Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, aagiza kusimamishwa kazi kwa Mkurugenzi wa Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii na Meneja udhibiti na ubora

Cha kufanya ilikuwa ni kuchunguza hivyo vifaa vya upimaji badala ya kuwasimamisha kazi wakuu wa maabara, ilibidi wachunguze kama kweli hizo sampuli zina Korona.

Uongozi wa Tanzania umejaa ujinga na ubabe, Mungu yupo utaisha na kusahaulika lakini baada ya kutuacha kwenye madeni makubwa ya wachina hata nchi yetu kutaifishwa na Wachina.
 
Uko sahihi RNA inayoangaliwa ni ya Virus sio antibody ya binadamu...inaweza kudetect virus popote kama alikuwepo...

Kuna uwezekano hizo samples zilikuwa contaminated kwenye process za handling.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tuna rais wa ajabu. Tumbua Tumbua aliyoingia nayo, sasa anaitumia kwa kumalizia. Anafikiria itampa kiki tena. Hovyo kabisaaaaaaa!
 
IS IT?
1. Failure of clinical procedures
2. Falure of sample handling(inawezekana pia maabara pia kuna corona)
3. Failure of Testing equipments?
4. Deliberate or cooked results?

Watanzania walioko kwenye sehemu nyeti za maabara mmezoea business as usual.
Sasa mmeingia mkenge wa Joni Pombe Goldilocks!
 
Mimi nilishangaa pale aliposisitiza kwa hiyo mapapai yote yana Coronavirus. Kwa hiyo mbuzi wote wana Coronavirus .Nilishangaa kwani binadamu mmoja akikutwa na Coronavirus maana yake binadamu wote wana Coronavirus ?Unajua Rais hataki kuamini hiyo number kubwa ya cases.
 
Ni sawa "kusimamishwa" kupisha uchunguzi ni taratibu za kawaida duniani Kote nadhani.

Hawajafukuzwa hawa watumishi....

Hivyo tuwape muda watuletee majibu.

Kwani hakuna utaratibu unaotumika kupima ubora wa machine hizo kwa kutumia wataalam wenye mamlaka hiyo wanaotambuliwa na WHO kuliko kuleta siasa kwenye hilo jambo.

Wengine bado tunakumbuka ile kamati iliyochunguza makinikia na kusema tunadai zaidi ya trillion 400 kumbe zilikuwa siasa tu hakuna kitu.
 
Nusu yao WAchagga ila hateui hata siku moja maana ana kinyongo nao, inasemekana katika kukaa kwake UDSM kuna dem wa kilimanjaro ....."
 
Kuna usemi katika kiswahili ,"kichaa kapewa rungu"
Namshauri Dr. Nyambura Moremi asepe upesi sana akafanye kazi W.H.O kama yule boss wa NIMRI. Kwa jiwe hakuna dili!
 
Kwamba anatumika na mabeberu au sio?

Hivi kwanini amekuwa obsessed na mabeberu kiasi hicho?

Kwa nni usijiulize hao mabeberu hata jambo kidogo tu wao wanapiga kelele kuhusu tanzania wakati sehem zingine wananyamaza tu?
 
Nimeona hapo mwisho wanasema shughuli za upimaji zinaendelea.
Ila hili lingetokea tu baada ya speech ya jana.Nilifahamu lazima uchunguzi upite.
Hata sifahamu kuna kosa gani hapo sasa.
Shughuli za upimaji zinaendelea kwa vifaa vile vile vya mabeberu na wapimaji wale wale ambao tayari wameonekana kuwa upande wa mabeberu. Je tutegemee majibu gani toka upimaji huo?
 
Kwani virusi akitua
Pumbavu sana kama corona hakuna Rudisha Watoto Shule, Ligi Zianze toka chato Njoo Dodoma Tupambane, Taifa La Kipumbavu Sana.
Wakosoaji/watukanaji wa JPM kazi mnayo mwaka huu
Kwa sababu mnaemkosoa hakosoleki
Wananchi mnaowatetea hawana hata habari
 
Hahaha WHO wana kazi zao tofauti kabisa na kuhakiki ubora wa vifaa tiba.
Ubora wa vifaa tiba vingi uhakikiwa na MSD nadhani, lakini navyo kama wao ndio wamevisambaza. Vingine uhakikiwa na vendors wenyewe ambao pia ni wengi.
Validation ndiyo hufanywa na watumiaji wenyewe.

