Nimezitama hizo picha na kugundua haya.
1. Lengo sio kufanya mazoezi, lengo hapo ni kupiga picha. It is a staged photo.
2. Muonekano unaonyesha kuwa sio watu wa mazoezi.
3. Body language inaonyesha hawana ule muunganiko wa kimapenzi baina ya mke na mume au mtu na rafiki yake wa
karibu. Hakuna chemistry baina yao.
4. Mama inaonekana anamburuza mwenzake.
HITIMISHO LANGU.
Uhusiano wao huenda una shida kubwa mahali fulani na hili ni jaribio la kutafuta kufunika shida isije ikaonekana.
USHAURI WANGU KWA DR. GWAJIMA
-Achana kabisa na mtindo wa maisha yako binafsi kuyaleta mbele ya kamera, gharama yake ni kubwa huko mbele ya safari.
-Ukiamua kuwa mwanasiasa basi jifunze kuishi kama mwanasiasa. Usitamani kuishi kama mtu maarufu wakati bado unajifunza kuwa mwanasiasa.