Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu: Wagonjwa 37 wamethibitishwa kupona virusi vya Corona na wameruhusiwa kwenda nyumbani

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu: Wagonjwa 37 wamethibitishwa kupona virusi vya Corona na wameruhusiwa kwenda nyumbani

Wote tunajua kua taarifa si sahihi nchini kwetu
 
Don't believe everything and question everything.
Wanasema suspect wa convid 19 anatakiwa kutengwa kwa siku 14, tangu ugonjwa umeingia nchini idadi ya suspect au wagonjwa ambao miili yao ina kinga nzuri ya kuweza kupambana na kupona haitangazwi au inatangazwa ndogo sana ukilinganisha na idadi ya vifo.

Je ni kweli watu hawaponi wenyewe?

Kwa nini idadi ya vifo ipewe kipaumbele sana sana na wanaopona wasitangazwe?

Karibu nchi zote duniani idadi ya watu wanaopona haitangazwi isipokuwa ya vifo tuu.
Nadhani kuna watu/kikundi cha watu wanatuhadaa sana kwenye hili janga kiasi ambacho habari za kweli huonekana ni uongo na za uongo huonekana ni za kweli.

Usiamini maneno ya watu bila kufanya uchunguzi wako mwenyewe


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Magufuli alisema wamepona 100 mbona waziri kasema wamepona 37 na sio 100!! Tumuamini nani kati yao?

Hiyo idadi ya mia itafikiwa ndani ya hizi siku 2-3 kama alivyosema Ummy. Kumbuka lengo ni kuhakikisha rais anafurahi. Wale wenye mashaka na serikali hii kupika data sidhani kama wanashaka na hilo tena.
 
Katika huu mkanganyiko baina ya sayansi na Siasa, tutavuna tulichopanda! Kuna mtu hapa anatamani kuuficha ukweli ili akwepe wajibu!
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema hadi sasa jumla ya Wagonjwa waliopona ni 48 ambao ni kati ya Wagonjwa 108 waliothibitika kuwa na Ugonjwa huo, ila kwa sasa hawana dalili

Amesma, "Tuna vifo 10, na hivyo tukabakiwa na wagonjwa 274 na kati ya 11 tumeshawatolea taarifa kuwa wamepona. Ni kweli kama alivyosema Rais Magufuli katika watu 263 waliobaki, 108 hawana ugonjwa wowote"

Ameongeza, "Watua hao 108, hawana homa, kifua, kikohozi wala chochote, ila tuliwazuia katika vitua ili kusubiri vipimo vya mwisho na kuthibitisha kama hawana maambukizi kabla ya kuwaruhusu kwenda nyumbani."

Amesema leo wameruhusu watu 37, na kuwa vipimo vyao vimeonesha hawana maambukizi ya #COVID19. Ametoa wito kwa jamii kuwa isiwanyanyapae na kuongeza kuwa wengine 71 vipimo vyao vinasubiri siku 2-3 wataruhusiwa kurudi nyumbani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mumesahau nijuzi tu tuliomba kila mutu kwa imani take mungu kadikia kilio chetu,tuzidi kumuomba mungu sana amina.
 
Mumesahau nijuzi tu tuliomba kila mutu kwa imani take mungu kadikia kilio chetu,tuzidi kumuomba mungu sana amina.
Tatizo pale Mungu anajibu kwa njia wanayoijua yeye na si walivyo tegemea hapo sasa.
 
Leo nimemsikikiliza Waziri wa Afya kwa makini sana takwimu alizozitoa za watu 37 waliopona huku watu 71 vipimo vya mwisho ili waruhusiwe ni habari inayorejesha matumani katikati ya mapambano.
Hii inatoa takwimu ya jumla watu 108 wanaoonesha matumaini tena baada ya maambukizi .Hapa tunapata picha kuwa ile takwimu aliyoitaja Rais katika hotuba yake ni takwimu sahihi inayorejesha matumani zaidi.
Tuendelee kumtanguliza Mungu kwa kumuomba atusaidie huku tukijilinda kwa kuzingatia maelekezo yote tunayopatiwa na wataalamu wa afya pamoja na Serikali yetu.
MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Back
Top Bottom