMI kujengewa Visima vya Maji ili kukabiliana na moto

Shida ya fire brigade ni aina ya watu waliopo pale siyo vifaa wala maji, ni wajanjawajanja fulani, hata mwaka ule nyumba ya Rais (kama sijakosea Mkapa) ilipoungua walisuasua mpaka wakalalamikiwa Bungeni, nadhani ili kufupisha hadithi kikosi kifumuliwe kiundwe kitu kingine kabisa
Mkuu, hao watu mara zote wamekuwa wakishindwa kudhibiti majanga ya moto na mara zote wamekuwa wakisingizia kuishiwa maji au miundombinu mibovu kufikia maeneo ya tukio.

huu moto wa kariakoo kwao naufananisha na zoezi la kutest uwezo wao, kwa sababu hakuna kitu unaweza sema ni impediment iliyokuwapo, magari yapo,maji yapo,askari wapo,na jengo lenyewe ukiliangalia lilijengwa katika namna ambayo ni friendly kabisa kukabiliana na majanga.

kwa nini wameshindwa?

tunatakiwa kupata majibu badala ya kukubali kuentertain statement za hovyo kama za umi, yaani katikati ya failure kubwa namna hii anajitokeza waziri anatoa ahadi, hii na dharau au upumbavu?
 
Nilishangaa eneo kama Kariakoo, center yenye mkusanyiko Mkubwa na biashara, eti inakosa Fire Hydrant ya Maji....

Sekta ya Zimamoto wamefeli sana ktk hili.....

Sent from my TECNO LA7 using JamiiForums mobile app
 
Angetafuta ushauri wa kitaalamu kabla ya kutoa kauli hiyo ya ajabu. Hivi hajui kuwa visima vinaweza kuwepo na visiwe na maji?
Kujenga visima pekee bila kutoa elimu ya kuzingatia taratibu za "emergency preparedness and response plans" nadhani si suluhisho!
Akajipange tena!
😇
 
Tumelisema hili baada ya tukio ila kauli zao wakati mwingine bila kujieleza ilikuwa wafanye tu

Fire hydrants zinahitajika sehemu nyingi tu sio kwenye masoko tu

Utakuta wanajenga visima vya maji kama vya nyumbani [emoji23]
 
ni maji tu ya kawaida ama ni kama yale ya zima moto, maana maji ya kawaida si mazuri kwa uzimaji wa moto hasa unaotokana na hitilafu ya umeme.
 
Kumbe fire hawana reserve ya maji pale ofisini kwao,aibu sana pambafu kabisa
 
Bado tunatatizo kubwa sana hasa katika kuamua kufanya 'preventive measures' badala yake kila uchwao tunakomaa na 'corrective measures' hii ni mbaya sana.
 
Kutoboa kisima shingapi? Hebu acha utoto basi.

Pesa za choose za stand kwa mwezi mmoja tu zinatosha kutoboa kisima
Nimekubali utoto,
Ukubwa huo ungetumika kutoboa visima vijijini tusingelalamika maji.
 
Uwekezaji uliopo kariakoo unakosa hydrants pipe za kuzimia moto? Nimeamini msemo wa"Entrepreneur is a risk taker"
 
Hii nchi ina fiongosi khe yah fiongosi
Badala ya kujenga sanamu za wafu jengeni miundo mbinu sasa visima vya nini mnataka magorofa ya wenyewe yaanze kuanguka
Kwa nini huwa hamshauriani na wataalamu kabla ya kuja kumwaga upupu wenu
Kila mtu anasema mara kamati mara siku saba mara wakijulikana mara visima
Kwa nini asiseme mtu mmoja kutoa mwongozo
Akili zenu zinafikiria wapi mtapiga deal

Swala la visima ni kujidanganya na kuwadanganya wenye pesa walipa kodi
 
Waziri wa Tamisemi mh Ummy Mwalimu amesema Serikali itajenga visima vya maji kwenye masoko na stendi za mabasi zote zinazomilikiwa na Halmashauri ili kukabiliana na majanga ya moto pindi yanapojitokeza.

Chanzo: Radio One
Majibu mepesi kwa maswali magumu

Amandla...
 
Waziri wa Tamisemi mh Ummy Mwalimu amesema Serikali itajenga visima vya maji kwenye masoko na stendi za mabasi zote zinazomilikiwa na Halmashauri ili kukabiliana na majanga ya moto pindi yanapojitokeza.

Chanzo: Radio One
Bora ameongeza neno '.........vya maji'
Hata hivyo naiona sababu ya JPM kuwaambia wanaoandika EIA kwamba ni upuuzi tu. Yapo mengi ambayo hayajafanyika ktk mikusanyiko hii.
 
Hakuhitajiki kauli za kukurupuka. Badala uake kunatakiwa kuwa na mpango maalum wa kuangalia namna ya kushughulikia majanga. Janga siyo moto pekee yake.

Wanatakiwa watu wenye uwezo wa kuyaona majanga kabla hayajatokea. Hao ndio wanaweza kutengeneza action plan ya kushugjulikia majanga ya aina mbalimbali.
Tatizo mkuu hao wateule wa kisiasa wanadhani wana majibu yote kwenye figure tips.Bora hata angejiongeza akatumia AI(Artificial intelligence)Ingempa perfect answers kuliko kukurupuka.
 
Kwanini nchi hii inamiliki MAVI8 mengi kuliko mahitaji ya maji ambalo ni hitaji la lazima
 
Back
Top Bottom