So unataka MD awe anaprescribe dawa na kudispense dawa?Naona baada ya hili bandiko Famasia na mafundi dawa wanaishia kutukana na kusonya bila kujibu hoja za msingi..
Ungechambua kitalaamu bwana kimasihara ,unataka kushindana na huyo Prof ,mbona andiko lake limekaa poa Sana Tena kiprofeshino.Mteremko wa Addo umefutwaa mnaanza kulia liaa...!! No shortcut vinajaa rudini darasanii kama ambavyo mnasema hatuyajui magonjwa bhasi na nyie Dawa hamzijui vile vileee...
Mkuu Prof Koboko, hongera Sana kwa kuleta mada hii. Kusema kweli, Tanzania siasa hizi zinatuharibu Sana. Sasa, siasa za wafamasia na Maduka ya dawa kwa maana ya Maduka ya dawa muhimu na famasia zinastaajabisha Sana. Walifanya lobbying wakaja na Sheria ya ajabu ya ADDO ambayo kimsingi haina mantiki Wala uhalisia. Imagine Daktari aliyesoma kozi ya pharmacology kwa mwaka mzima, anazuiwa kuuza duka la dawa muhimu ati ili auze, Basi sharti asomee ADDO kwa muda wa wiki sita. Kwamba Wiki sita zinatosha kwa mtu kupata ujuzi wa dawa kuliko ujuzi alioupata kwa kozi ya mwaka mzima( 2 semesters)?WAZIRI UMMY MWALIMU, USIPOTOSHWE NA WAFAMASIA KUHUSU ADDO, MTAANGAMIZA AFYA ZA WATANZANIA.
Na Prof Patrick Koboko(MD,MMED,PhD)
Salaam Mhe Waziri!
Kwanza kabisa nikupe pole na hongera nyingi sana kwa majukumu iliyonayo ya ujenzi wa taifa hususani dhamana kubwa uliyopewa ya kushikilia afya za watanzania. Maana wewe ukitetereka na afya za watanzania zinatetereka.
Mhe Waziri Ummy Mwalimu umekua ni miongoni mwa wanasiasa wanamama wanaofanya kazi kubwa sana na nzuri sana katika kulijenga taifa hili na hii ndiyo maana ulirejeshwa katika katika wizara iliyopo hivi sasa.
Lakini nikushauri Mama yangu kuna watu wanekuzunguka usipokua makini watakuharibia kazi, wanatumia mwanya kwa sababu wewe siyo Mtaaluma katika fani ya Afya. Katika hili swala la ADDO umepotoshwa na msipoangalia mnaenda kuliangamiza taifa, titatolea sababu hapa chini.
ADDO NI MRADI WA NANI?
Mhe waziri, tunashukuru kwamba mmesitisha mpango wa kutoa mafunzo kwa watoa dawa za binadamu ambao hawana taaluma ya famasia almaarufu kama ADDO. Huu ulikua ni mradi ambao ulibuniwa na baadhi ya wachumia tumbo wachache ambao walitaka kujitengenezea namna flani ya kula pesa za watanzania wenye taaluma za afya hasa wauguzi na matabibu kwa madai kwamba hawana taaluma za famasia(Sijui kuna uhusiano gani hapa). Huu ulikua ni upigaji wa pesa za watanzania tena walitoza pesa nyingi sana kuanzia shilingi 250,000 na kuendelea. Kuondoa ADDO ni kuwandolea ulaji wachumia tumbo hawa ambao hawakua na maslahi kwa taifa.
Maana vyeti vilitolewa kwa rushwa nyingi sana na hata walipewa wasiokua na taaluma za afya ndiyo maana tuliona yanayotokea kwenye baadhi ya maduka, mtu ana cheti cha ADDO lakini taaluma ya Afya hana. Niwe muwazi mradi huu uliratibiwa na baraza la famasia Tanzania, hata leo ukaguzi ukifanyika yatagundulika Madudu mengi sana na ningeomba mamlaka za serikali kama vile PCCB na CAG walichunguze baraza la famasia Tanzania mtajionea mengi.
KATI YA MFAMASIA, NESI NA DAKTARI NANI ATOE DAWA KWA MGONJWA? WAZIRI UMEPOTOSHWA!
