Waziri Ummy, Usipotoshwe maamuzi yako kuhusu ADDO na wafamasia mtawaumiza Watanzania

Waziri Ummy, Usipotoshwe maamuzi yako kuhusu ADDO na wafamasia mtawaumiza Watanzania

Nimekuambia wanayojifunza ni basics tu kwa ajili ya therapeutics na sito kubaini magonjwa. Kozi 99% imejikita kwenye utengenezaji na uhifadhi wa dawa. Kujipa kazi ya biashara ya dawa ni Tanzania tuu kutafuta ulaji ila kwa wenzetu haya hayapo.
Acheni uhuni mnawivu mnataka wauze sura za namazenu, nyie mende mmeroga sana sasa imefika mwisho.
 
Hili swala ni kwa maslahi binafsi naona.

Mgawanyo wa majukumu upo wazi kabisa, daktari atamuona mgonjwa, mgonjwa ataenda kuchukua dawa famasi(mfamasia) kisha mgonjwa atapatiwa dawa chini ya usimamizi wa manesi, sasa nyinyi mnataka kazi zote za hospital mfanye nyinyi?

Mbona hamuongelei ultrasound , x rays na lab investigation ? Kwanini huwa mnaoder vipimo hakapime mtu mwingine hamjasomea lab nyinyi semister nzima? Tufanye mzunguke na mgonjwa basi, anza naye chumba cha consultation, nenda ukampime, urudi umwandikie dawa na uende naye diapensing ukampe dawa
 
Usitafute sifa! Huyu mwandishi yuko sahihi kabisa! Siyo kazi ya mfamasia kugawa dawa kwenye maduka na vidirisha. Hiyo ni fact na iko wazi. Mfamasia hawezi kuwa na kazi ya kutoa dawa kwa wagonjwa mitaani, halafu hospitalini hahusiki. Mfamasia hawezi kutoa dawa za vidonge tu, sindano iwe ni kazi ya nesi. Hiyo ni kujichanganya na kutafuta pesa mitaani ikiwa ni hatari kwa wagonjwa.

Wafamasia fanyeni kazi za kuchanganya madawa na kutafuta dawa mpya za magonjwa na kuzitengeneza. Kama hamuwezi kutengeneza dawa, ninyi ni bure kabisa!!!! Wafamasia kutoa dawa ni kudandia kazi isiyowahusu.
Huna unachojua Kuhusu pharmacist
 
Huyu kaandika Kwa kifupi tuu...ila kapitie carriculum ya pharmacist ipoje

Alafu usiende direct kwenye conclusion,Nenda kaangalie

Responsibilities of Pharmacist in Hospital setting......ukijua HUTAKAA UONGEE UJINGA HUU
Huyu ni mchawi wivu umewajaa hawa hawataki ushindani au kupitwa kitu chochote mende hawa
 
Hili swala ni kwa maslahi binafsi naona…. Mgawanyo wa majukumu upo wazi kabisa,,, daktari atamuona mgonjwa, mgonjwa ataenda kuchukua dawa famasi(mfamasia) kisha mgonjwa atapatiwa dawa chini ya usimamizi wa manesi….. sasa nyinyi mnataka kazi zote za hospital mfanye nyinyi? Mbona hamuongelei ultrasound , x rays na lab investigation ? Kwanini huwa mnaoder vipimo hakapime mtu mwingine hamjasomea lab nyinyi semister nzima? Tufanye mzunguke na mgonjwa basi… anza naye chumba cha consultation, nenda ukampime, urudi umwandikie dawa na uende naye diapensing ukampe dawa……
Wana wivu wa kichawi ukoloni wao unaexpire wana hofu ya maisha
 
Kwanza kabisa pamoja kubeza elimu yangu na kunitukana sana, nikiri kusema tu kwamba Wafamasia nchini Tanzania ni MZIGO KWA TAIFA.
Sijajua wanaobisha humu ni wafamasia kweli au wengine ni Mafundi sanifu wa dawa na Dispensers ambao kimsingi mjadala huu is beyond their capacities.

NISIKIKIZENI KWA UFUPI PENFINGINE HAMSOMI ANDIKO LANGU LOTE.
Nimesema hivi.......

1.Pamoja na kwamba wafamasia wanasoma anatomy,microbiology, Physiology nk, hivi ni basic knowledge pale wanapotakiwa kusoma therapeutics, mechanisms of actins za dawa kwa wadudu mwilini. Hii siyo knowledge ya kumfanya Mfamasia ajue mgonjwa anaumwa nini, yeye siyo daktari anayeweza kufanya Diagnosis.

