Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu: Wagonjwa 37 wamethibitishwa kupona virusi vya Corona na wameruhusiwa kwenda nyumbani

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu: Wagonjwa 37 wamethibitishwa kupona virusi vya Corona na wameruhusiwa kwenda nyumbani

Wewe una akili ndogo kwa hiyo unafurahia Waziri anapotangaza maambukizi mapya,unafkiri wanaoambukizwa wanataka?Acha ujinga,ndugu wenzako tunalia wanapotangazwa wameongezeka wewe unafurahia nadhani familia yako itakapopata ndio utajua adha yake,Waziri akitangaza waliopona anawapa hata wenye maambukizi kuondoa hofu na kujipa matumaini ya kupona
Unadhani wewe utasalimika kwa kutoambiwa maambukizi
 
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema hadi sasa jumla ya Wagonjwa waliopona ni 48 ambao ni kati ya Wagonjwa 108 waliothibitika kuwa na Ugonjwa huo, ila kwa sasa hawana dalili

Amesma, "Tuna vifo 10, na hivyo tukabakiwa na wagonjwa 274 na kati ya 11 tumeshawatolea taarifa kuwa wamepona. Ni kweli kama alivyosema Rais Magufuli katika watu 263 waliobaki, 108 hawana ugonjwa wowote"

Ameongeza, "Watua hao 108, hawana homa, kifua, kikohozi wala chochote, ila tuliwazuia katika vitua ili kusubiri vipimo vya mwisho na kuthibitisha kama hawana maambukizi kabla ya kuwaruhusu kwenda nyumbani."

Amesema leo wameruhusu watu 37, na kuwa vipimo vyao vimeonesha hawana maambukizi ya #COVID19. Ametoa wito kwa jamii kuwa isiwanyanyapae na kuongeza kuwa wengine 71 vipimo vyao vinasubiri siku 2-3 wataruhusiwa kurudi nyumbani
Wewe hauaminiki sana naomba Tangazo la wizara ya afya uliattach. Maana wewe sio mzalendo.
 
Unadhani wewe utasalimika kwa kutoambiwa maambukizi
Mkuu, tuambiwe Tu hata kama hawapo?

Juzi tu namba zilpokuwa zikipanda Kwa maambukizi, unazikumbuka comments za wadau hapa!

Hakuna marefu yasiyokuwa na ncha, shikilia hii kitu mkuu
 
Tatizo watu hupenda kusikia vile tu vinavyofurahisha masikio yao,ingekuwa taarifa inasema wagonjwa wapya 99+ wapatikana ungeshangilia,pole sana ,jitahidi kubadilika mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
Tulipofikia kwa kweli hali inasikitisha,yan watu wanaombea mabaya ili wapate kuponda tu!taarifa ya watu kupona kuna wengine hawataki hata kuisikia,walitaka wasikie maambukizi mapya 100!
 
Mkuu, tuambiwe Tu hata kama hawapo?

Juzi tu namba zilpokuwa zikipanda Kwa maambukizi, unazikumbuka comments za wadau hapa!

Hakuna marefu yasiyokuwa na ncha, shikilia hii kitu mkuu
Haiwezekani wasiwepo katika peak ya pandemic. Epidemiology inapingana na contention hiyo! Nitakubali kama akisema data za maambukizi baadaye. Lkn akitoa hiki kipande tu, hapana lazima wenye wahoji
 
Duh naona kaamua kuficha uso kwa kidole
 
Yani toka ugonjwa uingie mpaka ile juzi waliopona walikua ni 11 tu

Ila sasa toka juzi mpaka leo yani siku mbili tu waliopona ni 37 ! Ni maajabu haya
 
Lilikuwa jambo jema angeanza kwa kutuambia kuwa hatuna maambujizi mapya, tunasubiria tu walioambukizwa kupona, na kwa wastani kila siku wanapona wagonjwa 37.

Baada ya wiki moja aitangazie Dunia, kuwa wagonjwa wote wamepona na hatuna maambukizi mapya. Tutakuwa nchi ya 3 Duniani kuwahi kupata maambukizi, na wagonjwa wote kupona, na kisha kutokuwa na maambukizi mapya.

Baada ya hapo maisha yaendelee. Ukibahatika kuendelea kuwepo, shukrani kwa Muumba wetu. Ukiondoka, ni mapenzi ya Mungu. Tunakuombea ili apate pumziko la milele.

Sent using Jamii Forums mobile app
Umenena vyema, ila watanzania tulio wengi tuna ujinga mwingi sana zaidi ya neno lenyewe.
 
Sasa kwa nini tusifungue mashule ?Tumeshaushinda ugonjwa. Hakuna maambukizi tena. Bora kuwa mjinga maana kunakufanya uwe curious.
Aisee, fikilia kidogo tu mkuu, Leo ndio Kwanza wagonjwa wengi kutangazwa wamepona, Kwa hiyo wewe ulitarajia kianze kipi? Kati ya kufunguliwa shule na matumaini ya watu wengi kupona!!!

Funika basi huo uji....wako
 
Mwigulu nchemba aliliona hili. Watu wakambeza.
Huwezi kutoa taarifa za kuongezeka idadi ya maambukizi huku husemi idadi ya waliopona, huo ni uchawi. Kwanini uwatie watu hofu?
 
Aisee, fikilia kidogo tu mkuu, Leo ndio Kwanza wagonjwa wengi kutangazwa wamepona, Kwa hiyo wewe ulitarajia kianze kipi? Kati ya kufunguliwa shule na matumaini ya watu wengi kupona!!!

Funika basi huo uji....wako
Ukweli ni kuwa kuna visa vipya,vifo na waliopona pia. Sema wameamua kuacha kukomunicate to the public visa vipya na vifo. Tumia akili.
 
Basi sawa mzee rudi toka chato by next week wagonjwa wote watakua wamepona tunaomba shule zifunguliwe sasa.
Uzuri ugonjwa uko dar hakuna mbumbumbu hapa
 
Back
Top Bottom