1.MFAMASIA KAZI YAKE NI IPI?
Kwa bahati mbaya sana Mhe waziri sijui lengo lako la kusitisha mafunzo ya ADDO ni kudhibiti mianya ya Rushwa au mnalenga kazi hii ifanywe na wafamasia pekee? Kama lengo ni wafamasia watoe dawa kwa wagonjwa basi umepotoshwa vibaya sana mnataka kuangamiza Afya za wananchi.
✓Kazi ya Mfamasia ni kutunza na kuhifadhi dawa,kusambaza maeneo yenye uhitaji pamoja na kutengeneza dawa viwandani na siyo kutoa dawa moja kwa moja kwa mgonjwa . Kwahiyo kazi yake siyo drugs Administration, hii ni kazi ya watu wengine. Mfamasia hajasomea Magonjwa wala wadudu wanaosababisha maradhi, hajasomea dalili za magonjwa. Hivi anapoenda mgonjwa kwenye duka la dawa na hana cheti cha daktari, Mfamasia anajua Diagnosis ya ugonjwa wake? Amesomea dalili? Ni maduka mangapi yanayotoa dawa kwa vyeti vya madaktari nchini? Hivi mnajua kua mnataka kuliangamiza taifa kwa maslahi ya wachache?
2.DAKTARI NA NESI KWENYE UTOAJI WA DAWA
Sihitaji kutoa utetezi katika taaluma hizi kwa sababu mimi ni mwanataaluma pia lakini huu ndio ukweli na Mhe waziri nitoe somo hapa ili ukatae wale waliokupotosha.
✓ Daktari yeye amesomea magonjwa na dalili zake hivyo, mgonjwa anapoumwa tayari anajua anaumwa kitu gani na anajua ampe dawa gani maana dalili za ugonjwa husika anazijua, sasa unaposema Mfamasia akae dukani auze dawa, akija mgonjwa bila cheti atanisaidia nini? Atatambuaje ugonjwa husika na kwa taaluma gani?
✓Nesi hana tofauti sana na daktari maana naye anasomea magonjwa na dalili zake pamoja kutoa dawa moja kwa moja kwa mgonjwa na yeye amejikita zaidi katika kumwangalia mgonjwa anapopata matibu. Kiutaratibu Nesi ndiye anayeenda na cheti cha daktari katika dirisha la dawa na atapewa dawa na Mfamasia kisha ataenda kumpa mgonjwa dawa maana anajua anatoa dawa ipi kwa mgonjwa na kwa ugonjwa upi. Ndiye anayepokea maagizo ya daktari kisha aende kwa mhifadhi dawa ambaye ni Mfamasia ampatie ili akampe mgonjwa.
Halafu kuna kikundi cha watu wachache wanaanzisha miradi wakaupa jina la ADDO ili manesi na madaktari wasomee kisha wakauze dawa.Mbona mahospitalini manesi na madaktari wanatoa dawa hawasomi ADDO? Utapeli mtupu!
USHAURI: NINI KIFANYIKE KATIKA UTOAJI WA DAWA NCHINI KWENE MADUKA YA DAWA?
1.KWENYE PHARMACY ZA JUMLA NA REJA REJA.
(i)Kwakua maduka haya ni makubwa na yana dawa nyingi, pawepo na Wafamasia ambao kazi zao ni kuhifadhi na kusambaza dawa kwenda kwa wauzaji au watoa dawa na siyo wao kuuza dawa kwa wagonjwa moja kwa moja maana wao hawana taaluma ya magonjwa.
(ii) Kuwepo na nesi au tabibu kwa ajili ya kutoa dawa kwa wagonjwa walioandikiwa kwenye vyeti au wawasikilize na kisha kubaini wanaumwa nini na kisha watoe dawa. Hizi ndizo kazi zao hasa kwenye maduka ya rejareja. Mfamasia hana utaalam wa kubaini ugonjwa, anaweza kuleta matatizo kwa mgonjwa.
(iii) Dawa zisitolewe bila cheti cha daktari katika duka lolote na ukaguzi wa kila mara ufanyike. Maana anaweza kutoa dawa mtu ambaye hana taaluma ya magonjwa ikiwa mgonjwa hana cheti na kuleta madhara makubwa.
