Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu: Wagonjwa 37 wamethibitishwa kupona virusi vya Corona na wameruhusiwa kwenda nyumbani

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu: Wagonjwa 37 wamethibitishwa kupona virusi vya Corona na wameruhusiwa kwenda nyumbani

hao ni kweli mmewaruhusu au ndio wale walijifanya wanamkimbiza likwidi ili wamshangae kwa kuwa hawajawahi kumuona tangu wazaliwe kumbe ndio wanabonyea nae moko kwa moko!ila Likwidi na wenzio mlichotufanyia Maulana anawaona!😂😂
 
Ila kwanini hao watu wanaleta masihara ya siasa kwenye suala hatari hili la ugonjwa, ukweli nikwamba watanzania wame athirika wengi tu leo tu wa Tanzania sita 6 ma dereva wa ma lori wamepimwa na kukutwa wameathirika na covid 19 pale mpakani wa Uganda na Tz Mtukula, je wangapi wameathirika huko dar es salam, jambo la kufanya kwa sasa nikijua rate ya mambukizi katika nchi na my chuki hatua mpya za kudhibiti mambukizi, badaye ndotuangarie na kujua rate ya uponaji hili tumalize huo ugonjwa once and for all, haitatusaidia kwa sasa kujua waliopona....
Wewe nawe bure kabisa. Unaamini propaganda za Uganda za kila siku madereva wa Tanzania wana corona?Hii CORONA mtu anapiga gia Dar to Uganda, corona kweli hii?Au kuna corona mbili?

Senti bai yuzingi tecno T301
 
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema hadi sasa jumla ya Wagonjwa waliopona ni 48 ambao ni kati ya Wagonjwa 108 waliothibitika kuwa na Ugonjwa huo, ila kwa sasa hawana dalili

Amesma, "Tuna vifo 10, na hivyo tukabakiwa na wagonjwa 274 na kati ya 11 tumeshawatolea taarifa kuwa wamepona. Ni kweli kama alivyosema Rais Magufuli katika watu 263 waliobaki, 108 hawana ugonjwa wowote"

Ameongeza, "Watua hao 108, hawana homa, kifua, kikohozi wala chochote, ila tuliwazuia katika vitua ili kusubiri vipimo vya mwisho na kuthibitisha kama hawana maambukizi kabla ya kuwaruhusu kwenda nyumbani."

Amesema leo wameruhusu watu 37, na kuwa vipimo vyao vimeonesha hawana maambukizi ya #COVID19. Ametoa wito kwa jamii kuwa isiwanyanyapae na kuongeza kuwa wengine 71 vipimo vyao vinasubiri siku 2-3 wataruhusiwa kurudi nyumbani
Wanaopoana wanapewa dawa gani??
 
Sawa sawa
1587714475-picsay.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom