Waziri Ummy, Usipotoshwe maamuzi yako kuhusu ADDO na wafamasia mtawaumiza Watanzania

Waziri Ummy, Usipotoshwe maamuzi yako kuhusu ADDO na wafamasia mtawaumiza Watanzania

Naona baada ya hili bandiko Famasia na mafundi dawa wanaishia kutukana na kusonya bila kujibu hoja za msingi

Naendelea kukazia, Ikiwa kazi zao ni kutengeneza dawa na kemikali zingine kuzihifadhi na kuzisambaza je hii mandatory ya kutoa dawa kwa nini watu wanaohusika na wagonjwa wasizifanye?

Nawaheshimu wafamasia kweli akianza kukuchambulia paracetamol ilivyo kuanzia umbo,rangi hadi radha wako vizuri, nafikiri wanafaa kuingeneza zaidi kuliko kazi ndogondogo za kuigawa kwa wagonjwa.
 
Mteremko wa Addo umefutwaa mnaanza kulia liaa...!! No shortcut vinajaa rudini darasanii kama ambavyo mnasema hatuyajui magonjwa bhasi na nyie Dawa hamzijui vile vileee...
Ungechambua kitalaamu bwana kimasihara ,unataka kushindana na huyo Prof ,mbona andiko lake limekaa poa Sana Tena kiprofeshino.

Wewe umeandika huku una emotions itakuwa ni ego so umeona inashambuliwa ego.

Ila Nina Imani ume specialize kwa matunda kimasihara. Jinsi ulivyoandika umejiabisha Sana kwa huyu prof.kwanza umeandika Kama mtu anaimba taarabu kimapasho.

Am sorry Kama nitakuwa nimeku attach Ila just my perception Sina shida na wewe personal Bali ulichoandika
 
Ila kiukweli waafamasia wana hela kuliko madaktari. Hata mie ningesoma afya nilipenda Sana famasi ili nije nifungue duka la dawa aka famasi. Hata hapa napambana ili niifungue iyo famasi.

Na nilikataa kusomea udaktari Mana Nina utu Sana halafu napenda pesa kuliko unavyoweza kuwaza. Mie kutomtibu mtu eti Hana hela ni ngumu Sana so nitachukiwa na wenzangu
 
WAZIRI UMMY MWALIMU, USIPOTOSHWE NA WAFAMASIA KUHUSU ADDO, MTAANGAMIZA AFYA ZA WATANZANIA.

Na Prof Patrick Koboko(MD,MMED,PhD)

Salaam Mhe Waziri!

Kwanza kabisa nikupe pole na hongera nyingi sana kwa majukumu iliyonayo ya ujenzi wa taifa hususani dhamana kubwa uliyopewa ya kushikilia afya za watanzania. Maana wewe ukitetereka na afya za watanzania zinatetereka.

Mhe Waziri Ummy Mwalimu umekua ni miongoni mwa wanasiasa wanamama wanaofanya kazi kubwa sana na nzuri sana katika kulijenga taifa hili na hii ndiyo maana ulirejeshwa katika katika wizara iliyopo hivi sasa.

Lakini nikushauri Mama yangu kuna watu wanekuzunguka usipokua makini watakuharibia kazi, wanatumia mwanya kwa sababu wewe siyo Mtaaluma katika fani ya Afya. Katika hili swala la ADDO umepotoshwa na msipoangalia mnaenda kuliangamiza taifa, titatolea sababu hapa chini.

ADDO NI MRADI WA NANI?
Mhe waziri, tunashukuru kwamba mmesitisha mpango wa kutoa mafunzo kwa watoa dawa za binadamu ambao hawana taaluma ya famasia almaarufu kama ADDO. Huu ulikua ni mradi ambao ulibuniwa na baadhi ya wachumia tumbo wachache ambao walitaka kujitengenezea namna flani ya kula pesa za watanzania wenye taaluma za afya hasa wauguzi na matabibu kwa madai kwamba hawana taaluma za famasia(Sijui kuna uhusiano gani hapa). Huu ulikua ni upigaji wa pesa za watanzania tena walitoza pesa nyingi sana kuanzia shilingi 250,000 na kuendelea. Kuondoa ADDO ni kuwandolea ulaji wachumia tumbo hawa ambao hawakua na maslahi kwa taifa.

Maana vyeti vilitolewa kwa rushwa nyingi sana na hata walipewa wasiokua na taaluma za afya ndiyo maana tuliona yanayotokea kwenye baadhi ya maduka, mtu ana cheti cha ADDO lakini taaluma ya Afya hana. Niwe muwazi mradi huu uliratibiwa na baraza la famasia Tanzania, hata leo ukaguzi ukifanyika yatagundulika Madudu mengi sana na ningeomba mamlaka za serikali kama vile PCCB na CAG walichunguze baraza la famasia Tanzania mtajionea mengi.

KATI YA MFAMASIA, NESI NA DAKTARI NANI ATOE DAWA KWA MGONJWA? WAZIRI UMEPOTOSHWA!

1.MFAMASIA KAZI YAKE NI IPI?
Kwa bahati mbaya sana Mhe waziri sijui lengo lako la kusitisha mafunzo ya ADDO ni kudhibiti mianya ya Rushwa au mnalenga kazi hii ifanywe na wafamasia pekee? Kama lengo ni wafamasia watoe dawa kwa wagonjwa basi umepotoshwa vibaya sana mnataka kuangamiza Afya za wananchi.

✓Kazi ya Mfamasia ni kutunza na kuhifadhi dawa,kusambaza maeneo yenye uhitaji pamoja na kutengeneza dawa viwandani na siyo kutoa dawa moja kwa moja kwa mgonjwa . Kwahiyo kazi yake siyo drugs Administration, hii ni kazi ya watu wengine. Mfamasia hajasomea Magonjwa wala wadudu wanaosababisha maradhi, hajasomea dalili za magonjwa. Hivi anapoenda mgonjwa kwenye duka la dawa na hana cheti cha daktari, Mfamasia anajua Diagnosis ya ugonjwa wake? Amesomea dalili? Ni maduka mangapi yanayotoa dawa kwa vyeti vya madaktari nchini? Hivi mnajua kua mnataka kuliangamiza taifa kwa maslahi ya wachache?

2.DAKTARI NA NESI KWENYE UTOAJI WA DAWA
Sihitaji kutoa utetezi katika taaluma hizi kwa sababu mimi ni mwanataaluma pia lakini huu ndio ukweli na Mhe waziri nitoe somo hapa ili ukatae wale waliokupotosha.

✓ Daktari yeye amesomea magonjwa na dalili zake hivyo, mgonjwa anapoumwa tayari anajua anaumwa kitu gani na anajua ampe dawa gani maana dalili za ugonjwa husika anazijua, sasa unaposema Mfamasia akae dukani auze dawa, akija mgonjwa bila cheti atanisaidia nini? Atatambuaje ugonjwa husika na kwa taaluma gani?

✓Nesi hana tofauti sana na daktari maana naye anasomea magonjwa na dalili zake pamoja kutoa dawa moja kwa moja kwa mgonjwa na yeye amejikita zaidi katika kumwangalia mgonjwa anapopata matibu. Kiutaratibu Nesi ndiye anayeenda na cheti cha daktari katika dirisha la dawa na atapewa dawa na Mfamasia kisha ataenda kumpa mgonjwa dawa maana anajua anatoa dawa ipi kwa mgonjwa na kwa ugonjwa upi. Ndiye anayepokea maagizo ya daktari kisha aende kwa mhifadhi dawa ambaye ni Mfamasia ampatie ili akampe mgonjwa.

Halafu kuna kikundi cha watu wachache wanaanzisha miradi wakaupa jina la ADDO ili manesi na madaktari wasomee kisha wakauze dawa.Mbona mahospitalini manesi na madaktari wanatoa dawa hawasomi ADDO? Utapeli mtupu!

USHAURI: NINI KIFANYIKE KATIKA UTOAJI WA DAWA NCHINI KWENE MADUKA YA DAWA?
1.KWENYE PHARMACY ZA JUMLA NA REJA REJA.
(i)Kwakua maduka haya ni makubwa na yana dawa nyingi, pawepo na Wafamasia ambao kazi zao ni kuhifadhi na kusambaza dawa kwenda kwa wauzaji au watoa dawa na siyo wao kuuza dawa kwa wagonjwa moja kwa moja maana wao hawana taaluma ya magonjwa.