2.MADUKA YA DAWA MUHIMU
Kwakua maduka haya mengi yapo sehemu ambazo ziko mbali na huduma za afya, wataalam wenye taaluma za kubaini mgonjwa anaumwa nini kupitia dalili waachwe wauze au watoe dawa. Hawa ndio waliosomea Magonjwa,dalili pamoja na kutibu. Hapa anaweza kukaa daktari au nesi akauza dawa. Kumwambia Mfamasia akae dukani auze dawa wakati hajasomea dalili wala kubaini magonjwa ni kutaka kuleta madhara makubwa kwa wagonjwa.
Kwakua maduka haya hayana dawa nyingi, uhifadhi unaweza kufanywa na daktari au nesi mwenye stoo maana pia wamefundishwa kipengele hicho.
HITIMISHO
Nishsuri tuwe na chombo cha ukaguzi wa maduka ya dawa ambacho kitahusisha wanataaluma wa Famasia,Udaktari na Uuguzi ili ifanye kazi ya kusimamia maduka ya madawa na isifanywe na Barazaa Famasia wala TMDA. Hatutaanza sisi, mataifa ya wenzetu wanafanya hivi na wamefanikiwa sana wala hawana migogoro kama hii ya kwetu.
Baraza la Famasia libakie kazi yake kudhibiti taaluma na siyo kukagua maduka ya dawa.TMDA wanamajukumu makubwa wabakie kukagua dawa zinazoingia nchini na vifaa tiba na kukakua ubora wa madawa viwandani huko zinakotengezwa, kwenye maduka ya dawa kiundwe chombo maalumu kijitegemee.
Prof Patrick Koboko(MD,MMED, PhD in Human anatomy)
Huu mjadala ukiendelea bila kuainisha kazi za mfamasia kwenye sekta ya afya hasa hasa hospitalini ntawaona wote mnajikweza bila sababu ya msingi
Mfamasia atolee maelezo kuhusu majukumu yake hospitalini kulingana na taaluma yake alivyofundishwa chuoni
Na daktari nae aelezee majukumu yake
Kulingana na taaluma yake
profesa kilazaMDs ni incompetent wengi sana yanasoma theory tu hayana kitu yamejaa wivu tu, Hio cannibalism waikubali haikwepeki MDs kaeni huko mahospitalini
profesa mbona unatoa mabokoWewe naye ni fake tu, daktari asijue namna dawa inayotolewa wakati ndiye anayejua ugonjwa na wadudu wake na kutoa Orders kwa Mfamasia atoe dawa leo unasemaje hajui?
Acha Ulongo, hakuna sehemu Pharmacist anakosomea kutibu. Uko sahihi kuwa as Drs, wanafundishwa Basic pharmacology hata hivyo, kuuza dawa mtu hahitaji knowledge ya kiwango Cha Pharmacist ndio maana mkaona wiki sita za ADDO zinatosha kum equip mtu na basic knowledge ya kuuza dawa.Kwa kifupi umepost ujinga, na nadhani inabid uchunguzwe tujue kama kweli wewe ni daktari au una matatizo ya akili. Unajua maana ya Pharmacy? Unajua aina za wafamasia? Unajua kazi za wafamasia?
Unajua kwa nini ADDO ilianzishwa?
Lengo kuu lilikuwa ni kutatua changamoto ya upatikanaji wa dawa ambao wahusika wakuu wa kuzitoa ni wataalamu wa dawa walikuwa hawajitoshelezi kwa wakati huo.
Wataalamu waliopo kwa sasa wanatosha kuihudumia jamii katika nafasi hiyo. Ikumbukwe madaktari mnasoma "basic pharmacology", lakini wataalamu wa dawa wanaenda mbali zaidi ya kile mnachosoma nyie. Kwa hiyo siku zote mfamasia NDIYE MTAALAMU WA DAWA, ANAIJUA DAWA NJE NA NDANI, ANAJUA KWA NINI MGONJWA APEWE DAWA HUSIKA, APEWE KIWANGO GANI NA KWA MUDA GANI, AMESOMA MAGONJWA, DALILI ZAKE NA JINSI YA KUTIBU KAMA WEWE... LAKINI KUHUSIANA NA DAWA YEYE NDIYE MBOBEZI ZAIDI.
