Waziri wa Ardhi na ahadi za kutatua kero za wananchi

Waziri wa Ardhi na ahadi za kutatua kero za wananchi

Bulesi

Platinum Member
Joined
May 14, 2008
Posts
14,275
Reaction score
13,929
Waziri wa Ardhi na Makazi William Lukuvi ni fundi sana wa kujitokeza kwenye vyombo vya habari na kutoa ahadi keme kem za jinsi Wizara yake itakavyotatua kero za wananchi. Lakini ukichunguza sana ahadi zake ni maneno tu na hazitekelezi. Mara nyingi hujitokeza wakati kama hivi sasa ambapo Rais ametangaza kuwa kutakuwa na mabadiriko ya baraza la mawaziri. Huko nyuma aliwahi kutangaza kuwa Wizara yake ingeweza kutoa hati za viwanja haraka sana kuondoa kero wanazopata wananchi lakini ukweli ni kwamba wananchi bado wanapata taabu sana kupata hati za viwanja vyao kwani rushwa bado imekithiri kwenye hiyo Wizara.

Hivi juzi kajitokeza tena akitangaza kuwa Wizara yake imefungua centre hapo Dodoma ambayo wananchi wanaweza kupiga Simu na matatizo yao kutatuliwa bila wao kufika hapo ofisini! Nani asiyejua kuwa wafanya kazi wa serikali huwa hawapokei simu [hata kwenye ofisi za hao mawaziri] hivyo wananchi inawabidi kwenda mpaka huko ofisini. Kuna matatizo chungu nzima ya Ardhi hapo Dar es Salaam na mengine karibu na huko anakoishi yeye Mbezi Beach lakini bado hayajapatiwa ufumbuzi kwasababu ya ufisadi wa watumishi wa Wizara.

Wakati wa mvua kwa mfano kuna sehemu hapo JANGWANI BEACH haijaendelezwa kwasababu wenye viwanja wanashindwa kujenga kwani kuna tajiri mmoja aliyeziba barabara hivyo kusababisha mafuriko kwenye sehemu hiyo. Jitihada za kutaka muhusika afungue hiyo barbara zimegonga mwamba kwasababu ya nguvu ya fedha.

Hivyo Lukuvi kujitokeza wakati hu na kujionesha kwamba anatatua kero za Ardhi za wananchi ni mbinu tu ya kutaka kumuhadaa Rais kuwa anashuhurikia matatizo ya wananchi ili abakie kwenye baraza.
 
Warasimishaji wametapeli pesa za watu wamepotea hakuna kinachoendolea yy yupo kimya
 
Hapo Mbeya eti wanapima harafu wanatoa leseni ya kiwanja kwa miaka mitatu sio Hati na wanalipia kwa control namba ule ni wizi kama wizi mwingine leseni kwenye viwanja inatoka wapi badala ya kutoa hati...watu wameibiwa kweli
 
Back
Top Bottom