(ii) Kuwepo na nesi au tabibu kwa ajili ya kutoa dawa kwa wagonjwa walioandikiwa kwenye vyeti au wawasikilize na kisha kubaini wanaumwa nini na kisha watoe dawa. Hizi ndizo kazi zao hasa kwenye maduka ya rejareja. Mfamasia hana utaalam wa kubaini ugonjwa, anaweza kuleta matatizo kwa mgonjwa.

(iii) Dawa zisitolewe bila cheti cha daktari katika duka lolote na ukaguzi wa kila mara ufanyike. Maana anaweza kutoa dawa mtu ambaye hana taaluma ya magonjwa ikiwa mgonjwa hana cheti na kuleta madhara makubwa.

2.MADUKA YA DAWA MUHIMU
Kwakua maduka haya mengi yapo sehemu ambazo ziko mbali na huduma za afya, wataalam wenye taaluma za kubaini mgonjwa anaumwa nini kupitia dalili waachwe wauze au watoe dawa. Hawa ndio waliosomea Magonjwa,dalili pamoja na kutibu. Hapa anaweza kukaa daktari au nesi akauza dawa. Kumwambia Mfamasia akae dukani auze dawa wakati hajasomea dalili wala kubaini magonjwa ni kutaka kuleta madhara makubwa kwa wagonjwa.

Kwakua maduka haya hayana dawa nyingi, uhifadhi unaweza kufanywa na daktari au nesi mwenye stoo maana pia wamefundishwa kipengele hicho.

HITIMISHO
Nishsuri tuwe na chombo cha ukaguzi wa maduka ya dawa ambacho kitahusisha wanataaluma wa Famasia,Udaktari na Uuguzi ili ifanye kazi ya kusimamia maduka ya madawa na isifanywe na Barazaa Famasia wala TMDA. Hatutaanza sisi, mataifa ya wenzetu wanafanya hivi na wamefanikiwa sana wala hawana migogoro kama hii ya kwetu.

Baraza la Famasia libakie kazi yake kudhibiti taaluma na siyo kukagua maduka ya dawa.TMDA wanamajukumu makubwa wabakie kukagua dawa zinazoingia nchini na vifaa tiba na kukakua ubora wa madawa viwandani huko zinakotengezwa, kwenye maduka ya dawa kiundwe chombo maalumu kijitegemee.

Prof Patrick Koboko(MD,MMED, PhD in Human anatomy)
Mkuu Prof Koboko, hongera Sana kwa kuleta mada hii. Kusema kweli, Tanzania siasa hizi zinatuharibu Sana. Sasa, siasa za wafamasia na Maduka ya dawa kwa maana ya Maduka ya dawa muhimu na famasia zinastaajabisha Sana. Walifanya lobbying wakaja na Sheria ya ajabu ya ADDO ambayo kimsingi haina mantiki Wala uhalisia. Imagine Daktari aliyesoma kozi ya pharmacology kwa mwaka mzima, anazuiwa kuuza duka la dawa muhimu ati ili auze, Basi sharti asomee ADDO kwa muda wa wiki sita. Kwamba Wiki sita zinatosha kwa mtu kupata ujuzi wa dawa kuliko ujuzi alioupata kwa kozi ya mwaka mzima( 2 semesters)?
Na ajabu zaidi ni kuwa dawa hizo hizo anazozuiwa Daktari kuuza, Sheria inasema zisitolewe bila kibali( prescription form) Cha Daktari.
Kwa faida ya wasio jua, dawa hizi za binadamu ziko za Aina mbili.

1. Over the counter drugs; hizi ni dawa ambazo mgonjwa anaweza kutumia bila kibali Cha Daktari. mf Panadol, Magnesium n.k. Na dawa hizi huweza kutolewa kwa ridhaa ya mtu yeyote mwenye uelewa sahihi au kulingana na matakwa ya mgonjwa.

2. Prescribed drugs; Hizi ni dawa ambazo haziruhusiwi kutolewa bila kibali (prescription form) Cha Daktari. Na hizi ndizo dawa zilizo nyingi.

Chakushangaza, huku kwetu, Daktari huyu anayeidhinisha dawa flani itolewe, haruhusiwi kumiliki/ kuuza duka la dawa ati mpaka awe na cheti Cha ADDO😅.
Nchi ya ajabu Sana hii.
 
