Waziri Ummy Mwalimu: Maambukizi COVID-19 ya ndani kwa ndani yameanza, Watanzania wajiandae kwa maambukizi ya Jumuiya

Kwa kipindi kile Covid 19 imezidi China kama huvai Mask unaweza kujikuta matatani na Serikali.

Je walikuwa wana maambukizi raia wote?
 
Watendaji na wataalam wetu tuwaonee huruma ya bure, wanapata wakati mgumu sana kuelezea hili janga kufuatia hitimisho na msimamo wa mkuu wetu juu ya gonjwa hili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
tunaendelea kusema na kushari kama tulivyo shauri hapo awali! gonjwa halina tiba wala kinga, bado tunaingiza watu nchini, bado uhamasishaji ni mdogo dhidi ya mikusanyiko,,,, mnataka tushauri vipi ndio tueleweke, hapa hatupigani wala hatushindani na mtu, wala hakuna siasa wala uchama, ni maslai ya watanzania wote na familia zetu, watoto wetu pia, tanzania tunajijua tulivyo lafu na wajuaji,kila mtu anataka kujifanya mjuaji,mikusanyiko,mikusanyiko bado tunakusanyika ni hatari.

ushauri kwa serikali: serikali ije na mbinu mbadala katika kupima nyumba kwa nyumba pia na kufunga safari zote za mikoani na nje ya nchi kwa muda, pasipo kufanya hivyo dalili sio nzuri, kabisa leo 14,kesho unakuta 26 mtondogo 200, hatutaki tufikie huko, this is secondary risk, avoiding one risk create another risk, tunajalibu kuepuka risk ya kudolola kwa uchumi lakini tunatengeneza risk ya maambukizi makubwa sana, kwa kuwaruhusu watu waendelee kukusanyika sokoni na mahala pengine,kama usafiri nk.

basi tuchague moja, tuumie kwa muda kudhibiti corona, au tujiachie nakuendelea kujichanganya itughalimu kama USA na ulaya? na hapa ndipo LEADERSHIP hupimwa!!!!!!!!!

asante.
 
Tanzania hakuna mtu mjuaji bali umbumbu, uzwazwa na umasikini ndiyo unatusumbua?
 
Kenya sasa hivi wametangaza watakuwa wanapima watu 35,000 kwa siku baada ya kupata vifaa vya kupimia 'Testing Kits'.

Sisi hatutaki kupima lkn tunatoa takwimu za wale Confirmed Cases only ambao kinadharia wanaonekana wachache pamoja na kwamba serikali inafahamu wazi kuwa huu ugonjwa ni "Highly Asymptomatic" kwa wale wenye nao.

Serikali iingie gharama iagize Test Kits watu wapimwe iache kuchukulia fedha za umma kama za mtu au watu fulani pia iache kulitumia hili janga kutafuta sifa feki za kisiasa.

Nini mantiki ya kuwambia watu waepuke mikusanyiko at the same time unaruhusu watu kwenye nyumba za ibada hii Irony maana yake nini, wakati Mungu ni "Omnipresent" anaweza akaabudiwa popote.
 
Nimeyajibu maswali haya kuhusu ugonjwa wa Corona (COVID-19):
1. Je vitamini husaidia kinga ya mwili dhidi ya Ugonjwa wa Corona?

2. Je kusukutuwa mdomo na maji ya chumvi husaidia kujikinga na Corona?

3. Je virusi vya Corona vinaweza kusambaa kwa mfumo wa mawasiliano wa 5G?

4. Je virusi vya Corona ni silaha iliyotengenezwa na China?

5. Je taarifa potofu kuhusu ugonjwa wa Corona hutoka wapi?

 
Huku tukihimizwa kuchukua tahadhari hali inazidi kuwa tofauti huku vijiji vya hawa nshomile, yani wametoka Dar kwa vingi sasa wamefika Vijijini huku ni kushinda kwenye vibaa huku wakifuatwa na wenyeji wao ili wakagongee pombe yaani full mikusanyiko hakuna anayeelewa tahadhari yoyote.

Sherehe za misiba ndo znapamba Moto huku pamoja na harusi ndoa Kama kwa yaani wanaotoka Dar ndo wanafadhili haya makusanyiko. Serikali tupieni jicho huku Kiziba
 
Nisalimie MURANGIRA
 
Mmesahau HIV eeh!! Na yale mameno ya top wakati wa tetemeko? Palilieni janga tu
 
Tujitahidi kufuata maelekezo yote tunayopewa na wataalamu, lakini katika yote tumtangulize MUNGU kwani YEYE ndiye mponyaji asiyeshindwa na gonjwa lolote.

Kwa namna ya kipekee nampongeza sana Mheshimiwa Rais wa JMT Dk. JPM kwa kumfanya MUNGU kuwa kimbilio la kwanza la taifa letu la TZ katika kukabiliana na janga la Covid19. Rais wetu amechagua kuanzia pale walipoishia wengine. Tuungane na Rais wetu, kulitaja jina la BWANA atupaye uzima.

MUNGU ataiponya TZ.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…