Maduka ya dawa yameanzishwa mtaani ni mengi na yamekaa kibiashara, wigo wa ADDO unazidi kupunguza ufanisi wa matumizi sahihi ya dawa.
Kwa kifupi ADDO inapaswa kuondolewa, wataalamu wa dawa waliopo kwa sasa wanatosha kabisa kuihudumia jamii.
Mkuu Prof Koboko, hongera Sana kwa kuleta mada hii. Kusema kweli, Tanzania siasa hizi zinatuharibu Sana. Sasa, siasa za wafamasia na Maduka ya dawa kwa maana ya Maduka ya dawa muhimu na famasia zinastaajabisha Sana. Walifanya lobbying wakaja na Sheria ya ajabu ya ADDO ambayo kimsingi haina mantiki Wala uhalisia. Imagine Daktari aliyesoma kozi ya pharmacology kwa mwaka mzima, anazuiwa kuuza duka la dawa muhimu ati ili auze, Basi sharti asomee ADDO kwa muda wa wiki sita. Kwamba Wiki sita zinatosha kwa mtu kupata ujuzi wa dawa kuliko ujuzi alioupata kwa kozi ya mwaka mzima( 2 semesters)?
Na ajabu zaidi ni kuwa dawa hizo hizo anazozuiwa Daktari kuuza, Sheria inasema zisitolewe bila kibali( prescription form) Cha Daktari.
Kwa faida ya wasio jua, dawa hizi za binadamu ziko za Aina mbili.
1. Over the counter drugs; hizi ni dawa ambazo mgonjwa anaweza kutumia bila kibali Cha Daktari. mf Panadol, Magnesium n.k. Na dawa hizi huweza kutolewa kwa ridhaa ya mtu yeyote mwenye uelewa sahihi au kulingana na matakwa ya mgonjwa.
2. Prescribed drugs; Hizi ni dawa ambazo haziruhusiwi kutolewa bila kibali (prescription form) Cha Daktari. Na hizi ndizo dawa zilizo nyingi.
Chakushangaza, huku kwetu, Daktari huyu anayeidhinisha dawa flani itolewe, haruhusiwi kumiliki/ kuuza duka la dawa ati mpaka awe na cheti Cha ADDO😅.
Nchi ya ajabu Sana hii.
Acha Ulongo, hakuna sehemu Pharmacist anakosomea kutibu. Uko sahihi kuwa as Drs, wanafundishwa Basic pharmacology hata hivyo, kuuza dawa mtu hahitaji knowledge ya kiwango Cha Pharmacist ndio maana mkaona wiki sita za ADDO zinatosha kum equip mtu na basic knowledge ya kuuza dawa.
Pili, sio kweli kuwa pharmacist wanasomea kutibu. Tunaposema kutibu(Management of disease) tuna maana ya investigations( Vipimo) na treatment ( ambayo inaweza kuwa Dawa, Upasuaji au ushauri mahsusi), hapo mfamasia anaingia kwenye kipengele kimoja tuu Cha Dawa.
Tatu, ufahamu wa wafamasia kwenye magonjwa ni mdogo Sana hauwezi kulingana na robo ya ufahamu wa Daktari. Mna basic knowledge ya Anatomy, physiology, pathophysiology of different disease conditions, Pathology even Microbiology ukilinganisha na huyu Dr.
Ndio sababu Dr anabaki kuwa Kiongozi kwenye timu ya kutoa huduma.
Nadhani ni kwasababu ya uchache wa wafamasia.Prop yupo sahihi kwa walofanya kazi hospitali kazi nyingi za utoaji dawa zinafanywa na manesi baada ya kukotoa mahitaji yalioagizwa na madaktari,na kwenda kuchukua famasi au stoo waliko wafamasia na manesi wanao tunza stoo.
Shida ni njaa madaktari wengi wamepishana na pesa..hivyo wakiona kada flani inapiga pesa wanakimbilia kujibanza hapo.Shida sanaaa hilo suala lililtea vitaa kali Mnoo.. Watu nyuzi walikuwa wanabeba sijui hizi Controlled ndo usiseme mtu anataka Akija achukue morphine anavyotakaa.. Fentanyl ndo usisemee sasa ukiwawekea utaratibu Vitaa inaanzaaa!..!! Kuna shidaa sanaa...