Huu mjadala ukiendelea bila kuainisha kazi za mfamasia kwenye sekta ya afya hasa hasa hospitalini ntawaona wote mnajikweza bila sababu ya msingi

Mfamasia atolee maelezo kuhusu majukumu yake hospitalini kulingana na taaluma yake alivyofundishwa chuoni

Na daktari nae aelezee majukumu yake
Kulingana na taaluma yake

Well...katika Msingi wa Taaluma..Mfamasia ndiyo anatambua kuanzia dawa inavotengenezwa hadi inavyokuja kutumika kwa mtumiaji wa mwisho(mgonjwa)...kwa mantiki hiyo mchakato mzima hadi kwanini dawa fulani itumike kwenye Tatizo fulani la kiafya basi ni mfamasia anaweza toa maelezo sahihi zaidi ya kitaalam kuliko wataalam wengine wa afya.Hivyo fursa kwa wafamasia zinaanzia kwenye Viwanda vya dawa hadi Kwa watumiaji (hospitali na kwenye jamii)...Sasa hapa tunakuja kuwapata wafamasia ambao wanafanya kazi Viwandani....( Industrial Pharmacists).....wanaofanya kazi Hospitali ( Clinical and hospital Pharmacist)...waofanya kazi kwenye jamii ( Community Pharmacist)......... lakini pia wapo wafamasia wanaofanya kazi kwenye kampuni za Uingizaji na usambazaji wa dawa....bila kusahau wanao fanya kazi kwenye Mamlaka za udhibiti wa Ubora na ufanisi wa Dawa ... ...kulingana na mchanganuo huo majukumu huwa tofauti tofauti na ni sehemu ya taaluma pia !....Turudi Hospital & Community Pharmacy sasa ambako ndio kuna migongano ya ufanyaji kazi....Majukumu ya mfamasia ni haya
1)kuweka Kumbukumbu za dawa
2) Kuanisha mahitaji ya dawa kwa kipindi fulani mwaka au robo mwaka
3)kushirikiana na watu wa manunuzi katika kuagiza na kununua dawa sahihi kulingana na mahitaji ya hospitali/ Community Pharmacy
4) Kutoa dawa na vifaa tiba kwaajili ya kuhudumia wagonjwa hizi kazi utakutana nazo "Store za dawa"
5)"KUSIMAMIA MATUMIZI SAHIHI YA DAWA"" ...Daktari anapo prescribe dawa ...jukumu la kuangalia usahihi wa dawa kulingana na tatizo na dozi sahihi linabaki kwa "mfamasia"....Kifupi kazi ya kudispense ni ya watu wa famasi sio ya Daktari...na hapa ndio tatizo linapokuja Daktari anataka ""aprescribe yeye na kudispense yeye""" sio kazi ngumu lakini sio sehemu ya majukumu yake.
6) kutengeneza dawa hospitali /Community Pharmacy. ( compounding)
7)Kuelimisha watumishi wengine wote wa hospital juu ya matumizi ya dawa.
8)kutoa taarifa kuhusu madhara ya muda mfupi na muda mrefu yatokanayo na matumizi ya dawa....!
9) Kutambua muingiliano wowote wenye athari hasi kati ya dawa na dawa au dawa na chakula.

Kifupi ndio majukumu hayo hasaaa kwenye mazingira ya Hospital na Pharmacy za mitaani.
 
Wewe naye ni fake tu, daktari asijue namna dawa inayotolewa wakati ndiye anayejua ugonjwa na wadudu wake na kutoa Orders kwa Mfamasia atoe dawa leo unasemaje hajui?
profesa mbona unatoa maboko
😂😂😂
 
