Hujamuelewa Pro. Koboko.
Yeye yupo Sahihi,
Tabibu ikiwa yeye ndiye anafanya Diagnosis Kwa magonjwa, kisha baada ya majibu kutoka maabara anamuandikia Dawa, iweje azuiewe kuuza Duka la dawa au kuwa na Famasi?
Tabibu amesoma kozi ya Pharmacology iweje mpaka apewe kozi nyingine ya ADDO Ndipo aruhusiwe kuuza kwenye Duka la Dawa au Famasi?
Unajua MD Kwa sehemu kubwa anaweza kufanya kazi ya Mfamasia lakini mfamasia hawezi kufanya kazi za MD?
Mkuu, duniani kote kuko hivyo hii haipo Tanzania pekee. Huu ni muundo wa kikazi ulivyo popote duniani.
Hili swala la daktari kusoma pharmacology hakuondoi tatizo la muingiliano wa maslahi kwa mtu huyo huyo kufanya biashara bila kuweka maslahi ya mgonjwa mbele. Daktari ni binaadam tu kama binaadam wengine.
Hiyo pharmacology unayosema anaisomea, Mfamacia anaisoma maradufu ya huyo daktari, na licha ya hapo mfamacia anaijua dawa zaidi kuliko daktari anavyoifahamu.
Unajua, dawa ni kemikali, kama kemikali zote zilivyo zina mahitaji yake maalum na mwilini zinafanya kazi kama kemikali. Kujua pharmacology hakumfanyi mtu kujua uhusiano wa kemikali hizo na viini vya biologia mwilini.
Unasema "Unajua MD kwa sehemu kubwa anaweza kufanya kazi ya Mfamacia...", kwa mtu kama wewe usiyejua pharmacia anasomea nini ni rahisi kusema hivyo, kwa maana unachoona tu wewe ni kugawa dawa. Hii siyo kazi mahsusi ya mfamacia.
Sasa nieleze, kwa nini unadhani Famacia hawezi kufanya kazi ya kutibu? Si nikiasi tu cha kuongezea ujuzi katika kutambua dalili za ugonjwa, kwani kuna nini cha ziada.
Anatomy, anajifunza, hata kama haendi kupasua cadaver. Physiology anajifunza, Biochemistry anajifunza. Asichosoma kwa undani ni hiyo Pathology.