Tatizo unazungumza kutoka na unachokiona hapa tanzania angalia Nje1.Nesi anagawa dawa kulingana na prescriptions za daktari.
2.Mfamasia anaweza kugawa dawa kwenye hospitali kubwa,ambako advanced knowledge inahitajika.
NB: Tofautisha kugawa na kutoa dawa.
Tanzania degree ya pharmacy inasomwa miaka 4 na degree ya udaktari ni miaka 5. Tuache kuandika bila kufanya utafiti japo kidogo wa kile tunachoandika! Acha upotoshaji!huu ndio ukweli. anashindwa kuelewa ni kwanini mfamasia anasoma miaka 3 degree, na daktari anasoma miaka 7 degree? hii yoote ni kutaka kuwabana manesi ambao siku zote maisha yao ni magumu, wasiwe na nafasi ya kutoa dawa. manesi huwa wanafundishwa namna ya kutoa dawa na kusoma nini daktari amemaanisha, mfamasia icho kitu naamini anasomea pia. wafamasia tunao wangapi? hadi tuwasambaze vijijini? au mnataka dawa mpate tu huku mijini, wa kijijini wakiugua watafute nauli waje mjini kununua dawa?
Fanya utafiti kuhusu course content ya pharmacy ya Tanzania kabla hujaandika kuhusu pharmacists na kushusha thamani ya taaluma ya pharmacy.Wewe bwana mimi ni Mtanzania ninayeishi South Africa, nimesajiliwa huku ingawa nafundisha madaktari and soon nitaanza kufundisha huko na pia Tanzania namiliki hospitali. Wanaonijua wapo humu humu hawaongei.
Shut up!!
Kwanza kabisa pamoja kubeza elimu yangu na kunitukana sana, nikiri kusema tu kwamba Wafamasia nchini Tanzania ni MZIGO KWA TAIFA.
Sijajua wanaobisha humu ni wafamasia kweli au wengine ni Mafundi sanifu wa dawa na Dispensers ambao kimsingi mjadala huu is beyond their capacities.
NISIKIKIZENI KWA UFUPI PENFINGINE HAMSOMI ANDIKO LANGU LOTE.
Nimesema hivi.......
1.Pamoja na kwamba wafamasia wanasoma anatomy,microbiology, Physiology nk, hivi ni basic knowledge pale wanapotakiwa kusoma therapeutics, mechanisms of actins za dawa kwa wadudu mwilini. Hii siyo knowledge ya kumfanya Mfamasia ajue mgonjwa anaumwa nini, yeye siyo daktari anayeweza kufanya Diagnosis.
2.Nimesema kwa nchi za Wenzetu hata hapa SA 80% of pharmacists wako viwandani kutengeneza dawa na wengine kwenye Godowns za kuhifadhia dawa and rest of them 20% wako mahospitali kusaidiana na madaktari kwenye kufadhi na kutoa dawa. Kwakua Tanzania hatuna viwanda vya vya kutosha vya kutengeneza, Wafamasia wengi hawana kazi wapo kwa ajili ya kuuza vyeti vyao kwa wale wanaotaka kufungua madawa, hata hizi ADDO ni kwa sababu wengi hawana kazi za kufanya wanatafuta kupiga tu pesa. Wanapoona nesi au daktari ana kufika cha dawa basi wanachanganyikiwa na kupanic wanaona kama wanaporwa ulaji wao.
3.Nimesema kua kazi ya Daktari ni kusoma magonjwa na kuyabaini, anasoma Pathophysiology jinsi ugonjwa unavyoingia na kuenea mwilini kwa dalili pamoja na kutibu either kwa dawa au Upasuaji. Sawa unaposema Mfamasia atoe dawa kwa mgonjwa moja kwa moja bila cheti cha daktari l, amesomea wapi magonjwa na dalili zake? Anatomy and physiology ndio zinawafanya waweze kutibu?
-Mfamasia anaweza hata kuchoma sindano?
-Mfamasia anaweza kupasua hata jipu na anajua baada ya upasuaji ni dawa gani itolewe?
-Nesi yupo zaidi kwenye kutoa dawa na uangalizi wa mgonjwa anayetibiwa.