Kwa kifupi umepost ujinga, na nadhani inabid uchunguzwe tujue kama kweli wewe ni daktari au una matatizo ya akili. Unajua maana ya Pharmacy? Unajua aina za wafamasia? Unajua kazi za wafamasia?
Unajua kwa nini ADDO ilianzishwa?
Lengo kuu lilikuwa ni kutatua changamoto ya upatikanaji wa dawa ambao wahusika wakuu wa kuzitoa ni wataalamu wa dawa walikuwa hawajitoshelezi kwa wakati huo.
Wataalamu waliopo kwa sasa wanatosha kuihudumia jamii katika nafasi hiyo. Ikumbukwe madaktari mnasoma "basic pharmacology", lakini wataalamu wa dawa wanaenda mbali zaidi ya kile mnachosoma nyie. Kwa hiyo siku zote mfamasia NDIYE MTAALAMU WA DAWA, ANAIJUA DAWA NJE NA NDANI, ANAJUA KWA NINI MGONJWA APEWE DAWA HUSIKA, APEWE KIWANGO GANI NA KWA MUDA GANI, AMESOMA MAGONJWA, DALILI ZAKE NA JINSI YA KUTIBU KAMA WEWE... LAKINI KUHUSIANA NA DAWA YEYE NDIYE MBOBEZI ZAIDI.
Maduka ya dawa yameanzishwa mtaani ni mengi na yamekaa kibiashara, wigo wa ADDO unazidi kupunguza ufanisi wa matumizi sahihi ya dawa.
Kwa kifupi ADDO inapaswa kuondolewa, wataalamu wa dawa waliopo kwa sasa wanatosha kabisa kuihudumia jamii.
Acha Ulongo, hakuna sehemu Pharmacist anakosomea kutibu. Uko sahihi kuwa as Drs, wanafundishwa Basic pharmacology hata hivyo, kuuza dawa mtu hahitaji knowledge ya kiwango Cha Pharmacist ndio maana mkaona wiki sita za ADDO zinatosha kum equip mtu na basic knowledge ya kuuza dawa.
Pili, sio kweli kuwa pharmacist wanasomea kutibu. Tunaposema kutibu(Management of disease) tuna maana ya investigations( Vipimo) na treatment ( ambayo inaweza kuwa Dawa, Upasuaji au ushauri mahsusi), hapo mfamasia anaingia kwenye kipengele kimoja tuu Cha Dawa.

Tatu, ufahamu wa wafamasia kwenye magonjwa ni mdogo Sana hauwezi kulingana na robo ya ufahamu wa Daktari. Mna basic knowledge ya Anatomy, physiology, pathophysiology of different disease conditions, Pathology even Microbiology ukilinganisha na huyu Dr.
Ndio sababu Dr anabaki kuwa Kiongozi kwenye timu ya kutoa huduma.
 
Mkuu Prof Koboko, hongera Sana kwa kuleta mada hii. Kusema kweli, Tanzania siasa hizi zinatuharibu Sana. Sasa, siasa za wafamasia na Maduka ya dawa kwa maana ya Maduka ya dawa muhimu na famasia zinastaajabisha Sana. Walifanya lobbying wakaja na Sheria ya ajabu ya ADDO ambayo kimsingi haina mantiki Wala uhalisia. Imagine Daktari aliyesoma kozi ya pharmacology kwa mwaka mzima, anazuiwa kuuza duka la dawa muhimu ati ili auze, Basi sharti asomee ADDO kwa muda wa wiki sita. Kwamba Wiki sita zinatosha kwa mtu kupata ujuzi wa dawa kuliko ujuzi alioupata kwa kozi ya mwaka mzima( 2 semesters)?
Na ajabu zaidi ni kuwa dawa hizo hizo anazozuiwa Daktari kuuza, Sheria inasema zisitolewe bila kibali( prescription form) Cha Daktari.
Kwa faida ya wasio jua, dawa hizi za binadamu ziko za Aina mbili.

1. Over the counter drugs; hizi ni dawa ambazo mgonjwa anaweza kutumia bila kibali Cha Daktari. mf Panadol, Magnesium n.k. Na dawa hizi huweza kutolewa kwa ridhaa ya mtu yeyote mwenye uelewa sahihi au kulingana na matakwa ya mgonjwa.

2. Prescribed drugs; Hizi ni dawa ambazo haziruhusiwi kutolewa bila kibali (prescription form) Cha Daktari. Na hizi ndizo dawa zilizo nyingi.

Chakushangaza, huku kwetu, Daktari huyu anayeidhinisha dawa flani itolewe, haruhusiwi kumiliki/ kuuza duka la dawa ati mpaka awe na cheti Cha ADDO😅.
Nchi ya ajabu Sana hii.

Ungefuatilia lengo la kuanzishwa ADDO lilikuwa nini hasa!! ...Kwanini Daktari hatakiwi maabara wakati amesoma Parasitology??....Daktari au tabibu shughuli yake ni kuorder vipimo vya kufanyikaa ila mambo ya maabara wanabaki nayo lab scientists ...yeye anasubiri majibu.....ukipata jibu namnaa mgawanyo wa majukumu unavokuwa ndio utaelewa ...kuwa daktari akiprescribe .....mambo ya utoaji na usahihi wa dawa kwa mgonjwa wanabaki nayo wafamasia...Daktari akikosea nani wa kutambua kosa kama yeye anataka kuprescribe na kudispense yeye mwenyewe?..
 