2.Nimesema kwa nchi za Wenzetu hata hapa SA 80% of pharmacists wako viwandani kutengeneza dawa na wengine kwenye Godowns za kuhifadhia dawa and rest of them 20% wako mahospitali kusaidiana na madaktari kwenye kufadhi na kutoa dawa. Kwakua Tanzania hatuna viwanda vya vya kutosha vya kutengeneza, Wafamasia wengi hawana kazi wapo kwa ajili ya kuuza vyeti vyao kwa wale wanaotaka kufungua madawa, hata hizi ADDO ni kwa sababu wengi hawana kazi za kufanya wanatafuta kupiga tu pesa. Wanapoona nesi au daktari ana kufika cha dawa basi wanachanganyikiwa na kupanic wanaona kama wanaporwa ulaji wao.

3.Nimesema kua kazi ya Daktari ni kusoma magonjwa na kuyabaini, anasoma Pathophysiology jinsi ugonjwa unavyoingia na kuenea mwilini kwa dalili pamoja na kutibu either kwa dawa au Upasuaji. Sawa unaposema Mfamasia atoe dawa kwa mgonjwa moja kwa moja bila cheti cha daktari l, amesomea wapi magonjwa na dalili zake? Anatomy and physiology ndio zinawafanya waweze kutibu?
-Mfamasia anaweza hata kuchoma sindano?
-Mfamasia anaweza kupasua hata jipu na anajua baada ya upasuaji ni dawa gani itolewe?
-Nesi yupo zaidi kwenye kutoa dawa na uangalizi wa mgonjwa anayetibiwa.
Unajua kwamba pharmacist anasoma CLINICAL PHARMACY......

Nakuomba nenda kaangalie contents ya hii kozi pharmacist almost anasoma for 4 semister
 
Huyu pimbi hana adabu kaandika utumbo mtupu mbona anawivu sana na wafamasia huyu kibwengo, asilete uchawi ana akili za kikuda kidwanzi mtopolo. MD wanachuki, dharau na wivu kwa wafamasia. Ummy wakazie hawa vibwetere uchwara songa mbele wape nafasi wafamasia watumike ipasavyo
Hiki ndicho mnajifunza zaid katika semester zenu
 
Kwa kiwango hiki cha professional rivalry mitandaoni huko mahospitalini sijui hali ikoje; sector ambayo bila ya interprofessional working mafanikio hayawezakani.

Hiyo wizara inabidi apewe mtaalamu wa management ya afya ambae ni qualified MD.

Kwa kusoma madaa inaonekana ata hao pharmacists awaelewi kazi ya MD, yaani pharmacists atoe dawa kama ni ivyo vipimo vya mgonjwa vingekuwa vinapelekwa kwao.

Majigambo yasiyo na kichwa wala miguu; ni daktari tu mwenye mamlaka ya kuandika dawa. Pharmacists kama ana wasi wasi na prescription kutokana na condition ya mgonjwa anaweza kuomba verification kama anadhani sio sahihi ata kwa Dr mwingine lakini hana mamlaka ya kubadili dawa kwa maamuzi yake.

Afya ni team working na wataalamu wote wanatakiwa kuwa on the same mission; lakini kwa hii professional rivaly ya hii mada sijui itakuwaje tukiumwa tusio na ndugu wafanyakazi mahospitalini ni mungu tu ndio atakuwa mlinzi wetu.
 
Hujamuelewa Pro. Koboko.
Yeye yupo Sahihi,

Tabibu ikiwa yeye ndiye anafanya Diagnosis Kwa magonjwa, kisha baada ya majibu kutoka maabara anamuandikia Dawa, iweje azuiewe kuuza Duka la dawa au kuwa na Famasi?

Tabibu amesoma kozi ya Pharmacology iweje mpaka apewe kozi nyingine ya ADDO Ndipo aruhusiwe kuuza kwenye Duka la Dawa au Famasi?

Unajua MD Kwa sehemu kubwa anaweza kufanya kazi ya Mfamasia lakini mfamasia hawezi kufanya kazi za MD?
Hivi kwanini watu wengi mnadhani pharmacy ni pharmacology tu. Huwezi kujitapa unajua dawa kwa kusoma pharmacology tu.
 