Wizara inao biometrical engineers sijui kama wamehusishwa, hilo lao wenyewe wanajua wanachokifanya naamini.
Sijui hapo siasa ni ipi, ummy kutangaza tume au rais kuagiza uchunguzi?
 
kuna jamaa yangu amesema yafuatayo

1. kupitia namba za wagonjwa na vifo kupaishwa bila mpango basi labda kuna hujuma na kuna tag of war madokta wakitaka kutuaminisha raia kuwa ugonjwa umeenea sana na ni hatari sana bila lockdown tutakwisha na sote tuko njiani kuelekea kaburini na maambukizi ni makubwa sana na hapa lengo lao madokta ni wao wa ‘shine’

kila mtu awasikilize wao na huu ndo muda wao kupiga hela za posho za overtime na kutamba kwa profession yao!wanataka sote tukae chini tufuate wanayosema na wajue si wabongo wa kuwaendesha hivyo! madokta msitutishe hata sisi tuna macho na hao wagonjwa mamia mmewatoa wapi mbona huku mitaani hutawaoni?

2. aidha kuna wagonjwa wengi wanaumwa na kupona Corona bila kupimwa au hakuna maambukizi yoyote jibu ni mojawapo sababu raia hawapimwi huwezi kujua jibu sahihi hadi upimwe kwa wale wenye dalili au kwa wale walio kwenye ‘mnyororo’!

3.serikali inapenda tusiwe na hofu tuchape kazi tuzoee Corona na inapambana kuweka mambo sawa kuondokana na maambukizi na kuepusha lockdown kwa gharama yoyote (the wish of the father) versus DJ na genge lake wanaotaka chaos hata mda huu kupitia lockdown wapae kisiasa na kujipoza machungu ya kukamuliwa mamilioni ya faini ya Akwilina na kuvunjwa mikono na kulala Segerea ambako walilimishwa kunde!!

4. labda mashine za kupima Covid19 ni feki ndo maana zikatoa majibu feki ya papai na fenesi na hapa uchunguzi mkubwa sana ufanyike kila kitu kijulikane kuhusu hizo mashine na wahusika ( hujma kujaza namba za wagonjwa na ufisadi)

5. yawezekana mashine za maabara ni nzima waliotumwa wakazitest samples si waaminifu walicontaminate samples kabla hazijaingia maabara ili kumuaminisha Mkulu assumption yake kuwa watu au vifaa vya maabara ni hopeless

6. yawezekana sample zilikuwa sahihi na mashine ni nzima ila mule mule ndani Maabara mchezo ulifanyika kwa watumishi wasio waaminifu kuzicontaminate sample kabla hazijapimwa na bila mabosi wao kujua ili zilete majibu yanayotakiwa huko nje na wahusika wakuu watumbuliwe watu wapya wapate ulaji!!

katika hayo hapo juu kuna ukweli mmojawapo ni kazi ya tume kuunasa!! ‘sometimes research respondents please the researcher and give him statements of what they know he want or expect to hear!!’ hapa kuna kulishana matango pori tu!!

Guys just thinking outside the box! tujikinge na Coronavirus, tufungue mashule sasa kuepusha mimba za utotoni na kuokoa uchumi! Wahusika just think kuwaokoa Corona girls!!
 

Kama kweli nia ni kwenda kurekebisha Sasa mbona wanasema wanaendelea kupima wananchi tunaziaminije hizo mashine ambazo zimeonekana hazitoa matokeo sahihi. 7

Basi sample kwa sasa zingepelekwa hata nchi Jirani kwenye mashine zenye ubora. Kuliko watu waendelee kupimwa na mashine zinazotiliwa shaka ubora wake.
 
H


Hii dalili mbaya sana naona huu mwaka kama Ni ndoto nyakati za mfalme Herode nadhani kafika mwisho, niseme tu bye bye Herode is next mwendazake, Mungu tusimchezee tukiwa vitani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…