Acha Ulongo, hakuna sehemu Pharmacist anakosomea kutibu. Uko sahihi kuwa as Drs, wanafundishwa Basic pharmacology hata hivyo, kuuza dawa mtu hahitaji knowledge ya kiwango Cha Pharmacist ndio maana mkaona wiki sita za ADDO zinatosha kum equip mtu na basic knowledge ya kuuza dawa.
Pili, sio kweli kuwa pharmacist wanasomea kutibu. Tunaposema kutibu(Management of disease) tuna maana ya investigations( Vipimo) na treatment ( ambayo inaweza kuwa Dawa, Upasuaji au ushauri mahsusi), hapo mfamasia anaingia kwenye kipengele kimoja tuu Cha Dawa.

Tatu, ufahamu wa wafamasia kwenye magonjwa ni mdogo Sana hauwezi kulingana na robo ya ufahamu wa Daktari. Mna basic knowledge ya Anatomy, physiology, pathophysiology of different disease conditions, Pathology even Microbiology ukilinganisha na huyu Dr.
Ndio sababu Dr anabaki kuwa Kiongozi kwenye timu ya kutoa huduma.

Itoshe kusema na ufahamu wa daktari kwenye dawa ni mdogo sana sababu ana basic knowledge ya Pharmacology tuu.

ADDO Ilianzishwa kukabiliana na uhaba wa wafamasia Nchini Tanzania na sio kwamba inatambulika Dunia nzima...Sasa wafamasia wamekuwa wengi ....hatuna uhitaji wa Addo tena ndio maana wizara imesitisha sasa...kila mtu afanye majukumu yanayo muhusu kwa usahihi zaidi...tutapunguza pia Vifo na madhara yatokanayo na matumizi yasiyo sahihi sana ya dawa
 
So leave the profession about medicines to pharmacists, they are kings of medicines, nobody else... kila mtu afanye majukumu huku wakishauriana (wafamasia, manesi, madaktari na maabara) thats team work..
My point is mfamasia anaweza kudiagonis, akampima mgonjwa na kumpa dawa lakini HIYO SIO KAZI YAKE, Hivyo ASIIFANYE. DAKTARI HIVYO HIVYO, ATAFANYA YA KWAKE IKIWEMO KUPRESCRIBE DAWA, LAKINI IKIFIKA KUDISPENSE HILO LIPO KWA MTAALAMU WA DAWA
 
Shida sanaaa hilo suala lililtea vitaa kali Mnoo.. Watu nyuzi walikuwa wanabeba sijui hizi Controlled ndo usiseme mtu anataka Akija achukue morphine anavyotakaa.. Fentanyl ndo usisemee sasa ukiwawekea utaratibu Vitaa inaanzaaa!..!! Kuna shidaa sanaa...
Shida ni njaa madaktari wengi wamepishana na pesa..hivyo wakiona kada flani inapiga pesa wanakimbilia kujibanza hapo.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1.Nesi anagawa dawa kulingana na prescriptions za daktari.
2.Mfamasia anaweza kugawa dawa kwenye hospitali kubwa,ambako advanced knowledge inahitajika.

NB: Tofautisha kugawa na kutoa dawa.
Tatizo unazungumza kutoka na unachokiona hapa tanzania angalia Nje
 
Kumbe ndo maana huku kwetu mtu akiwa na duka la dawa huitwa daktari
 
huu ndio ukweli. anashindwa kuelewa ni kwanini mfamasia anasoma miaka 3 degree, na daktari anasoma miaka 7 degree? hii yoote ni kutaka kuwabana manesi ambao siku zote maisha yao ni magumu, wasiwe na nafasi ya kutoa dawa. manesi huwa wanafundishwa namna ya kutoa dawa na kusoma nini daktari amemaanisha, mfamasia icho kitu naamini anasomea pia. wafamasia tunao wangapi? hadi tuwasambaze vijijini? au mnataka dawa mpate tu huku mijini, wa kijijini wakiugua watafute nauli waje mjini kununua dawa?
Tanzania degree ya pharmacy inasomwa miaka 4 na degree ya udaktari ni miaka 5. Tuache kuandika bila kufanya utafiti japo kidogo wa kile tunachoandika! Acha upotoshaji!
 