Kwanza kabisa pamoja kubeza elimu yangu na kunitukana sana, nikiri kusema tu kwamba Wafamasia nchini Tanzania ni MZIGO KWA TAIFA.
Sijajua wanaobisha humu ni wafamasia kweli au wengine ni Mafundi sanifu wa dawa na Dispensers ambao kimsingi mjadala huu is beyond their capacities.

NISIKIKIZENI KWA UFUPI PENFINGINE HAMSOMI ANDIKO LANGU LOTE.
Nimesema hivi.......

1.Pamoja na kwamba wafamasia wanasoma anatomy,microbiology, Physiology nk, hivi ni basic knowledge pale wanapotakiwa kusoma therapeutics, mechanisms of actins za dawa kwa wadudu mwilini. Hii siyo knowledge ya kumfanya Mfamasia ajue mgonjwa anaumwa nini, yeye siyo daktari anayeweza kufanya Diagnosis.

2.Nimesema kwa nchi za Wenzetu hata hapa SA 80% of pharmacists wako viwandani kutengeneza dawa na wengine kwenye Godowns za kuhifadhia dawa and rest of them 20% wako mahospitali kusaidiana na madaktari kwenye kufadhi na kutoa dawa. Kwakua Tanzania hatuna viwanda vya vya kutosha vya kutengeneza, Wafamasia wengi hawana kazi wapo kwa ajili ya kuuza vyeti vyao kwa wale wanaotaka kufungua madawa, hata hizi ADDO ni kwa sababu wengi hawana kazi za kufanya wanatafuta kupiga tu pesa. Wanapoona nesi au daktari ana kufika cha dawa basi wanachanganyikiwa na kupanic wanaona kama wanaporwa ulaji wao.

3.Nimesema kua kazi ya Daktari ni kusoma magonjwa na kuyabaini, anasoma Pathophysiology jinsi ugonjwa unavyoingia na kuenea mwilini kwa dalili pamoja na kutibu either kwa dawa au Upasuaji. Sawa unaposema Mfamasia atoe dawa kwa mgonjwa moja kwa moja bila cheti cha daktari l, amesomea wapi magonjwa na dalili zake? Anatomy and physiology ndio zinawafanya waweze kutibu?
-Mfamasia anaweza hata kuchoma sindano?
-Mfamasia anaweza kupasua hata jipu na anajua baada ya upasuaji ni dawa gani itolewe?
-Nesi yupo zaidi kwenye kutoa dawa na uangalizi wa mgonjwa anayetibiwa.
Kwamba mtu mwenye malaria kwa dalili zake inahitaji Degree kujua na kuwa huyu ana malaria? Mtu anakuja na flu unataka aende Laboratory kupimwa kama ana mafua?

Physical examination ni suala ambalo anaweza kufanya kila mtuu yani usijione special kumuandikia Carbimazole mtu mwenye Goitre labda uniambie Suala la oparations ila sio Kuandika mtu afanyiwe vipimo flani ili kuconfirm Ugonjwa wake then Ujione special.

Dr hajui mtu anaumwa nini ila anajua dalili na Maabara ndio wanathibitisha mtu anaumwaa nini sasa ukiona umeweza kujua anaumwa nini mfamasia hashindwi kujua.. Kingine kuchoma sindano jambo dogo sana kijanaa yani hata teja anajichomaaa..
 
Kuna MD mstaafu alifungua duka la dawa akawa anauza yeye,walipokuja hawa jamaa wa Baraza la pharmacy wakamfungia eti hana cheti cha ADDO,sasa nikajiuliza huyu si ndio alikuwa anaandikia watu dawa hospitalini?Leo huko kwenye ADDO kuna kupi kipya ambacho hajui?

Dokta akaamua kugeuza duka la dawa ikawa baa tu,kaachana hio biashara.

Kila kitu kina sheria na miongozo yake, alifanya vema kufanya bar.”
 
Wewe naye ni fake tu, daktari asijue namna dawa inayotolewa wakati ndiye anayejua ugonjwa na wadudu wake na kutoa Orders kwa Mfamasia atoe dawa leo unasemaje hajui?
Kwa hiyo mtu aliyesoma pharmacy kama degree, unamlinganisha na mtu aliyesoma somo la basic pharmacoloy kwenye uelewa wao kuhusu taaluma ya madawa, you are not serious.....
 
Kwamba mtu mwenye malaria kwa dalili zake inahitaji Degree kujua na kuwa huyu ana malaria??? Mtu anakuja na flu unataka aende Laboratory kupimwa kama ana mafua??? Physical examination ni suala ambalo anaweza kufanya kila mtuu yani usijione special kumuandikia Carbimazole mtu mwenye Goitre labda uniambie Suala la oparations ila sio Kuandika mtu afanyiwe vipimo flani ili kuconfirm Ugonjwa wake then Ujione special... Dr hajui mtu anaumwa nini ila anajua dalili na Maabara ndio wanathibitisha mtu anaumwaa nini sasa ukiona umeweza kujua anaumwa nini mfamasia hashindwi kujua.. Kingine kuchoma sindano jambo dogo sana kijanaa yani hata teja anajichomaaa..
Narudia tena ingawa sijui level ya elimu yako. Si kazi ya Mfamasia kutibu mgonjwa. Mfamasia amesomea kutengeneza,kutunza, kuhifadhi na kusambaza dawa.

Kuchoma sindano ni somo kabisa na ni pana. Kusoma Pathophysiology ni somo na nibpana. History taking ina utaratibu wake. Physical examination ina utaratibu wake mpaka Systemic Examination, huwezi kutoa dawa tu mpaka hayo uyajue.

Acheni kujipa vyeo kwa kujiita madaktari, ninyi ndio mnaoua wagonjwa. Hii ni taaluma ya watu!!
 
Kwa hiyo mtu aliyesoma pharmacy kama degree, unamlinganisha na mtu aliyesoma somo la basic pharmacoloy kwenye uelewa wao kuhusu taaluma ya madawa, you are not serious.....
Hakuna anayekataa kua Mfamasia amesomea dawa. Daktari amesomea Magonjwa na namna ya kuyatibu. Mfamasia yeye akae dirishani asubirie cheti cha daktari.
 
Huu ni utaratibu wa dunia, Internal Standards, international structures. Dactarin ni Administrator wa Clinical setting yeyote ile. Huu si utaratibu wa Tz ni wa kidunia! Ukienda wilayani utakutana na DMO, Mkoani RMO, Na mahospitalini DGs wote na Incharges ni madaktari.

Sasa kwanini wengine wanajitutumua kutaka kujifananisha na vitu visivyowahusu?
 
Leave the drug to the pharmacist...!! Sasa mtu anataka Dr akakae pharmacy kisa tu amesoma pharmacology semister 2...[emoji28][emoji28] sisi tunasoma mpaka Infusion rate...incase kuna toxicity what to do kucalculate dose sahihi incase lower dose inahitajika than available dose.. Leo mtoto ana haeart failure anaandikiwa digoxin 0.0625mg lakini kuna kidonge cha 0.5mg hapo Dr kacalculate tu ila sasa unapataje hiyo dawa digoxin 0.0625mg??? Hapo ndo tunarudi kwenye suala la why mfamasia ni muhimu... Mahospitalini siku hizi Polypharmacy imejaa mtu anamanage PUD na Malaria mgonjwa anaandikiwa dawa karibu 7 hukoo mfamasi ukiwa kilazaa utataoa tu dawa hapo tunasema mfamasia kazi yake sio kutoa Dawaaa tu mfamasia ana majukumu mengi yahusuyo dawa mabapo hakuna namna Dr anaweza yatekelezaa... Management ya magonjwa mengi ni changamoto na wagonjwa hawaponi japo wanatumia pesa nyingi kununua madawa sababu Dr anajiona anajua kila kitu. Mgonjwa anaweza kuja famasi na prescription ina list ya dawa karibu 7 au unakuta ni Mtoto ila Dr dawa alizomuandikia unabaki kushangaaa.. Haya yote hayawezi kukoma kama dr anadhani anajua dawa vizuri kuliko mfamasia
Mkuu rikiboy mjadala ni mrefu lakini sijaona aliyeainisha kazi ya mfamasia kwenye sekta hii kulingana na alivyosomea chuoni
Embu weka wazi kazi zenu wafamasia kwenye sekta ya afya kabla mjadala haujaendelea
Mf:daktari akishaandika prescription ni nini role ya mfamasia baada ya hapo

Mtazunguka sana lakini bila kuweka wazi kazi za mfamasia mjadala hauwezi kuwa na maana yoyote(ni batili)

Na mkishaweka hizo kazi hapo mseme ni nini daktari hawezi kufanya na anachoweza kukifanya
 
WAZIRI UMMY MWALIMU, USIPOTOSHWE NA WAFAMASIA KUHUSU ADDO, MTAANGAMIZA AFYA ZA WATANZANIA.