Wewe bwana mimi ni Mtanzania ninayeishi South Africa, nimesajiliwa huku ingawa nafundisha madaktari and soon nitaanza kufundisha huko na pia Tanzania namiliki hospitali. Wanaonijua wapo humu humu hawaongei.

Shut up!!
Fanya utafiti kuhusu course content ya pharmacy ya Tanzania kabla hujaandika kuhusu pharmacists na kushusha thamani ya taaluma ya pharmacy.
 
Kwanza kabisa pamoja kubeza elimu yangu na kunitukana sana, nikiri kusema tu kwamba Wafamasia nchini Tanzania ni MZIGO KWA TAIFA.
Sijajua wanaobisha humu ni wafamasia kweli au wengine ni Mafundi sanifu wa dawa na Dispensers ambao kimsingi mjadala huu is beyond their capacities.

NISIKIKIZENI KWA UFUPI PENFINGINE HAMSOMI ANDIKO LANGU LOTE.
Nimesema hivi.......

1.Pamoja na kwamba wafamasia wanasoma anatomy,microbiology, Physiology nk, hivi ni basic knowledge pale wanapotakiwa kusoma therapeutics, mechanisms of actins za dawa kwa wadudu mwilini. Hii siyo knowledge ya kumfanya Mfamasia ajue mgonjwa anaumwa nini, yeye siyo daktari anayeweza kufanya Diagnosis.

2.Nimesema kwa nchi za Wenzetu hata hapa SA 80% of pharmacists wako viwandani kutengeneza dawa na wengine kwenye Godowns za kuhifadhia dawa and rest of them 20% wako mahospitali kusaidiana na madaktari kwenye kufadhi na kutoa dawa. Kwakua Tanzania hatuna viwanda vya vya kutosha vya kutengeneza, Wafamasia wengi hawana kazi wapo kwa ajili ya kuuza vyeti vyao kwa wale wanaotaka kufungua madawa, hata hizi ADDO ni kwa sababu wengi hawana kazi za kufanya wanatafuta kupiga tu pesa. Wanapoona nesi au daktari ana kufika cha dawa basi wanachanganyikiwa na kupanic wanaona kama wanaporwa ulaji wao.

3.Nimesema kua kazi ya Daktari ni kusoma magonjwa na kuyabaini, anasoma Pathophysiology jinsi ugonjwa unavyoingia na kuenea mwilini kwa dalili pamoja na kutibu either kwa dawa au Upasuaji. Sawa unaposema Mfamasia atoe dawa kwa mgonjwa moja kwa moja bila cheti cha daktari l, amesomea wapi magonjwa na dalili zake? Anatomy and physiology ndio zinawafanya waweze kutibu?
-Mfamasia anaweza hata kuchoma sindano?
-Mfamasia anaweza kupasua hata jipu na anajua baada ya upasuaji ni dawa gani itolewe?
-Nesi yupo zaidi kwenye kutoa dawa na uangalizi wa mgonjwa anayetibiwa.

Unapotosha sana wewe! Pharmacist anasoma pharmacotherapy akiwa mwaka wa nne, ndani ya hiyo course kuna components za pathophysiology na kabla ya hapo amesoma physiology, pathology, microbiology na biochemistry sasa unaposema hawezi kubaini ugonjwa unapotosha umma ingawa diagnosis sio kazi yake lakini haina maana kwamba ana zero idea.

Besides kuna thousands of over the counter drugs ambazo Pharmacist anaweza kutumia ku manage minor ailments ambazo sio lazima mgonjwa afike kwa MD ili atibiwe.

Na ndio kazi ya community pharmacies kuwa ni primary health facility ili kupunguza mlundikano wa wagonjwa wenye cases ndogo tu ambao wata clog the hospitals.

Pharmacist ana kazi kubwa ya kumlinda mgonjwa from drug errors ambazo clinician anaweza kuwa amefanya, pia kuna issue ya drug interactions ambazo zinaweza kutokea ambapo ni kazi ya Pharmacist ku screen hizo potential interactions kama imetokea clinian ame prescribe dawa zenye interactions na hiyo inatokea in practice.

Tuache dharau kwa taaluma za watu wengine!
 
Back
Top Bottom