Na Prof Patrick Koboko(MD,MMED,PhD)

Salaam Mhe Waziri!

Kwanza kabisa nikupe pole na hongera nyingi sana kwa majukumu iliyonayo ya ujenzi wa taifa hususani dhamana kubwa uliyopewa ya kushikilia afya za watanzania. Maana wewe ukitetereka na afya za watanzania zinatetereka.

Mhe Waziri Ummy Mwalimu umekua ni miongoni mwa wanasiasa wanamama wanaofanya kazi kubwa sana na nzuri sana katika kulijenga taifa hili na hii ndiyo maana ulirejeshwa katika katika wizara iliyopo hivi sasa.

Lakini nikushauri Mama yangu kuna watu wanekuzunguka usipokua makini watakuharibia kazi, wanatumia mwanya kwa sababu wewe siyo Mtaaluma katika fani ya Afya. Katika hili swala la ADDO umepotoshwa na msipoangalia mnaenda kuliangamiza taifa, titatolea sababu hapa chini.

ADDO NI MRADI WA NANI?
Mhe waziri, tunashukuru kwamba mmesitisha mpango wa kutoa mafunzo kwa watoa dawa za binadamu ambao hawana taaluma ya famasia almaarufu kama ADDO. Huu ulikua ni mradi ambao ulibuniwa na baadhi ya wachumia tumbo wachache ambao walitaka kujitengenezea namna flani ya kula pesa za watanzania wenye taaluma za afya hasa wauguzi na matabibu kwa madai kwamba hawana taaluma za famasia(Sijui kuna uhusiano gani hapa). Huu ulikua ni upigaji wa pesa za watanzania tena walitoza pesa nyingi sana kuanzia shilingi 250,000 na kuendelea. Kuondoa ADDO ni kuwandolea ulaji wachumia tumbo hawa ambao hawakua na maslahi kwa taifa.

Maana vyeti vilitolewa kwa rushwa nyingi sana na hata walipewa wasiokua na taaluma za afya ndiyo maana tuliona yanayotokea kwenye baadhi ya maduka, mtu ana cheti cha ADDO lakini taaluma ya Afya hana. Niwe muwazi mradi huu uliratibiwa na baraza la famasia Tanzania, hata leo ukaguzi ukifanyika yatagundulika Madudu mengi sana na ningeomba mamlaka za serikali kama vile PCCB na CAG walichunguze baraza la famasia Tanzania mtajionea mengi.

KATI YA MFAMASIA, NESI NA DAKTARI NANI ATOE DAWA KWA MGONJWA? WAZIRI UMEPOTOSHWA!

1.MFAMASIA KAZI YAKE NI IPI?
Kwa bahati mbaya sana Mhe waziri sijui lengo lako la kusitisha mafunzo ya ADDO ni kudhibiti mianya ya Rushwa au mnalenga kazi hii ifanywe na wafamasia pekee? Kama lengo ni wafamasia watoe dawa kwa wagonjwa basi umepotoshwa vibaya sana mnataka kuangamiza Afya za wananchi.

✓Kazi ya Mfamasia ni kutunza na kuhifadhi dawa,kusambaza maeneo yenye uhitaji pamoja na kutengeneza dawa viwandani na siyo kutoa dawa moja kwa moja kwa mgonjwa . Kwahiyo kazi yake siyo drugs Administration, hii ni kazi ya watu wengine. Mfamasia hajasomea Magonjwa wala wadudu wanaosababisha maradhi, hajasomea dalili za magonjwa. Hivi anapoenda mgonjwa kwenye duka la dawa na hana cheti cha daktari, Mfamasia anajua Diagnosis ya ugonjwa wake? Amesomea dalili? Ni maduka mangapi yanayotoa dawa kwa vyeti vya madaktari nchini? Hivi mnajua kua mnataka kuliangamiza taifa kwa maslahi ya wachache?

2.DAKTARI NA NESI KWENYE UTOAJI WA DAWA
Sihitaji kutoa utetezi katika taaluma hizi kwa sababu mimi ni mwanataaluma pia lakini huu ndio ukweli na Mhe waziri nitoe somo hapa ili ukatae wale waliokupotosha.

✓ Daktari yeye amesomea magonjwa na dalili zake hivyo, mgonjwa anapoumwa tayari anajua anaumwa kitu gani na anajua ampe dawa gani maana dalili za ugonjwa husika anazijua, sasa unaposema Mfamasia akae dukani auze dawa, akija mgonjwa bila cheti atanisaidia nini? Atatambuaje ugonjwa husika na kwa taaluma gani?

✓Nesi hana tofauti sana na daktari maana naye anasomea magonjwa na dalili zake pamoja kutoa dawa moja kwa moja kwa mgonjwa na yeye amejikita zaidi katika kumwangalia mgonjwa anapopata matibu. Kiutaratibu Nesi ndiye anayeenda na cheti cha daktari katika dirisha la dawa na atapewa dawa na Mfamasia kisha ataenda kumpa mgonjwa dawa maana anajua anatoa dawa ipi kwa mgonjwa na kwa ugonjwa upi. Ndiye anayepokea maagizo ya daktari kisha aende kwa mhifadhi dawa ambaye ni Mfamasia ampatie ili akampe mgonjwa.

Halafu kuna kikundi cha watu wachache wanaanzisha miradi wakaupa jina la ADDO ili manesi na madaktari wasomee kisha wakauze dawa.Mbona mahospitalini manesi na madaktari wanatoa dawa hawasomi ADDO? Utapeli mtupu!

USHAURI: NINI KIFANYIKE KATIKA UTOAJI WA DAWA NCHINI KWENE MADUKA YA DAWA?
1.KWENYE PHARMACY ZA JUMLA NA REJA REJA.
(i)Kwakua maduka haya ni makubwa na yana dawa nyingi, pawepo na Wafamasia ambao kazi zao ni kuhifadhi na kusambaza dawa kwenda kwa wauzaji au watoa dawa na siyo wao kuuza dawa kwa wagonjwa moja kwa moja maana wao hawana taaluma ya magonjwa.

(ii) Kuwepo na nesi au tabibu kwa ajili ya kutoa dawa kwa wagonjwa walioandikiwa kwenye vyeti au wawasikilize na kisha kubaini wanaumwa nini na kisha watoe dawa. Hizi ndizo kazi zao hasa kwenye maduka ya rejareja. Mfamasia hana utaalam wa kubaini ugonjwa, anaweza kuleta matatizo kwa mgonjwa.

(iii) Dawa zisitolewe bila cheti cha daktari katika duka lolote na ukaguzi wa kila mara ufanyike. Maana anaweza kutoa dawa mtu ambaye hana taaluma ya magonjwa ikiwa mgonjwa hana cheti na kuleta madhara makubwa.

2.MADUKA YA DAWA MUHIMU
Kwakua maduka haya mengi yapo sehemu ambazo ziko mbali na huduma za afya, wataalam wenye taaluma za kubaini mgonjwa anaumwa nini kupitia dalili waachwe wauze au watoe dawa. Hawa ndio waliosomea Magonjwa,dalili pamoja na kutibu. Hapa anaweza kukaa daktari au nesi akauza dawa. Kumwambia Mfamasia akae dukani auze dawa wakati hajasomea dalili wala kubaini magonjwa ni kutaka kuleta madhara makubwa kwa wagonjwa.

Kwakua maduka haya hayana dawa nyingi, uhifadhi unaweza kufanywa na daktari au nesi mwenye stoo maana pia wamefundishwa kipengele hicho.

HITIMISHO
Nishsuri tuwe na chombo cha ukaguzi wa maduka ya dawa ambacho kitahusisha wanataaluma wa Famasia,Udaktari na Uuguzi ili ifanye kazi ya kusimamia maduka ya madawa na isifanywe na Barazaa Famasia wala TMDA. Hatutaanza sisi, mataifa ya wenzetu wanafanya hivi na wamefanikiwa sana wala hawana migogoro kama hii ya kwetu.

Baraza la Famasia libakie kazi yake kudhibiti taaluma na siyo kukagua maduka ya dawa.TMDA wanamajukumu makubwa wabakie kukagua dawa zinazoingia nchini na vifaa tiba na kukakua ubora wa madawa viwandani huko zinakotengezwa, kwenye maduka ya dawa kiundwe chombo maalumu kijitegemee.

Prof Patrick Koboko(MD,MMED, PhD in Human anatomy)
Umenena vyema Prof
 
Back
Top Bottom